12 April 2011

CCM washangilia kuondoka Makamba

*Wala na kunywa Dodoma kujipongeza

Mwandishi Wetu

WAFANYAKAZI wa CCM Makao Makuu Dodoma wamejipongeza kwa kula na kunywa kwa kile wanachosema ni kufurahia kuondolewa ofisini kwa
aliyekuwa Katibu Mkuu, Bw. Yusufu Makamba jambo walilokuwa wanalisubiria kwa muda mrefu.

Baadhi ya wafanyakazi hao waliokutwa na Majira katika maeneo mbalimbali ya starehe mjini Dodoma wakizungumza bila kutaka majina yao yaandikwe gazetini, walisema kwamba furaha yao hiyo imenogeshwa zaidi na kuondolewa kwa sekretarieti nzima ambayo ilikuwa mzigo mkubwa, sio kwa chama tu bali pia kwa watumishi wa chama.

Walisema uwajibikaji wa watumishi ulipungua kutokana na maamuzi binafsi ya Bw. Makamba ambayo kila mara yalitolewa bila kuzingatia taratibu za utumishi na ajira. Kwamba baadhi ya watumishi walihamishwa kibabe kwa amri yake kwa sababu binafsi.

"Kuondoka kwa uongozi wa Makamba kwetu ni sawa na kuzaliwa upya, ndio maana tuko hapa tukiburudika kwa furaha na kupongezana. Kuondoka kwao haikuwa kazi ndogo kwani tayari baadhi ya wajumbe walishapewa kiasi kikubwa cha pesa ili kukwamisha na kuhujumu uamuzi wa kuwaondoa madarakani," alisema mmoja wa wafanyakazi hao.

Mwingine alisema, "Ni kweli chama kimepoteza mvuto kwa wananchi kiasi kwamba hata sisi watumishi tunapata shida na aibu kila tunapoumbuliwa na kukejeliwa na wananchi mitaani. Hatuna la kusema wananchi wanapokilalamikia chama, lakini viongozi kwa sababu za uswahiba wao usio na kikomo wanakauka au kutoa matamko ya ajabu dhidi ya wanachama na wananchi kwa ujumla."

Walisema ni matarajiio yao kwamba sasa baada ya kujiuzulu kwa wajumbe wa Kamati Kuu, chama kitakuwa na sura mpya na safu makini ya uongozi, ambayo pamoja na mambo mengine itajenga mshikamano na kuelekeza nguvu na kasi zaidi katika kupambana na ufisadi jambo ambalo ndio maradhi yanayodhoofisha afya ya CCM.

Aidha kwa nyakati tofauti watumishi hao walishauri kwamba uamuzi mgumu uliochukuliwa na chama usiishie kupanguana katika nafasi za uongozi tu, bali utazame na kuwamulika hata wale wanaoendeleza makundi yanayokigawa chama kwa lengo la  kutafuta uongozi wa juu, kwani wanakwaza juhudi za utekelezaji wa ahadi na ilani ya chama.

Pia walikumbushia kurejewa kwa dhamira ya rais ya kutenganisha mambo ya siasa na biashara. Tumeona wafanyabiashara walivyotuvuruga, hivyo sasa ni muda mwafaka kujitoa mikononi mwao na kurejea kwa wananchi wakulima na wafanyakazi ambao ndio wenye chama, alidokeza mwingine.

16 comments:

  1. mwandishi wewe ni muongo, na kama hujajuwa wenzako walikuwa wanafurahie kujivua gamba kwa maana ya kufanikiwa kuwaingiza watoto wao warithi uongozi baada ya baba zao kustaafu. msema kweli ni sumaye yeye alitupa siri na kututhibitishia tulichokuwa tunahisi;
    kuwa huu ni ufalme wa kisultani wa kuwarithisha watoto wao uongozi. huu ndio unabii na utabiri siyo mnajimu shkhe.

    ReplyDelete
  2. Mwandishi hajazungumzia viongozi wa chama, kazungumzia wafanyakazi walioajiriwa makao makuu ya CCM, jaribu kuwa makini kabla ya kutoa shutuma.

    ReplyDelete
  3. Kwa kweli mimi sijaona gamba lolote lililovuliwa. Hata hivyo wamejivua gamba lakini nyoka ni yule yule. Mbona watu ni wale wale kumwondoa Yusufu Makamba wakati tayari kwenye safu yuko Januari Makamba umefanya nini? Ina maana makada wote wa CCM Tanzania hakuna watendaji wengine ila hao hao kina Makamba? Mtoto wa nyoka naye ni nyoka. Sasa Tanzania tunakaribisha ufalme wa kisultani? Ukija kwa Mh. Kikwete yuko Ridhiwani Kikwete nyuma yake. Yusufu Makamba yuko Januari Makamba nyuma yake.Mzee Mwinyi nyuma yake kuna Dr. Hussein Mwinyi. Hii ina maana gani jamani hakuna Watanzania wengine waliojaliwa kuzaa watoto na wakasomesha pia? Tukiingia kwenye Kamati Kuu hakuna mvuto wowote ni hao hao kina Kinana, Wassira, Ana Abdala, Zakia Meghji mbona wameshazeeka mpaka akili hao? Bado kabisa CCM tuna kazi kubwa mbele yetu. Chama hiki kijitakase mpaka Mikoani na Wilayani chama hakiko tu Makao Makuu maana watendaji wengi wa Mikoani wamewekwa na Yusufu Makamba kwa maslahi yake. Kina Mama wengi waliopewa U-Katibu au wa Mkoa au wa Wilaya ni wa darasa la saba I-Q yao ni ndogo. Wafuasi wa Yusufu Makamba wanatakiwa waondoke naye vinginevyo tutegemee tena mpasuko ndani ya chama.

    ReplyDelete
  4. Labda atuambie ni mtoto yupi wa kiongozi karithishwa kama vile Mbowe alivyorithishwa na mkwewe Mtei uenyekiti na wkati wengine walipotaka kugombea ikawa nongwa. Mtoto wa makamba alishinda ubunge kwao Lushoto,mtoto wa mwinyi yupo siku nyingi kwenye uongozi,ridhwani alishinda kwenye uchaguzi kwa kugombea na sio kuteuliwa,ni vyema mkahoji familia ya mtei,ndesamburo na mbowe kwenye chadema. hao wazee wanahitajika sana huko na ndio maana zito alipotaka kugombea uenyekiti ilibidi wazee wa chadema wamsihi aachane na hilo. UZEE DAWA

    ReplyDelete
  5. Namuunga mkono msemamaji aliyepita. Watu hawaelewi na kufuata mkumbo wa kile wasichokielewa. Hii ni sawa na, "Funika kombe mwanaharamu apite"

    ReplyDelete
  6. Kwa kweli mimi sijaona gamba lolote lililovuliwa. Hata hivyo wamejivua gamba lakini nyoka ni yule yule. Mbona watu ni wale wale kumwondoa Yusufu Makamba wakati tayari kwenye safu yuko Januari Makamba umefanya nini? Ina maana makada wote wa CCM Tanzania hakuna watendaji wengine ila hao hao kina Makamba? Mtoto wa nyoka naye ni nyoka. Sasa Tanzania tunakaribisha ufalme wa kisultani? Ukija kwa Mh. Kikwete yuko Ridhiwani Kikwete nyuma yake. Yusufu Makamba yuko Januari Makamba nyuma yake.Mzee Mwinyi nyuma yake kuna Dr. Hussein Mwinyi. Hii ina maana gani jamani hakuna Watanzania wengine waliojaliwa kuzaa watoto na wakasomesha pia? Tukiingia kwenye Kamati Kuu hakuna mvuto wowote ni hao hao kina Kinana, Wassira, Ana Abdala, Zakia Meghji mbona wameshazeeka mpaka akili hao? Bado kabisa CCM tuna kazi kubwa mbele yetu. Chama hiki kijitakase mpaka Mikoani na Wilayani chama hakiko tu Makao Makuu maana watendaji wengi wa Mikoani wamewekwa na Yusufu Makamba kwa maslahi yake. Kina Mama wengi waliopewa U-Katibu au wa Mkoa au wa Wilaya ni wa darasa la saba I-Q yao ni ndogo. Wafuasi wa Yusufu Makamba wanatakiwa waondoke naye vinginevyo tutegemee tena mpasuko ndani ya chama.

    ReplyDelete
  7. Kwa kweli mimi sijaona gamba lolote lililovuliwa. Hata hivyo wamejivua gamba lakini nyoka ni yule yule. Mbona watu ni wale wale kumwondoa Yusufu Makamba wakati tayari kwenye safu yuko Januari Makamba umefanya nini? Ina maana makada wote wa CCM Tanzania hakuna watendaji wengine ila hao hao kina Makamba? Mtoto wa nyoka naye ni nyoka. Sasa Tanzania tunakaribisha ufalme wa kisultani? Ukija kwa Mh. Kikwete yuko Ridhiwani Kikwete nyuma yake. Yusufu Makamba yuko Januari Makamba nyuma yake.Mzee Mwinyi nyuma yake kuna Dr. Hussein Mwinyi. Hii ina maana gani jamani hakuna Watanzania wengine waliojaliwa kuzaa watoto na wakasomesha pia? Tukiingia kwenye Kamati Kuu hakuna mvuto wowote ni hao hao kina Kinana, Wassira, Ana Abdala, Zakia Meghji mbona wameshazeeka mpaka akili hao? Bado kabisa CCM tuna kazi kubwa mbele yetu. Chama hiki kijitakase mpaka Mikoani na Wilayani chama hakiko tu Makao Makuu maana watendaji wengi wa Mikoani wamewekwa na Yusufu Makamba kwa maslahi yake. Kina Mama wengi waliopewa U-Katibu au wa Mkoa au wa Wilaya ni wa darasa la saba I-Q yao ni ndogo. Wafuasi wa Yusufu Makamba wanatakiwa waondoke naye vinginevyo tutegemee tena mpasuko ndani ya chama.

    ReplyDelete
  8. MAKAMBA HAJAIGARIMU CCM PEKE YAKE BALI NA TAIFA KWA UJUMLA...HAFAI HATA KUWA KATIBU WA KIJIJI...

    ReplyDelete
  9. Gamba amelivua Yusufu Makamba, Amelivaa January Makamba,Ifuatayo ni orodha ya magamba yaliyobaki mwilini mwa CCM;John chirigati,Zakhia M,Nape Mnauye,Abdalah Kigoda,PinaChani,Stivin Wasira,Kinana(hivi faili lake la urahia liliisha patikana toka uhamiaji)?,Anna Abdalah,Pius Msekwa, Orodha ya magamba kwa ujumla ni kubwa na kwa Ujumla CCM imebaki na 95% ya magamba yake.

    ReplyDelete
  10. nimepata taarifa kuwa rostam azizi ana watu wake sita katika safu mpya ya uongozi, ikiongozwa na january makamba.....poleni ccm

    ReplyDelete
  11. Mtajibeba mwaka huu safu ndio hiyo imeishapangwa sasa subirini kitimtim kinachofuata.

    Waswahili wanasema toa boriti jichoni mwako kabla ya kutoa kibanzi jichoni mwa mwenzako. Ya CCM ni kibanzi tu lakini ya Chadema ni boriti. Kutwa kuwasema kina January na wengineo wanaosimama wenyewe kugombea lakini yenu ya watoto na ndugu za viongozi wanaopewa viti vya dezo hamuyaoni, na Mwenyekiti anayeekwa na baba mkwe pia hamuoni. Sasa sijui ndio yale yale ya nyani haoni......!

    ReplyDelete
  12. Muda na wakati umewadia kwa ccm kuwa chama cha upinzani, uzalendo umekwisha kabisa miongoni mwa viongozi wa ccm! Unaposhuhudia watoto mpaka wa shule za msingi wanaandamana, gharama za maisha kupanda, thamani ya sh ya Tanzania kushuka, kutumika hovyo kwa mali asili za taifa kusikokuwa kwa maslahi ya watanzania na mendeleo endelevu, dini kuingilia siasa, watu kuwa wakaidi, wasiowpenda wa kwao! NI DALILI CHACHE TU ZINAZOADHIRIA KUWA WATANZANIA TUNAENDA KUKOSA UVUMILIVU KUONA CCM INAYONUKA IKICHEZEA MAISHA YA WANYONGE.

    ReplyDelete
  13. ROSTAM KIBOBKO BADO KAPENYEZA WAFUASI WAKE CC, CCM KAZI MNAYO MKIMUUZI KING MAKER RA, ATAKIULIA MBALI CHAMA CHENU, SUBIRINI SASA EL, RA, EC, WANAKWENDA MSITUNI KMA CCM MTAPONA, CCM NDIO BASI TENA. NA HUYU ZAKHIA MEGJI SI NDIE ALIYEIDHINISHA PESA ZA EPA? MBONA MMEMPA NAFASI CC AU KWASABABU MAMAMKWE WA MHESHIMIWA SANA? ALIWAONGOPEA DELLOITE N TOUCH (AUDITING FIRM}, KUWA PESA ZA EPA ZIMETUMIKA KWA USALAMA WA TAIFA THEN IKAGUNDULIKA ZIMECHOTWA NA KAGODA YA KINA RA, CCM MBONA MNACHEKESHA, KWELI NIMEAMINI MGONJWA KIKATAA DAWA ANAUTAKA UMAUTI, BURIANI CCM, HAMTAPATA NAFASI NYINGINE TENA YA KUJIVUA GAMBA. HUYO JANUARY ANA NINI ZAIDI YA WATU MAKIN I KMA SITTA, MWAKYEMBE, MWANDOSYA, SALIM A SALIM, BADO JK UNAWARIDHISHA MAFISADI, WATAKUYUMBISHA SANA.BORA CCM IFE WATANZANIA TUKOMBOKE.

    ReplyDelete
  14. Mpambano utakuwa mtamu kati ya EL Vs Nape Nnauye, then Nape vs UVCCM mafisadi watoto, EL,RA vs JK Tutaona mengi kuelekea 2015. ADUI MUOMBEE NJAA, AKISHUKA SI TUNAPAA". CCM HAIKUWA KUVUA MAGAMBA BALI KUMVUA MAKAMBA. mola mlinde JK wetu n TZ Ameen.

    ReplyDelete
  15. CCM imeshajipachika yenyewe jina la JOKA. NDULI akivijua gamba ni mbaya zaidi.

    ReplyDelete
  16. KWA CHENGE, LOWASA NA ROSTOM-KWA VILE MZEE MAKAMBA ANAFURAHI KWAMBA AMETOKA NA WENGI NDANI YA KAMATI KUU, BASI KWA NJIE HAMNA LA KUFAYA NI KUFANYA MCHEZO MMOJA WA KUFA KWA WENGI NI HARUSI, KWA MAANA HIYO KWA VILE CHENGE UNAWAJUWA WATU WOTE MLIOGAWANA MSHIKO WA RADA NA WEWE WAWEKE HADHARANI NAO WATOLEWE NDANI YA CHAMA, PIA MZEE LOWASA KWA VILE UNAWAJUWA WALE WOTE WALIOKUKATIA MSHIKO WA RICHMOND BASI USIKUBALI KUFA PEKE YAKO, WATAJE WOTE NAO WATOLEWE CCM, NA PIA MHESHIMIWA ROSTOM WEWE NDIYO JEMBE, WALIME WOTE UNAOWAJUWA KUWA ULIWAPA MSHIKO ILI KUPITISHA DEAL ZAKO, USIKUBALI KWENDA MWENYEWE, HUONI MAKAMBA, NI LAZIMA UWE SHUJAA USIFE KIVYAKO KUFA NAO WOTE WALIOPOKEA FEDHA KUTOKA KWAKO

    ReplyDelete