20 April 2011

Watafiti watakiwa kuishirikisha serikali

Na Rehema Mohamed

WATAFITI nchini wametakiwa kutumia mfumo shirikishi wanapofanya tafiti zao kuanzia ngazi ya awali ili iwe rahisi kuzitumia pale zinapohitajika.Hayo yamesemwa
Dares Salaam jana na Bw. Arthur Mwakapugi wakati akiwasilisha utafiti kuhusu matumizi ya tafiti katika masuala mbalimabli nchini hasa kwa watunga sera.

Bw. Mwakapugi alisema mfumo huo ni pamoja na kuwahusisha wadau mbalimbali ambao hutumia tafiti hizo katika kazi zao.

"Pale ambapo tunafanya tafiti zetu tunatakiwa kushirikisha asasi mbalimbali pamoja na wadau wengine ili iwe rahisi kutumika badala ya kufanya wenyewe alafu tunaweka katika makabati," alisema Bw. Mwakapugi

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Uchumi na Jamii (ESRF), Dkt. Bohela Lunogelo alisema ufinyu wa bajeti unachangia watafiti kutoshirikisha wadau wengi.

Dkt. Lunogelo alisema katika nchi nyingi zinazoendelea bajeti ya utafiti haifiki hata asilimia moja ya bajeti ya nchi husika wakati nchi zilizoendelea huwa asilimia hiyo au zaidi.

Katika hatua nyingine, alisema uelimishaji wa wananchi kuhusu matokeo mbalimbali ya tafiti zinazofanyika kutachangia watu kutumia tafiti badala ya kuzihifazi maofisini.

No comments:

Post a Comment