11 April 2011

Mukama Katibu Mkuu CCM

*Nape, Megji, Kinana wateuliwa Sekretarieti

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

SIKU moja baada ya Kamati Kuu ya Chama Chama Mapinduzi (CCM)na Sekretarieti kujiuzulu, taarifa zilizovuja jana
kutoka kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) mjini Dodoma zilisema kuwa Bw. Wilson Mukana ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa chama hicho kushika nafasi iliyoachwa na Bw. Yusuf Makamba.

Wengine waliotajwa kuwamo kwenye sekretarieti hiyo ni Bw. Abdulahaman Kinana (Naibu Katibu Mkuu (Bara), Bw. Nape Nnauye (Katibu wa Itikadi na Uenezi), Bi. Zakia Megji (Fedha za Uchumi) na Bi. Rehema Nchimbi (Organazesheni).

Chanzo chetu ndani ya NEC kilisema kuwa wajumbe walikuwa tayari wametangaziwa uteuzi huo, lakini chanzo chetu kingine, kikadokeza kuwa pia kulikuwa na uwezekano wa kuteuliwa Jaka Mwambi, Balozi wa tanzania nchini Russia na aliyewahi kuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM katika sekretarieti ya kwanza ya Rais Kikwete.

Bw. Mukama alikuwa Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, kabla ya kuteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI na baadaye Katibu Mkuu Wizara ya Afya. Kwa sasa ni mstaafu, akiwa Mwenyekiti wa Bodi ya Magazeti ya TSN.

Bw. Makamba, aliyekuwa akiongoza sekretarieti hiyo amelazimika kujiuzulu kabla ya mwaka 2012 aliokuwa ametangaza kutoka na tuhuma mbalimbali dhidi yake, zikiwamo za kukigawa chama na kushindwa kumsaidia mwenyekiti wa chama hicho, Rais Jakaya Kikwete.

Kutokana na tuhuma hizo, juzi usiku, kiongozi huyo, sekretarieti nzima iliyo chini yake, pamoja na Kamati Kuu, isipokuwa Mwenyekiti na Makamu wake wawili, Bw. Pius Msekwa (Bara) na Aman Abeid Karume (Zanzibar) walilazimika kujiuzulu, katika kile kinachotajwa kama chama hicho kujivua gamba.

Wengine waliojiuzulu katika secretarieti ni manaibu makatibu wakuu wa CCM Bara na Visiwani, Bw. George Mkuchika, Bw. Saleh Ramadhan Feruzi na Katibu wa Itikadi na Uenezi, John Chiligati, Katibu wa Uchumi na Fedha, Bw. Amos Makala, Katibu wa Mipango, Bi. Kidawa Saleh na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mambo ya Nje, Bw. Bernard Membe.

Kwa maamuzi hayo, Rais Kikwete amepata fursa nyingine ya kuteua sekretarieti mpya na Kamati Kuu nyingine ikiwa ni takriban mwaka mmoja kabla ya uchaguzi mkuu wa chama hicho kufanyika mwakani, ikiwa ni njia ya kukinusuru chama hicho kilionesha kupauka mbele ya macho ya umma, kutokana na tuhuma mbalimbali, kubwa ikiwa ni kukumbatia ufisadi.

Waliokuwa wajumbe wa Kamati Kuu iliyoondolewa ni Bw. Makamba (Katibu Mkuu), Mkuchika - Naibu Katibu Mkuu (Bara)Salehe Ramadhan Ferouz - Naibu Katibu Mkuu (Z'bar), Dr. Ali Mohamed Shein - Mjumbe, Edward Lowassa na Shamsi Vuai Nahodha.

Pia walikuwamo marais wastaafu, Ali Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa na Dkt. Salmin Amour. Wengine ni John Malecela, John Chiligati, Amos Makala, Bernard Membe, Kidawa Hamid Salehe, Samuel Sitta, Pandu Ameir Kificho na Anna Abdallah.

Wajumbe wengine ni Rostam Aziz, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, Pindi Chana, Andrew Chenge, Dkt. Maua Daftari, Samia Suluhu Hassan, Mohamed Seif Khatib, Haji Omar Kheri, Dkt. Abdallah Kigoda, Abdurahman Kinana, Anne Makinda, Fatuma Said Ali, Zakia Meghji, Omar Yussuf Mzee, Dkt. Emmanuel Nchimbi, Ali Ameir Mohamed na Yussuf Mohamed Yussuf.

Habari kutoka Dodoma zilisema kuwa kulikuwa na juhudi za wajumbe mbalimbali, hasa wanaotuhumiwa kwa ufisadi kutaka uamuzi wa kuitema sekretarieti ushindikane, lakini baadhi ya wajumbe wa Kamati Kuu wakawa mbogo na kutoa uamuzi huo, huku wakimweleza mwenyekiti kuwa kamati hiyo wanaiacha mikononi mwaka kwa kuwa baadhi ya wajumbe ni marafiki zake.

Kwa mujibu wa habari hizo, mmoja wa watuhumiwa hao alijitetea akitaka tuhuma za ufisadi ambazo hazijathibitishwa na mahakama yoyote zisiwe kigezo cha kufanya maamuzi hayo, kwa madai kuwa hazikuwa sabau ya kupunguza kura za CCM katika uchaguzi mkuu uliopita wala kukichafua chama.

Inasemekana kuwa kigogo huyo alijitetea kuwa hata wao (watuhumiwa) walichaguliwa kwa kura nyingi kuwa wabunmge, na Rais Kikwete alipata kura nyingi kwenye majimbo yao.

23 comments:

  1. Mabadiliko yamefanyika lakini hayakidhi uhitaji uliopo sasa. Ni Changa la Macho tu. Katika hao waliochaguliwa sioni mwenye ujasiri wa kuwakabili mafisadi. HAYUPO.

    ReplyDelete
  2. ni sawa na chupa mpya "wine" ile ile!

    ReplyDelete
  3. Lakini mbona waandishi mna kiherehere mnaandika maneno yanayokisiwa kusikia radio mbao si mngojee itangazwe rasmi? Maana mpk saa 6 za usiku kikao kiliisha bila kutangazwa chochote sasa hii haraka ya nini?

    ReplyDelete
  4. mwaka wa shetani?makamba anaenda kukuna nazi Lushoto....teh eh./..teh..eh...

    ReplyDelete
  5. Mabadiliko yaliyofanywa na CCM ni mwanzo wa madiliko makubwa ktk safari ndefu ya kujisafisha na kukidhi mahitaji ya wanaccm

    ReplyDelete
  6. Tulitegemea sura mpya lakini wapi!punda ni yule yule ila sogi tu....

    ReplyDelete
  7. halafu ninyi vyama vya upinzani mlivyo na akili mbovu wakihamia kwenye chama chenu mnawapokea.
    Tunajua kansa haiponi lakini subiri utasikia wameingia chadema mnawapigia makofi, paimbafu senu.
    ACHENI HISO TAKA SIISIE HOKO MBORINI HIHIHIII!

    ReplyDelete
  8. bado hakuna matumaini kabisaaaa! Hata mnaowapatia madaraka ni mafisadi ili waendelee kuwalinda! Kama kweli mnaitakia Tanzania hii mema na hao mawaziri wote waliojipiga chini kwenye sekretarieti na pia wajiuluzu! Acheni danganya toto!

    ReplyDelete
  9. ni utaratibu tu wa uongozi bora na huru, haijaanzia na ccm, its a way forward. thanks

    ReplyDelete
  10. kamati ya sekratarieti hamujafanya vibaya kwani hiyo ndio siasa,ukiona maji yamezidi unga hauna budi kuachia ngazi,na kuwaachia wengine.ni mimi masumbuko mussa nachuchi wa mtwara mjini.

    ReplyDelete
  11. KIKWETE AANZE YEYE KUJIVUA GAMBA LA UDINI



    WIZI MTUPU HATULALI MPAKA KIELEWEKE

    ReplyDelete
  12. USHAURI WA BURE KWA CHADEMA NA VYAMA VINGINE VYA UPINZANI.

    Hakuna kuwapokea washenzi waliodumu CCM kwa muda mrefu maana damu yao ukiichanja imejaa uCCM tu; madhara yake ni kuchafua chama. Pili, ni kuwa mkiwapokea wachafu, mnawaelezaje watanzania kuwa wachafu wamebadilika?? Angalia Mh. Shibuda. alianza kidogo kuleta mgogoro baada ya kuchaguliwa kuwa mbunge. Ofcourse mlifanya vizuri kumpuuza (Namkumbuka Mh. Mdee). Aidha, tusiwasahau kuwa hao ni watu wa system (Mashushu tu)ambao hawaachi hulka zao katu. Hivi nani angeamini kuwa Prince Bagenda angerudi CCM na sasa kuwa mwakilishi wa chama ktk makongamano?? Mwaona hiyo hatari?? Washenzi hawa, waende wakaangue na wakakune nazi tu hawa. Hawafai!! Ni lazima vyama vya upinzani viwe makini na viendelee kuonyesha ukomavu wao kisiasa na si vinginevyo. Hawa ndio waliokuwa wanakitukana CHADEMA, Right?? YOU NEED TO BE SERIOUS AND WITH A VISION!!!!!!!. ALUTA CONTINUA.

    ReplyDelete
  13. Wajivue magamba yote! Waondoke pia halmashauri kuu pamoja na kuachia nafasi zao serikalini kama wanazo. Vinginevyo watajitahidi kukwamisha kila jitihada ya chama ya kujisafisha mbele ya jamii na zoezi lote litakuwa halina maana. Usiwaone hivi kina Ch-l-gat- wanacheka huko moyoni mambo yanaweza kuwa tofauti sana!

    ReplyDelete
  14. Rais wetu JK katika hili kama utafanya kweli na watanzania baada ya kutathmini wajiridhishe kuwa umelifanya kwa moyo wa dhati! utakuwa umefanya jambo kubwa ambalo watanzania watakukumbuka kwa hilo. Mambo yote yanayopigiwa kelele yatakosa nguvu na wapinzani watakosa hoja. Tunakuombea Mungu Akusaidie na tunakupenda

    ReplyDelete
  15. Hili ni changa la macho,msitupake mafuta kwa mgongo wa chupa jueni ya kuwa wa Tanzania wa sasa si wale wa mwaka 47.
    Mwanaharakati.

    ReplyDelete
  16. Kati ya hao wote walioteuliwa hakuna hata mmoja mwenye ujasiri ambao unatakiwa na watanzania wasasa labda tungewaona S.Sita au Dr Mwakyembe kati yao,hivyo kwa hilo bado mnatapatapa,mziki wa Chadema ni mnene.
    Mpenda amani.

    ReplyDelete
  17. Naomba mnapotoa maoni acheni matusi, huo sio ustaaarabu, Mhariri msiruhusu vitu kama hivi kuchapishwa gazetini sio ustaarabu hata kidogo. Ni kukosa elimu na heshima kwa wanadamu wengine. Sisi sote tunapenda kusoma kwa ustaarabu maoni ya watu wote lakini mtu mwingine anaona ni SIFA ZA HOVYO kutukana katika makala za maoni sio ustaarabu lazima heshima iwepo katika kutumia lugha safi unapojieleza.

    ReplyDelete
  18. Hapa CCM wamepiga bao kwa kweli lazima tuwe wakweli! Ni nani angedhani Kikwete angelimuacha Rostam, Chenge na Lowasa? Tena imekuwa busara kweli kuwaacha Mwakyembe na Sitta kwani kungeonekana wao ndo watakatifu. Ni ukweli usiopingika kwamba Sitta na Mwakyembe ni watu walio wazalendo lakini kuwaweka ingeliwaongezea maadui. Basi tunachotaka sasa ni kuona hali ya hewa ya kisiasa ndani ya nchi yetu inakuwa ya utulivu. Kwani ni kikundi kidogo cha watu wenye fedha waliokuwa wanayumbisha nchi kwa maslahi yao. Walikuwa wanaiendesha nchi kana kwamba haina wenyewe. Watanzania hawana shida ya kuishi na wahindi au waarabu hata wazungu. Tatizo wasifanye sisi tulipigania uhuru kwa ajili ya wao kututumia na kufilisi nchi yetu na kuuweka uhuru wa nchi yetu rehani. Waishi nasi waafrica kama wazalendo. Wafanye biashara kwa haki. Si kwa kunyonya uchumi wa nchi. Wawe matajili wa haki si kwa wizi na kudhulumu mali za watanzania kama Rostam alivyofanya kwenye shirika la umeme Tanesco. Na mtandao mkubwa wa ufisadi alionao ili kuua uchumi wa nchi kwa manufaa yake.

    ReplyDelete
  19. hata hao walioteuliwa hatuamini kama ni wasafi tutaona katika utendaji wao wa kazi habla ya uchaguzi wa chama

    ReplyDelete
  20. Kilichofanywa na CCM ni kitendo kinachofaa kuigwa na vyama vyote. Tunawajibika kama Taifa kutazama mbele tukizingatia maslahi ya NCHI yetu kwa manufaa ya watanzania wote. Mtazamo wangu......Nchi yetu haitajengwa kwa MAANDAMANO na kuwajaza wananchi JAZBA. Majukwaa ya mazungumzo yako mengi. Tuyatumie kujenga hoja zitakazotuunganisha na kutupa tija kama Taifa.

    ReplyDelete
  21. Hili joka linalojivua magamba baada ya kututafuna vilivyo, tusipokuwa makini likimaliza kazi hiyo litatumeza kabisa. Kwa muujibu wa maandiko ya Kitabu Kimojawapo cha Maandiko Matakatifu Joka au nyoka ni Shetatani! Na ukiangalia kwa makini mwenendo mzima wa hili joka linalojivua magamba, ni ushetani mtupu kwani mambo yao ni ya usirisiri sana ili kuliangamiza taifa! Angalia mikataba inayofanywa na hili joka! Hakuna anayeruhusiwa kuiona wala kuhoji. Watanzania wenzangu, Mungu ametudhihirishia wazi kuwa hawa ni mashetani na wamejitangaza wenyewe! Mwenye masikio na asikie, mwenye macho na aone na mwenye akili na ajue hili!

    ReplyDelete
  22. Ingekuwa fiti kama na mkiti jakaya angevua gamba,maana yeye ndiye aliyepalilia yote hayo,tangia mafisadi akiwa kinara hadi mipasuko ya chama,anamchukia hata sita kwa kuwa msemakweli.mawaziri wakuu wote wastaafu wamemponda ajivue mapema!

    ReplyDelete
  23. watanzania wenzangu Mungu ametujalia ufahamu wa kutosha hivyo tuseme asante kwake. Kilichotokea ndani ya CCM ni sahihi kwa upande wao, lakini ukweli uliowazi hata mbele za Mungu ni kwamba matendo ya surbodinates(wasaidizi)ni reflection ya mtawala (boss)wao. Makamba, na wenzake,pamoja na mtandao mzima wasingekuwa na dharau kwa matamshi na vitendo kwa watanzania kama wangejua kuwa boss wao hayuko nyuma yao. Ni mtazamo uliowazi na wakawaida kuwa kama bosi wako hapendi kejeli, wizi, ufujaji, ufisadi na aina yoyote ya mambo hayo hutoyafanya waziwazi na kwa kurudiarudia kwani atakuangukia. Ukiona unapata fursa ya kufanya hayo na boss anakuona na anaendelea kukusifia hata mbele za watu basi jua ya kwamba unatenda sawa na matendo yake. Kwahiyo hata hao wapya wa CCM lazima watatenda sawa na boss wao ambaye ni yule yule. Ni ili kujiridhisha zaidi kuwa kwetu sisi tunaona hawatendi vyema ila kwa boss wao nimatendo safi-hutamwona Makamba arudi kwao kukuna nazi wala Rostam na wenzake kukoma kuwachezea watanzania kupitia TANESCO na kwingineko badala yake wataenziwa kwa kazi mpya (Makamba) na Rostam kupewa tenda nyingi zaidi za serikali kupitia makampuni hewa.

    ReplyDelete