Na Edmund Mihale, Dodoma
RIPOTI iliyotolewa jana na Mkaguzi Mdhibiti Mkuu Fedha za Serikali (CAG), Bw. Ludovick Utouh imebaini kuwepo kwa matumizi mbaya ya fedha, Serikali Kuu na katika
baadhi ya halmashauri na kushauri kufanyika kwa ukaguzi maalumu katika maeneo hayo.
Akizungumza na waandishi wa habari Mjini
Dodoma jana, Bw. Utouh aliyataja maeneo
yanayotakiwa kuwekewa mkazo kwa kuyafanyia
ukaguzi maalumu ni Serikali Kuu za Serikali
za mitaa na ufanisi na utambuzi.
"Matokeo ya ukaguzi uliofanyika Juni 30 mwaka
jana yanonesha kuwa kumekuwepo na upungufu
kidogo katika ubora wa hati zilizotolewa kwa
serikali na taasisi zake ikilinganishwa na
mwaka uliopita," alisema Bw. Utouh.
Alisema kuwa katika ukaguzi huo kwa eneo la Serikali kuu waligusia kwa undani mambo muhimu kama usimamizi wa Sheria za Fedha za Umma ya mwaka 2001 na Usimamizi Sheria ya
Manunuzi ya 2004.
Alisema kuwa maeneo mengine, ni utunzaji wa
vifaa na mali uwekezaji mabovu wa kumbukumbu
na ukosefu wa nyaraka na hati za malipo
mamlaka ya mapato ambapo walijikita katika
kukagua masuala ya ukaguzi ya miaka ya nyuma
, makusanyo ya maduhuli na misamaha ya kodi.
Kwa upande wa hazina, Bw. Utouh alisema kuwa
walikagua hazina kwa kungalia deni la taifa,
Mtumizi ya serikali misaada kutoka kwa
wafadhili, matoleo ya ziada, madeni, dhamana,
mali ambazo hazipo kwenye leja na fidia kwa
waathirika wa hali mbaya.
"Eneo hili limechangia sehemu kubwa ya ripoti yangu aidha mafungu yote yalikaguliwa yameonesha udhaifu katika usimamizi wa Sheria Usimamizi wa Fedha za Umma ya 2001 na Usimamizi wa sheria ya manunuzi ya mwaka 2004,"
No comments:
Post a Comment