Na Said Njuki, Arusha
TIBA ya Mchungaji Ambilikile Masapila 'Babu' wa Loliondo imezidi kukumbwa na kizungumkuti baada ya wasafirishaji wa wagonjwa kuendelea kukiuka taratibu
zilizowekwa na serikali, ikiwamo kusafirisha abiria kwa malori.
Habari zilizopatikana jana kutoka Samunge zinaeleza kuwa foleni zimeongezeka kutokana kuachiwa kwa magari mengi tofauti na matarajio.
Kutokana na hali hiyo huduma za Babu si zimeanza kudorora tena kwa sababu ya kuzidiwa na wagonjwa baada ya kuruhusiwa watu wengi zaidi kufika Samunge.
Habari zilizopatika kutoka Samunge zimeeleza kuwa hali hiyo imesababisha viwanja vya Mchungaji Masapila kujaa watu upya sababu kubwa, ikiwa ni serikali kuachia wagonjwa 800 kwa siku moja badala ya 300 kutoka Kituo cha Bunda, kinachopitisha wagonjwa wote wa Kanda ya Ziwa na nchi jirani za Uganda, Rwanda, Burubdi na DRC.
Mkuu wa Wilaya Ngorongoro, Bw. Elias Wawa Lali alithibitisha hali hiyo alisema serikali imezuia zaidi ya malori 10 katika kijiji cha Yandito umbali wa kilomita sita kutoka kwa Babu, hivyo wagonjwa na watu wao wanalazimika kutembea kilomita 12 kwenda na kurudi katika malori yao kufuata kikombe.
“Tumezuia malori kusafirisha abiria kuja huku kwa babu, lakini jambo la kushangaza hakuna anayejali agizo hilo na badala yake lori hizo zinaachiwa na kuja hadi hapa kinyume na sheria. Tumewazuia sasa wanatembea kilomita sita kwenda kupata kikombe cha babu na kurudi kilomita sita kujiunga na malori yao tena. Mbaya zaidi malori hayo yanatoka mkoani kwetu,” alisema Mkuu wa Wilaya.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Bw. Thobias Andengenye alipoulizwa juu ya tuhuma hizo zinazooneka kulenga askari wa jeshi hilo, alisema hajapata taarifa juu ya tuhuma hizo lakini hatasita kuwachukulia hatua za kisheria wale wote watakagundulika kuhusika na tabia hiyo.
“Nashukuru kwa kunijulisha hilo, tutafuatilia na tukigundua ukiukaji wa sheria zilizowekwa hatutasita kuwachukulia hatua kali askari watakaogundulika kuhusika na tuhuma hizo…nipe nafasi nishughulikie’alisema Kamanda Andengenye jana.
BIN ADAM NI WAZITO KUBEBEKA NA KUELEWA, KWELI WATU WANAUMWA NA KILA MMOJA ANAJIONA YEYE NI MGONJWA KULIKO MWINGINE.BAADA YA KUONA WATU WANAFURIKA KWA BABU UWEZO WAKE KWA SIKU WAGONJWA 2,000 SERIKALI IMEWEKA UTARATIBU WA KILA NJIA KUPITISHA IDADI MAALUMU SASA WATU NI WABISHI WAKIPATA MATATIZO NI RAHISI KUILAUMU SERIKALI KOSA LAO NINI? MFANO JUZI KUMTELEKEZA MAITI NYUMBANI KWA DC YEYE KAKOSA NINI?IMETANGAZWA WAGONJWA WALIOPO PALE BUNDA NI 4,500 ITACHUKUWA SIKU 15 KUMALIZIKA,HICHO KITUO KIMOJA JE,HIVYO VITUO VINGINE SITA VINA IDADI GANI? LAKINI MTU BADO ANAKWENDA KUJIPANGA PALE HUKU WAKIDAI LAZIMA WAENDE MNAENDA WAPI? WAKATI HUYO BABU KESHASEMA IDADI YA WAGONJWA KWA SIKU TUWE WASIKIVU NA KUWE NA MIPANGO MAALUMU NA MUWE WASTAHMILIVU.
ReplyDelete