*Amtaka naye ajivue gamba CCM
*Adai amekuwa akitetea mafisadi
Na Moses Mabula, Tabora
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dkt. Willibrod Slaa amesema Rais Jakaya Kikwete
anapashwa ajivue gamba CCM kwa kuwa yeye na washirika
wake wameshrikiana kufanya ufisadi ndani ya Serikali.
Dkt. Slaa alisema hayo katika mkutano wa hadhara wakati akihutubia wananchi kwenye
Uwanja wa Chipukizi mjini Tabora.
Alisema kuwa Rais Kikwete amekuwa akiwatetea maswahiba wake wanaotuhumia kuiingizia
Serikali hasara ya mamilioni ya shilingi licha ya kuelezwa bayana lakini amekuwa
akikaa kimya bila kuwachukulia hatua zozote zile za kisheria.
"Kikwete naye inafaa ajivue gamba ndani ya CCM kwa kuwa naye ni muhusika, asiwadanganye
Watanzania kwamba eti CCM imejivua gamba wakati naye ni gamba katika CCM," alisema
Dkt. Silaa huku akishangiliwa na umati wa watu na kuongeza:
"Huyu naye Chiligati eti anawatangazia Watanzania kwamba amewapa siku tisini wale wote wanaotuhumiwa na ufisadi, wawe wameondoka wenyewe ndani ya CCM na kumwacha Mkuu wake wa kazi Rais Kikwete kumtangaza naye awe ameondoka ndani ya hizo siku tisini" alisisitiza Dkt. Slaa.
Akimgeukia Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Saidi Mwema Dkt. Slaa alisema
kwamba achague mambo mawili siasa au upolisi.
Alisema kuwa Mkuu huyo wa Polisi amekuwa akikipigia debe Chama Cha Mapinduzi na
kusahau kazi aliyotumwa na Watanzania ya kulinda usalama wa watu na mali zao lakini
hivi sasa amegeuka kuwa mwanasiasa ndani ya Jeshi la Polisi.
Alieleza kwamba iwapo ameshindwa kufanya kazi ya Upolisi ni vyema
akawatangazia Watanzania haraka kuwa yeye ameshindwa kazi hiyo na mwanasiasa.
Kuhusu watu wanaotuhumiwa kuwa mafisadi Dkt. Slaa alimtaka Rais Kikwete kuwachukulia
haraka hatua za kisheria na kuwafikisha mahakamani na kwamba kama hawezi basi naye
aondoke madarakani kwa kuwa ameshindwa kufanya kazi kwa wananchi waliomchagua
kuingia madarakani.
Kuna wasi wasi na maneno ya Slaa. Kila wakati hutaka Rais ajiuzuru, ina maana gani? Kwani hajui au hajakubali kuwa kulifanyika uchaguzi na mshindi akapatikana. Kuna kila sababu ya kumtambua Slaa kama mpenda madaraka na mtu asiyekubali kushindwa. Jipangeni kwa uchaguzi ujao.
ReplyDeleteNina wasiwas na mtoa maoni wa kwanza kama anauelewa sahihi wa siasa na mwelekeo wa nchi yetu. Kuna haja ya watu kufikiri sana kabla hawajachangia. tatizo kuu la nchi hii ni rais Jakaya mrisho kikete. Anatakiwa atafute pakukimbilia na aondoe aibu zake. mtaji wake wa wajinga kumchagua ndo unaompa shida. amewkabidhi kazi marafiki zake wasio na ufanisi.
ReplyDeletemtoamada wapili unaweza kazi tukupe?
ReplyDeleteMtoa mada wa tatu hujui mtoa mada wa pili alichoandika kwenye maoni. Naunga mkono mtoa mada wa pili mfano mzuri ni wa Mubarak wa Misri alishindwa kuziba ukuta mapema sasa wanataka kujua alikusudia au? Mubarak hoi!
ReplyDeleteMtoa mada wa kwanza ni TABULA LAZA,misibishane naye kwani nahisi anatoka familia za kifisadi,hajui shida na dhiki za watanzania
ReplyDeleteMi najiuliza Endapo hawa mafisadi watatoka CCM watakwenda wapi na mtandao wao?
ReplyDeleteHapa kuna hatihati ya network yao kuhamia upinzani kiaina. Maana msicheze na hela jamani.
Sijui
hiyo ndiyo kazi unayostahili.kutoa siku kila kukicha. kwa hiyo rais ajiuzuru ili tuitishe uchaguzi mwingine kwa gharama za nani? je kwa gharama hizi hizi za walipa kodi walalahoi? wewe kama unao ushahidi wa nao mafisadi kwa nini haufungui kesi mahakamani? hivi kila kesi ya mafisadi inatakiwa kufunguliwa na rais? Slaa unesha mfano kwa kumfungulia kesi angalau fisadi mmoja ambaye una ushahidi ili tukuamini kweli unayo sema unamaanisha hivyo moyoni mwako. mbona kila siku kazi yako ni kutaja majina tuu hauendi japo kufungua kesi moja maana chama chako kinajinasibu kuwa na wanasheria waliobobea. onesha mfano mzee ili 2015 tukuchague.
ReplyDeleteHaya sasa1 Twambie wee mtoa maoni wa pili kuwa katika uchambuzi wako unaousifia sana UMEGUNDUA kuwa tatizo kuu la nchi hii ni Raisi. Hongera sana. ILA umejisahau kuwa wewe mweyewe ni tatizo kwa chi kwani hata wewe ni fisadi. Mwizi ni mwizi, awe wa vitu vidogo au vikubwa. awe anajulikana au hajulikani. wewe ni fisadi masikini na unawashambulia mafisadi matajiri. Wivu ndo tatizo lako kwani unatamani kuwa na makubwa na huyapati. Kuanzia leo jua kuwa tatizo kuu la watanzania ni watanzania wenyewe. Hivyo hata Slaa tunayemlilia,hatatusaidiaan atakutana na yaleyale kama hatutakubali kubadirika sisi wote. Maana yangu ni kwamba HAKUNA MSAFI. Ukweli unauma lakini ndivyo ilivyo. Imefika wakati sasa tuseme ukweli.
ReplyDeleteNyote mliochangia mpo sawa, endeleeni kuchangia kwa kuwa ninahakika mnauchungu na nchi hii, HONGERENI SANA
ReplyDeleteWee wa wapi? Unajua kilichomtokea Mbeki kule South Africa? Alishindwa kazi akaleta watu wakamwambia apishe kwa maslahi ya nchi. Si huyo anaheshimika.
ReplyDeleteSlaa anafaa kuwa rais wa Tanzania kwani anatetea tabaka la wanyonge na kuwaweka wazi mafisadi wanaofiris nchi yetu. hongera DR SLAA
ReplyDeleteHaya malumbano ya Slaa sijui yataisha lini maana kuna wakati unaona kama mtu wakati mwingine kama akili imeruka hatuelewi na ile bei yake ya mfuko wa cement kwa sh 5,000 ndio ataongozea nchi..kwa sababu ana hamu haasa ya urais ngoja tumuombe raisi apumzike hata mwezi mmoja ili apewe kiranja slaa ni kama mtoto unupomkataza kitu anarudiarudia apewe kiti hata kwa wiki moja apigiwe saluti na mizinga 21 ataridhika ndio arudi uraiani.
ReplyDeleteHaya malumbano ya Slaa sijui yataisha lini maana kuna wakati unaona kama mtu wakati mwingine kama akili imeruka hatuelewi na ile bei yake ya mfuko wa cement kwa sh 5,000 ndio ataongozea nchi..kwa sababu ana hamu haasa ya urais ngoja tumuombe raisi apumzike hata mwezi mmoja ili apewe kiranja slaa ni kama mtoto unupomkataza kitu anarudiarudia apewe kiti hata kwa wiki moja apigiwe saluti na mizinga 21 ataridhika ndio arudi uraiani.
ReplyDeleteMambo ya CCM chadema yawahusu nini, mana mbona chadema mlifanya uchaguzi CCM haikusema chochote hii ni ishara kuwa Chadema wanaiogopa CCM, na wanafanya juhudi kuwa kuichafua ili waiondoe, Propaganda hazisaidii sana, la mana jengeni imani kwa wananchi ili wawachague, lakini kazi yenu kuwaladanganya wanafunzi, kumbukeni 75% ya watanzania wanishi vijijini na ndiko CCM inakopata nguvu.
ReplyDeleteAsilimia kubwa ya watu wanaoitetea ccm na serikali ya mkwele hawajitambui na hawajui nchi inaelekea wapi,wake up
ReplyDeleteTanzania inahitaji mtu anyeweza kuwatumikia watanzania na awe MWAMINIFU na MKWELI. Hatuangalii anatoka chama gani au dini gani. Kwa maana hiyo Slaa ameshashindwa kwani sifa hizo HANA. Histira yake imemshitaki kwa mambo matatu muhimu. "HANA UAMINIFU"
ReplyDelete1. Slaa,alishindwa kuwa mwaminifu kwa kushindwa kutimiza ahadi alizozitoa mbele ya Mungu, mbele ya Kanisa na mbele ya watu waliohudhuria misa ile. Kama mtu anasema hiki leo kwa Mungu, na kesho anambadirika hata Mungu, je atawatii watu na kuwa mwaminifu kwao? Tafakari.
2. Slaa, baada ya kuacha upadre alioa.Lakini akashindwa kutekeleza hata kile kiapo chake na mkewe. Hata kama hawakuoana kanisani, lakini ndoa ni ndoa. Leo hii mke huyo anahudumiwa na nani? Slaa alimdanganya mkewe. Tfakari.
3. Slaa, hakuishia hapo. Amediriki hata kuchukua mke wa mtu mwingine. Mme bado anaishi. Jamani tutafakari. Je leo hii kiapo anachotaka kuapa kukaa ikulu kweliameshaongoka? Atkuwa mwaminifu kweli? Tafakari.
Ukweli unauma lakini UNAWEKA HURU.
Sidhani kama angekuwa hata na nguvu ya kumpatia kiongozi mwingine siku 90, kwani kwa maoni yangu na mtu yeyote mwenye akili timamu ni kwamba Slaa angekuwa anfahamu UDHAIFU wa mtu mwingine, kwani hata yeye yuko vile. Nadhani anaijua biblia. yesu anasema "Mtu anyemwacha mwenzi wake wa ndoa, naye atakuwa afanya dhambi kwani atasababisha mwenzie atende uzinzi"