Na Rehema Maigala
MSICHANA wa kazi za ndani Khadija Athumani (27), mkazi wa Kimara amehukumiwa kifungo cha miaka saba jela kwa kosa la kuiba mtoto wa kiume jina
Victory Charles (4).
Kabla ya hukumu hiyo, ilidaiwa na Mwendesha Mashitaka Bw. Mtani Magoma mbele ya Hakimu Bw. Athumani Nyamlani kuwa Februari 18, 2009 mshitakiwa alimuiba mtoto wa mwajiri wake Charles Aloyce.
Mshitakiwa anadaiwa kumuiba mtoto huyo alipomfata kituo cha basi ili kumrudisha nyumbani kutoka shule.
Shahidi wa pili ambaye ni dereva wa basi la shule alidai kuwa alimshusha mtoto huyo kama ilivyo kawaida na alimkuta pale kituoni dada wa mtoto huyo akiwa amesimama na wavulana wawili ambao ni wauza viatu.
Alidai kuwa kwa kuwa wao walikuwa wanamsubiri mzazi mwingine kwa ajiri ya kumchukua mtoto wake, walimuona mshtakiwa anaongea na vijana hao huku na mtoto huyo akiwa hapo hapo.
Mshitakiwa huyo alisema alimfata mtoto kituoni ambako pia walitokea vijana wawili wakamwambia kuwa wanamuomba mtoto huyo.
'Waliniambia kuwa wanamuomba mtoto ili wanipe pesa lakini mimi niliwakatalia kwani nilikuwa siwaelewi, baada ya muda mfupi mtoto aliomba anataka kwenda kujisaidia nilimruhusu baada ya hapo sijamuona tena," alidai mshitakiwa huyo.
Baada ya Hakimu kusikiliza usahahidi wa pande zote mbili alimuuliza Mwendesha Mashtaka kama mshtakiwa anakosa linginenaye akajibu kuwa hakuwa nalo, lakini apate adhabu kali ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hiyo.
Baada ya hukumu hiyo kusomwa ilisikika sauti za ndugu yake mtoto wakilia kwa uchungu wakidai kuwa, haisaidii kitu hata angefungwa kifungo cha maisha ni bora tungeona maiti yake kuliko kusoma misa ya wafu bila ya kujua mtoto wetu amekufa au la.
No comments:
Post a Comment