21 March 2011

Wayne Rooney ataka mwanaye awe kama Ronaldinho

LONDON, Uingereza

WAYNE Rooney ana mpango wa kumpeleka nchini Brazili katika shule ya soka mtoto wake, Kai wakati akiwa na umri miezi 16 tu.Mshambuliaji huyo wa
Man United, Rooney mwenyewe alipitia katika shule ya soka na anataka kumfanya mwanaye aje kuwa mzuri kama akina, Ronaldinho nyota wengine wa Brazil ambao walianza kugunduliwa na kulelewa vipaji tangu wakiwa wadogo.

Katika shule hizo hulenga kuwaendeleza, kushirikiana na kujichanganya na watu wengine.

Rooney mwenye miaka 25, alipata habari za kozi hiyo akiwa Cheshire na hakupoteza muda kutaka kuomba nafasi kwa ajili ya Kai.

Chanzo kilisema: "Rooney ameanza kumshawishi mwanaye Kai kuingia katika soka na alishamnunulia jezi ya timu yake ya utotoni Everton, na jezi kadhaa za United na timu ya taifa ya England. Amekuwa akimnunulia mwanaye Kai mpira katika umri mdogo na anatumaini mwanaye huyo atarithi uwezo wake."

Kai mara kadhaa amekuwa akienda na wazazi wake kwenye mechi za soka. Mama yake Coleen mwenye umri wa miaka 25, amekuwa akienda naye kwenye mechi kadhaa za Mashetani Wekundu katika Uwanja wa Old Trafford.

No comments:

Post a Comment