13 April 2011

Mabadiliko CCM yaibua mjadala

*Wengine wadai yalichelewa, uchafu umeganda
*Baadhi wasema ni ndio mwarobani wa ufisadi
*Yusuf Makamba afurahia kuondoka na wengi


Na John Daniel na Chales Masyeba

SIKU moja baada ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kutangaza rasmi mabadiliko makubwa
katika safu yake ya uongozi, kwa kujiuzulu sekretarieti na Kamati Kuu yake, wananchi wametoa maoni tofauti huku wengi wakitaka mabadiliko hayo yaendelee hadi serikalini.

Wakizungumza na Majira kwa nyakati tofauti jana, wananchi hao walisema licha ya mabadiliko hayo kulenga kuleta mabadiliko ndani ya CCM lakini hatua hiyo imechelewa kuchukuliwa, hadi kukifanya chama hicho kukosa mvuta kwa wananchi.

Miongoni mwa walitoa maoni ni aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama hicho, Bw. Yusuph Makamba ambaye amewataka Watanzania na wanachama wa CCM wasifadhaike kwa kujiuzulu kwao kwani 'wanarudi kwa baba ambaye amewaletea mtume mwingine'.

Mbali na hilo, Bw. Makamba alionesha furaha yake kwa kutowajibika peke yape, bali ukawa ni mkumbo wa wengi.

“Nashukuru tumetoka wote, kama tulivyoingia pamoja na tunatoka pamoja tukiwa wamoja. Haiwezekani mmoja anyoshewe kidole. Hata baadhi ya wajumbe wa mkutano huu walisema atoke Makamba, mimi nikasema tutoke wote”.

Bw. Makamba aliyasema hayo alipopewa fulsa ya kuaga kwa niaba ya wajumbe wenzake wa sekretarieti iliyojiuzulu majuzi, huku akishangiliwa na wajumbe wa halmashauri kuu ya taifa katika ukumbi wa NEC maarufu mjini Dodoma.

Kutokana hatua hiyo, Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho imewateau Bw. Wilson Mukama amechaguliwa kuwa Katibu Mkuu, nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na Bw. Makamba, akisaidiwa na Naibu Makatibu Wakuu (Bara na Visiwani), Bw. John Chiligati na Bw. Vuai Ali Vuai. Katibu mpya wa Itikadi na Uenezi ni Bw. Nape Nnauye, huku, Bw. Mwigulu Mchemba akichaguliwa kuongoza Idara ya Fedha na Uchumi. Mkuu wa Oganaizesheni ni Bi. Asha Abdallah Juma na Katibu wa Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Bw. Januari Makamba.

Kwa kutumia misemo ya biblia, Bw. Makamba alisema wanarudi kwa baba yao kutayarisha makao mapya na hata wenzao waliokuja na kukalia viti walivyoviacha watawakuta huko.

"Baba ameleta mfariji mwingine ambaye ni Wilson Mukama na wajumbe wengine. Wanachama tuendelee kuvumiliana na kujipanga ili kupata ushindi mkubwa mwaka 2015.

"Tulipoteuliwa tuliaminiwa kufanya kazi za chama na tukafanya kazi hizo kikamilifu na chama kikapata ushindi. Ndiyo, tulishinda hata kama ni kwa namna gani, lakini tulishinda, alisema.

Alisema wao wamekubali kumwaga damu kuokoa chama, kwani hawana tofauti sana na waliobaki na kwamba amefurahi kuona wengine nao wakichukua nafasi zao na kuwaasa kwamba wakitaka kutumia fagio la zamani wao wako tayari wakati wote, lakini wasipolihitaji wakiharibu watawasema.

Akizungumzia hulka ya yake ya kauli za kuudhi, alisema kwa mifano na kusisitiza kuwa kama unatukanwa na mtu mdogo aliyetumwa na mtu mzima ili kuweka mambo sawa, na yeye anamtukana kwa lengo la kusawazisha ili iwe sare.

Mkazi mwingine wa Dar es Salaam alisema, "Chama ni watu na watu ndio wanakuwa na mapungufu, kama mapungufu yao yameonekana ni vizuri waondoke kabisa, alisema akifurahia uamuzi huo wa CCM.

Aliongeza: "Suala la ufisadi upo na siyo siri, fisadi si lazima yeye achukue hela, lakini anaweza kumsaidia mtu mwingine kupata hizo hela, huo pia ni ufiasadi, kama wamepewa muda wa kuondoka wenyewe wafanye haraka wasije wakaahibishwa," alisema Bw, Ashrif Khan, aliyejitaja kama kada wa CCM.

Alisema kumekuwepo na malalamiko mbalimbali ndani ya chama hicho na kwamba hatua ya kuwaondoa watendaji hao na kupanga upya safu ni moja kati ya taratibu za CCM.

"Hatua iliyochukuliwa ni sawa kabisa na kuheshimu maoni ya wananchi, kama chama kikiona kinakwenda vibaya ni lazima irudi kwenye kati na kanuni zake," alisema.

Alisema hatu hiyo inatoa nafasi kwa walioteuliwa kuwa makini na kutothubutu kurudia makosa huku akisisitiza umuhimu wa wana-CCM kurejea itikadi za chama hicho.

Kwa upande wake Bw. Raymond Talawa, mkazi wa Kinyerezi Dar es Salaam licha ya kupongeza mabadiliko hayo alisema yamechelewa kufanywa kwa kuwa mapungufu ya kiutenaji ndani ya CCM yalianza mapema mwaka 20067/2008

"Kama hao akina Makamba wameondolewa na mafisadi wengine wamepewa muda kujiondoa wenyewe, basi hata wale wafanyakazi wazembe serikalini nao waondolewe haraka," alisma.

Alisema kumekuwa na wizi wa fedha za umma zinazotolewa na serikali kwa ajili ya miradi mbalimbali lakini wahusika wanahamishwa badala ya kuondolewa kama ilivyofanywa na CCM.

Naye Bi. Rehema Abdala, wa Kimara alisema amefarijika kwa mabadiliko hayo japo hatua hiyo imechelewa kufikiwa na kusababisha madhara makubwa kwa CCM.

"Itabidi CCM ifanye kazi kubwa kurudisha imani iliyopotea, lakini wamefanya vizuri," alisema Bi. Abdallah bila kutoa ufafanuzi wa kina.

Wananchi wengi walionyesha wazi kufurahishwa na hatu ya mabadiliko hayo huku wakisisitiza umuhimu wa Rais Jakaya Kikwete, kuelekeza nguvu kama hizo kwa baadhi ya watendaji wa serikali wazembe na wala rushwa badala ya kuishia kwenye chama.

"Ujenzi wa shule, barabara na huduma za wananchi zinaishia njiani kutokana na watendaji wa serikali wala rushwa na wazembe, rais angefanya kama alivyofanya kwa CCM kuwaondoa,"alisema mmoja wa walimu wa Chuo cha Uongozi wa Fedha IFM na kuomba jina lake kutotajwa.

16 comments:

  1. Makamba acha maneno ya kitoto, mlishinda au mliiba kura.??????

    ReplyDelete
  2. Nimefurahishwa na kitendo cha kuondoka kwa Mh.Makamba kwa sababu alikuwa amejisahau sana kupita kiasi.Istoshe ndie aliesabisha CCM kushindwa kwenye uchaguzi baadhi maeneo katika majimbo yalioko Bara na Visiwani.
    Kuanzia hivi sasa Mh.afunge mdomo wake wala asijihusishe na siasa.

    ReplyDelete
  3. Tujadili hoja na siyo matusi jamani. Maamuzi yaliyochukuliwa na Mwenyekiti pamoja na NEC ni mazuri kwa uhai chama hususani kama hao waliopewa siku 90 kufanya uamuzi watafanya hivyo. Vinginevyo wasije wakaleta mfarakano kwa ukwasi wao.

    ReplyDelete
  4. Miradi mingi iliyokuja kwa kishindo na kasi mpya wakati awamu hii inaanza kipindi chake cha kwanza imegubikwa na sura ya kifisadi na mingi imeonesha kutoleta tija. Pamoja na kujiuzuru kwa viongozi wa kifisadi huko awali, tunaomba watumishi waliopandikizwa wakati huo kuwezesha ufisadi katika ngazi ya kitaifa hadi huko wilayani waondolewe haraka.

    Tunampongeza mwenyekiti, lakini, tunamwomba anapovaa kofia ya pili ajue kuwa huko pia kuna hali mbaya zaidi. mwenyewe si anaona miradi ya kifisadi isivyokamilika na jinsi wananchi wanavyoteseka?? Au mpaka watu wazima waandamane kwa machoziii????

    ReplyDelete
  5. Sijaona mabadiliko yoyote hapo, bali ni danganya toto, ccm haijashindwa kwa sababu ya makamba bali ni kutokana na jina lake kwani watu wamelichoka jina pamoja na watu wake, wapi omary ramadhani mapuri, yule jamaa ndio alikuwa hamnazo kabisa lakini sasa analiwakilisha taifa huko mashariki ya mbali, so msishangae kusikia makamba balozi ulaya au amerika, kikwete awezi kuwatosa masela wake Membe, mkuchika rostam na wengineo kiivyo, kwani wao ndio wamemuweka hapo, hata hizo siku tisini walizo toa wabongo mtakuwa mmesahau, ww tangu lini m2 umpe nafasi ajitoe mwenyewe eti yeye fisadi which means baada ya hapo ni mahakamani kwani atakuwa kakili yeye mwenyewe kuwa fisadi, believe me no one atakaefanya hivyo and they know that, bt they try to look our mind, since watanzania wengi ni wasahaulifu siku tisini nyingi mmnoooo

    ReplyDelete
  6. Mnachofurahia hapa cha mabadiliko ni nini? Labda nambieni, Chiligati aliyetajwa hapa hakuwepo kwenye timu ya Makamba au amefanyiwa upasuaji wa ubongo na fikra zake? January anaesemwa hapa ni huyu huyu tunaemfahamu mwana wa Makamba au mwingine? kilichofanyika hapa wadanganyika ni suala la muda tu mtaanza kulalama sasa hivi. HAPA NI ZAIDI YA KIINIMACHO. Huu ni msiba wa taifa tulionao. Eti, iigwe tabia ya nyoka kujivua gamba?(labda kwa hili nampongeza mwenyekiti kwa kueleza ukweli nyoka ni nyoka hata akivua gamba hawezi kuwa mjusi). Kwani akivua gamba uhalisia wake nao atauvua, hatakuwa na sumu? MAFISADI NDANI CCM hawawezi kwisha hata siku moja. Ukweli ni kwamba atakaeuweza ufisadi wa ccm ni yule atakaeuvunja mfumo mzima wa utawala na uongozi wa ccm ambaye kwa sasa simuoni ndani ya chama hicho. MUNGU INUSURU NCHI YANGU PENDWA TANZANIA.

    ReplyDelete
  7. Huu ni usanii, hakuna kujivua gamba wala ngozi. Mafisadi wanaheshimika sana nchi hii, kwenye EPA mh. alielewana nao warudishe fedha taratibu, kwenye CHAMA wanabembelezwa wajiuzulu. Halafu mbona gamba hili halijavuliwa kichwani (MWENYEKITI NAE ANGEJIUZULU).

    ReplyDelete
  8. Mimi nadhani CCM wamebadili shati au suti toka ile iliyochafuka na kuvaa safi. Hawajajivua gamba bali wamebadili gamba. Jihadharini na chama cha ukoo. Ina maana hao akina Nape,January, na Nchimbi ndio vijana peke wa CCM au ni kutokana na majina ya baba zao. Kwa Nape, na January sioni jipya kwanza si makada wazoefu na sidhani kama watahimili mikikimikiki ya makada wazoefu ambao ndio chanzo cha vurugu ndani ya CCM. Kumbuka Nnauye bado anakumbukwa kwa utovu wa nidhamu akiwa UVCCM. Nawatakia kila la heri lakini mtu wa maana ninayemuona hapa ni Mukama pekee ingawa sina uhakika na ukada wake maana amefanya kazi serikalini kwa muda mrefu.

    ReplyDelete
  9. Siasa za CCM ni za ubabe, sikio la lao halisikii dawa kwa sababu ni wapenda madaraka mno. hali ya CCM imeharibu hata hali ya utawala sehemu mbali mbali zimekuwa ni mzigo kwa viongozi.

    Tatizo la hawa wajamaa wanajipa uhuru kupita kiasi na kujisahau kutumia sheria sijui ni kwa sababu ni chama cha mjomba shangazi watoto wa mafisadi hakuna wa kumkemea mwingine. Hapa hakuna kilichobadilika bado ni sumu ile ile tu. Hawajaweza kuwashawishi watanzania kubadilisha mawazo yao.

    ReplyDelete
  10. Nahisi kama ni kituko hicho, Yaani mtoto atafanya mambo mazuri ya kuonesha baba yake alikuwa wrong? bado sijawasoma C.C.M, Makamba mtoto atakuwa pale kama boya tu bila kufanya jambo lolote la maana kwani akifanya mazuri atakuwa anamdhalilisha baba yake kwani tutauliza mbona mzazi wake hakufanya hivyo? na labda afanye mambo ya hovyo ambayo kwa siasa za sasa hawezi kuzifanya wakati anapenda kuendelea na cheo cha Mh. Mbunge wakati waTz wakisikia umeharibu tu hawana tena mpango na wewe, mimi naona waendelee kubadili staili ya kutembea ila sio urefu wa hatua zao wala uwezo wa kukimbia badala ya kutembea kama walivyozoea. Nawapa Big Up sana ccm kwa staili yenu yakututeka sisi wananchi naona mnadhani bado tumelala ila mwisho wenu upo kama wa Laurent Bagbo. Kiulaini kama kuvua gamba

    ReplyDelete
  11. Hiyo safu mpya ni danganya tupu, maana ilishapangwa kiaina kabla ya kuvunjwa.walishajipanga na mapemwa,na mafisadi wakashauriwa watulie wakiachwa ili kupunguza jazba lakin wako pamoja,hivi rostam au lowasa waachane na jakaya,kwa akl ya haraka itawezekana?hiyo ni namna ya kutuliza mukari!wao ndo wamemwezesha urais kama hujui!hawezi kuwatosa kwa aina ya kijinga.
    Hivi anaachwa mtu makin kama sita,kisa hapendi mafisad.huyo January kapachikwa ili babake awe anamtuma kwenye kikao akaseme nini, na awe anaenda kumpa babake taarifa kikao kimeendaje,jakaya ameona asimtose Makamba kabisa,hivyo wanaridhishana chama cha ukoo.Bado chama tete,hakuna cha gamba wala nguo chakavu,inataka moyo kubadilika.hawawezi walishazoea,na watakufa jumla,maana mpasuko ktk chama ni mkubwa,na makundi yana nguvu!

    ReplyDelete
  12. Hivi JK atakuwa na ujasiri lini? Kama angekuwa jasiri wa kuleta mabadiliko bila shaka Januari Makamba asingekuwa katika safu ya uongozi. Ni yaleyale tu - URAFIKI. Uozo ni ule ule tu wa ufisadi na kulindana. JK umepata nafasi ya kuleta mabadiliko ya kweli katika CCM na nchi lakini kwa UDHAIFU umeshindwa. Hakuna la kushabikia hapo wala kupongeza.

    ReplyDelete
  13. kama ulizoea kulala na njaa basi hata aje nani hiyo njaa haitakutoka hayo mambo ya kushindwa na kushinda mnapoteza muda wenu bure umasikini ulionao usitegemee ccm au chadema watauondoa nawasikitikia sana watu mnaopoteza muda wenu kwenda kuwasikiliza wanasiasa wanaotaka kujiridhisha wenyewe na familia zao eti aje akusaidie ww tusijidanganye kila mtu ataubeba mzigo wake mwenyewe hayo maneno nakumbuka aliwahi kuyasema mzee msuya alipokuwa waziri wa fedha miaka hiyo kwa watu ambao hamkuwepo na ameyarudia tena mzee mkulo hiyo ndiyo hali halisi hakuna mtu atakae kuokota ukianguka ndugu yangu mtanzania mwenzangu sifa na elimu mungu aliotujalia watanzania na elimu tuliyopewa na mungu ni kuongea saaaaaana na uongo ulio tawala maishani mwetu umasikini hautaondoka ng;ooooooooooo kwa mtaji huo watu wanachokitumia ni kauli ya kula na kipofu usimshike mkono mwaka wa komomonyoka unakuja na haupo mbali vita wala vurugu haitatokea mungu ni mwema tunaliomba hilo wenye nchi wapo sio nyie mnaopiga kelele

    ReplyDelete
  14. Huo wimbo wa CCM yaani ubeti wa kwanza Ufisadi, ubeti wa pili Tatizo ni MFUMO ubeti kuropoka na wa nne ni hue sasa wa Mukama nitawaondoa Mafisadi. Tutaona wamuulize mwigizaji mwanasheria Shitambala yaliyompata kwao Mbeya uyole. Watu wakipata nyadhifa hupenda kutamba hooooo nitafanya hike, nitafanya kile, utadhani mkolon aliyekuwa anasema nimevumbua mlima Kilimanjaro.

    ReplyDelete
  15. JK Umeshindwa kabisa,hata wanaosuport mabadiliko siyaoni,meghiji ,chilighati wote walishindwa posistion zao.leo tena yaleyale.haya january mtoto wa nyoka ni..,Mnauye wale wale hamana chochote ulichofanya ni danganya toto naomba ujiudhuru tu nawewe.sioni hata unatupeleka wapi.

    ReplyDelete
  16. Mabadiliko haya ni fule ya CCM kuchanja mbuga. Kuna vyama ambavyo havifanani kabisa na mazingira ya Tanzania vinajifanya viko tayari kuchukua nchi ili vituletee mambo ya kuiga nchi za ngambo zinazowafadhili. Watanzania tutabaki na CCM yetu iliyotuwezesha kuishi kwa amani na utulivi kuliko nchi yeyote Afrika. Hongera CCM kwa kujisafisha

    ReplyDelete