13 April 2011

Carroll aing'arisha Liverpool

LONDON, Uingereza

MANCHESTER City juzi ilipata kipigo cha mabao 3-0, dhidi ya Liverpool katika Uwanja wa Anfield.Katika mechi hiyo mshambuliaji, Andy Carroll alikuwa mwiba
mchungu kwa kufunga magoli mawili na kuiweka timu ya Roberto Mancini, katika hati hati ya kufuzu michuano ya Ligi ya Mabingwa.

Na kocha Mancini, alikiri kuwa mshambuliaji wake Carlos Tevez, atakosa kucheza katika mechi ya Jumamosi ya nusu fainali ya michuano ya kuwania Kombe la FA dhidi ya Manchester United, baada ya kuumia msuli kwenye mechi dhidi ya Liverpool na kufanya atolewe baada ya kupita dakika 15.

Mancini alisema baada ya mechi: "Hatukucheza katika dakika 20 za mwanzo wakati ambapo Liverpool ilicheza vizuri.

"Lakini hii ilikuwa ni makosa. Ilikuwa ni makosa yangu."

Kocha huyo wa kiitaliano alikataa kuelezea, lakini pia ana mashaka na Tevez.Alisema: "Ni tatizo la msuli na ninafikiri itakuwa ni ngumu kwake kucheza Jumamosi. Sidhani kama atacheza."

Carroll alifunga goli lake la kwanza la Liverpool, katika umbali wa yadi 25 na kisha alifunga jingine kwa kichwa huku goli jingine likiwekwa kimiani na Dirk Kuyt.

Alisema: "Ilikuwa ni siku nzuri kwangu, kupata goli langu la kwanza kwa Liverpool na matokeo mazuri.

"Nafasi ya tano hakuna utata, kwa wachezaji tulionao, kwa jinsi tunavyocheza.

"Goli langu la kwanza lilikuwa zuri kwangu. Nilipiga vizuri. "Bao la pili lilikuwa langu kabisa."

No comments:

Post a Comment