Na Damiano Mkumbo, Singida
WATU wawili wamekufa papo hapo baada ya kugongwa na lori wakati wakiwa kwenye pikipiki waliyokuwa wakisafiria katika eneo la Kibaoni barabara ya
Singida Dodoma.
Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida Bw. Nyigeta Wankyo watu hao waliokufa juzi saa 8:00 mchana ni Ramadhani Jumanne (25), mkazi wa Mwenge mjini hapa aliyekuwa akiendesha pikipiki hiyo na abiria wake Jerome Rafael (30) wa Mtaa wa Kibaoni, wote ni wafanyabiashara.
Bw. Wankyo alieleza kuwa watu hao waliokuwa wakitokea Kibaoni kwenda mjini wakiwa na pikipiki hiyo Na T536 BNX SANLAG, waligongwa baada ya bomba lililokuwa likitumika kuvuta gari hilo kukatika na kupoteza mwelekeo kisha kuwagonga watu hao na kufa papo hapo.
Kaimu Kamanda huyo alisema kuwa gari hilo T613 ARA lililokuwa likiongozwa na Petro Chimwaga (45) wa Vingunguti Dar es Salaam ambalo lilikuwa linavutwa na lori T809 likiwa na trela T132 ATS Scania la Dereva Musa Kopa(50) wa Mburahati Dar es Salaam.
Alisema madereva wote wawili walikamatwa na polisi na walitarajiwa kufikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.
No comments:
Post a Comment