*Wahoji iweje JK, Pinda wamzuie kutekeleza sheria
Na Suleiman Abeid, Shinyanga
KATIKA hali inayoashiria ni ya kumtetea waziri wa ujenzi nchini, Dkt. John Magufuli baadhi ya wananchi wameeleza kusikitishwa na mashambulizi yanayoelekezwa kwake na
wakuu wake wa kazi kutokana na agizo lake la bomoabomoa katika maeneo ya hifadhi ya barabara.
Wananchi hao wamesema kauli za hivi karibuni zilizotolewa na Rais Jakaya Kikwete na Waziri Mkuu, Bw. Mizengo Pinda kupinga agizo lililotolewa na Dkt. Magufuli kuhusiana na suala la ubomoaji wa majengo yaliyojengwa ndani ya hifadhi ya barabara zimetolewa bila ya kutumika kwa busara.
Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti jana mjini Shinyanga, wananchi hao wamedai kauli hizo za Rais Kikwete na Bw. Pinda zinaweza kumuathiri kisaikolojia Dkt. Magufuli kwa njia moja ama nyingine na kusababisha ashindwe kutekeleza majukumu yake mengine kikamilifu.
Walisema agizo lilitolewa na Dkt. Magufuli ni suala la kisheria, na kwamba alichotekeleza yeye ni kuweka mkazo ili sheria hiyo iweze kuheshimiwa, na hali hiyo inatokana na sehemu kubwa ya Watanzania kujenga utamaduni wa kutoheshimu sheria za nchi zilizopo hasa katika sekta ya ardhi.
Wananchi hao walisema hata kama ungekuwepo umuhimu wa kumtaka Waziri Magufuli kupunguza kasi ya utekelezaji wa agizo lake hilo, basi busara ingetumika zaidi kwa kulijadili suala hilo ndani ya kikao cha Baraza la Mawaziri ambalo mwenyekiti wake ni Rais Kikwete mwenyewe badala ya kumkemea hadharani.
Kwa kweli Dkt. Magufuli hajatendewa haki, alianza kushambuliwa na kiongozi mkuu wa shughuli za serikali bungeni, Bw. Pinda, tena kibaya zaidi yeye aliamua kwenda kumshambulia mbele ya wapiga kura wake jimboni Chato, sasa kwanini Bw. Pinda hakupeleka suala hili ndani ya Baraza la Mawaziri, ambapo angemuomba huyu bwana apunguze kasi yake?
Mimi binafsi sipingani sana na Bw. Pinda au Rais Kikwete, lakini kinachonisikitisha ni jinsi ya hawa viongozi wetu walivyoamua kumzuia mbele ya kadamnasi, wengine tumehisi serikali haiko pamoja katika utekelezaji wa majukumu yake, maana haya ni mambo ya ndani wangekaa na kuelezana huko badala ya utaratibu uliotumika.
Kwa kawaida Magufuli anafahamika, kila anapokabidhiwa wizara hupenda kuona sheria inafanya kazi yake, hata kule kwenye uvuvi alibadili hali ya mambo, watu waliheshimu sheria, kwa vile hakuna wakubwa huko wanaofanya kazi ya uvuvi mdogo mdogo hakuna aliyepiga kelele.
Sasa leo kwenye bomoabomoa imekuwa tatizo, na nafikiri wakubwa na vigogo wengi hapa nchini wamejenga katika maeneo ya hifadhi, ndiyo maana anapigwa stop kubwa, kwa kweli hajatendewa haki, maana rais naye juzi kakomelea msumari kwenye kauli za Pinda alizotoa kule wilayani Chato,†alieleza Bw. Shija Stephen mkazi wa Maganzo.
Kwa upande wake mmoja wa makada wa CCM mjini Shinyanga ambaye hata hivyo hakupenda kutajwa gazetini alieleza kushangazwa kwake na kauli ya Rais Kikwete iliyodai kuwa Bw. Magufuli anatumia ubabe zaidi katika utekelezaji wa shughuli zake.
Kada huyo alisema kauli hiyo haikuwa nzuri kutolewa na kiongozi wa ngazi ya juu nchini, na kwamba huenda ikasababisha watu wenye tabia ya kuvunja sheria waendelee kufanya hivyo kwa vile wataamini yupo atakayewatetea na kwamba ameagiza walipwe fidia pale wanapovunjiwa.
“Binafsi sijafurahishwa na kauli ya Rais Kikwete kudai kuwa Bw. Magufuli anatumia ubabe katika utekelezaji wa shughuli zake, hii wizara ya ujenzi pamoja na ile ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi zinahitaji watu kama Bw. Magufuli, ukitumia siasa zaidi katika wizara hizi ni wazi utakwama.
Wapo watu wamekuwa wakitumia uwezo wao wa kifedha kufanya lolote wanalotaka hata kama linapingana na sheria, sasa leo tishio la Bw. Magufuli limewashtua alipoelezea dhamira yake ya kubomoa majengo yote yaliyojengwa ndani ya hifadhi ya barabara wakaona na wao wataguswa.
Bw. Magufuli alianza kwa kuonesha mfano wa uvunjaji wa ofisi za Tanroads jijini Dar es Salaam, jengo lilijengwa ndani ya eneo la hifadhi, alitumia busara, maana huwezi kuvunjia watu wengine wakati wewe mwenyewe jengo lako limejengwa kimakosa, na alisema hata kama ni jengo la CCM atabomoa, hii imetisha watu,†alieleza kada huyo wa CCM.
Aidha baadhi ya wananchi hao wameonesha wasiwasi iwapo Bw. Magufuli ataendelea na utekelezaji wa majukumu yake mengine ya kikazi kwa vile anaweza kuogopa kukemewa tena na viongozi wake wa ngazi ya juu, kitu ambacho kitasababisha akae ofisini na kusubiri kupokea ujira wake wa mwezi kama walivyo baadhi ya mawaziri.
Hata hivyo, Bw. Magufuli mwenyewe amemthibitishia Rais Kikwete kuwa ataendelea kutekeleza majukumu yake na kusimamia sheria bila kulegea na kwamba daima ataongozwa na kiapo chake alichokula alipokuwa akiapishwa kushika wadhifa huo.
Wakati huohuo Wizara Ujenzi imekanusha madai ya gazeti moja kuwa gharama za ujenzi wa barabara zimepanda baada ya Magufuli kuingia katika wizara hiyo hadi kufikia sh bilioni 1.4 kwa kilometa moja ya lami.
Katika taarifa yake iliyotumwa kwa vyombo vya habari jana, wizara hiyo ilitoa ufafunuzi kuwa utekelezaji wa ujenzi wa barabara ya Iringa hadi Dodoma yenye urefu wa kilometa 260 ambao umegwanyika sehemu tatu ili kuhakikisha utendaji kazi.
Ilieleza kuwa sehemu ya kwanza ni ujenzi wa barabara ya Iringa hadi Migori yenye urefu wa kilomita 95.1 sehemu hiyo imejengwa na mkadarasi SIETCO kwa gharama ya sh. bilioni 84 ambayo ni wastani wa sh. milioni 886 kwa kilomita moja ya lami na inategemewa kukamilika Januari 13, 2014.
Ilieleza kuwa sehemu ya pili ni kutoka Migoli hadi Fufu escarpment yenye urefu wa kilomita 93.8 na itajengwa na mkandarasi SIETCO kwa gharama sh. bilioni 73.61 ambayo ni wastani wa sh. milioni 785 kwa kilomita moja ya lami na inategemewa kukamilika Januari 13, 2014.
Ilieleza sehemu ya tatu ya ujenzi huo ni Fufu hadi Dodoma yenye urefu wa kilometa 70.9 inajengwa na Mkandarasi China Communication Construction kwa gharama ya sh. bilioni 64.33 ambayo ni wastani wa sh. milioni 907 kwa kilomita moja na inatarajiwa kukamilika Aprili 26, 2013.
Taarifa hiyo iliyotiwa saini na Msemaji wa Wizara hiyo, Martini Ntemo ilieleza kuwa gharama za ujenzi huo ziko chini sh bilioni 1 kwa kilomita moja kwa lami tofauti ha gharama za miradi mingine ambayo iko zaidi ya sh. bilioni 1 kwa kilomita.
Waheshimiwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Waziri Mkuu, hawakumtendea haki Waziri wa Ujenzi, Dr John P. Magufuli mbele ya wananchi. Swala hili wangezungumza kwenye "Baraza la Mawaziri".
ReplyDeleteusitetereke hao wakina jk na pinda wasikutishe hao serikali imewashinda wamelewa na madaraka. FANYA KAZI KWA MUJIBU WA SHERIA
ReplyDeletemwambieni aje chadema?mnataka nn sasa na akitoka tu ccm hamtamsikia tena na msijidanganye kuwa wenu chadema wapuuzi wakubwa nyie nchi hii hamuipati hata kwa nguvu ya kucha au kikombe cha babu kwani masikini ni nyie tu?hata mi nimasikini nani kaja kuomba chai kwenu?msijidanganye hata kidogo hamna bao
ReplyDeleteHizi ziara za rais katika wizara zina zidi kutuonyesha udhaifu wa uongozi alionao JK na serikai yake. Kuwakemea mawaziri sio kujisafisha na ombwe la uongozi! Hapa natoa mifano ya vituko vya JK katika ziara zake: Mfano ni hili la kusema shule ziunganishwe sijui na mkongo wa internet! Shule zetu hazina madarasa wala umeme wala kompyuta wala wataalamu wa kompyuta sasa huko kuunganishwa si utani mkubwa na fedheha kwa walimu wanaolipwa shs laki 2?
ReplyDeleteIngine mpya aliitoa jana! Eti Tanzania tuanze kufikiria kujenga kinu cha kufua umeme wa nyuklia! Hiki nikichekesho kikubwa kwani kwa nchi yenye uzembe mkubwa kiasi cha mabomu kupasuka mara mbili kwa uzembe Mbagala na Gongo la Mboto, wakidai ni bhati mbaya, ingekuwa ajali ya nuklia watanzania na nchi jirani wangekua wameteketea. Wanamchukulia JK serious watahudhunishwa na makaripio yake kwa Dkt Magufuli lakini kwa mtanzania kama mimi hayo yote JK anayofanya ni usanii tu! Nchi imeshindwa kutumia gesi iliyonayo nyingi inazungumzia nuklia ambayo hata huko ulaya wanafikiria kuachana nayo. JK kukaa kimya mara nyingine ni busara!
Dkt Magufuli naona wanao mpango wao wakuwkukufunga gavana usije ukawa tishio kwa urais 2015! Watanzania tunajua yupi ni mkweli na yupi anatupaka mafuta kwa mgongo wa chupa! JK angekua na uchungu na nchi hii asingeliwaachia mafisadi kama Chenge, Lowassa, Karamagi, Rostam na Manji waifilisi nchi! Kujidai kuwahurumia wananchi wanaobomolewa ni machozi ya mamba huwa analia huku anameza! JK karibuni tutasema Usaii mwisho!
ReplyDeleteMsitake kujipendekeza musikilize raisi alichotamka,waache ubabe,wawalipe fidia wanaowavunjia,na pia wawape muda wa kubomoa
ReplyDeletesasa hapa kosa liko wapi?Mtu kakaa miaka zaidi ya 40 hata wewe hujazaliwa leo unakuja kunambia nivunje ndani ya masaa 48 kweli huo ni uungwana?ndi maana akmwambia aangalie muda wa kuhitajika hiyo barabara kama itajengwa baada ya miaka 5 mpe muda wa miaka 2 huyu mtu wa kubomoa sio ghafla,pili baadhi ya wabomoaji wanatumia ubabe hata muda wa kutoa vitu vyako huna mvunjaji sio Magufuli ni wale walioagizwa ni wababe,wakati mwingine wanakuja usiku kuvunja hiyo ni sawa?tatu JK kasema hii sheria mpya ya kuongeza hifadhi ya njia imeongezwa wakati mtu alishajenga pale sasa ifatwe sheria sio kwa watu tuu hata serikali nayo ifate sheria nani alianza kuwepo pale?Acheni fitna za uongo kwa kuwa wewe halijakukumba unasema tuu Raisi hajasema sheria isifatwe ila kwa taratibu zake hv unapobomoa tuu ni kwa faida ya nani au manufaa yapi? kwani hakuna kona ktk njia?Tusitake kujidai kaonewa ila kaambiwa ukweli yeye kweli askari wa mwamvuli,mchapa kazi,na jasiri lakini awe makini.Mfano kwake kavunja hata nyumba yake je,hiyo njia ishajengwa mpk leo? Na hata Pinda alimwambia ifanywe utafiti ijulikane fungu lililopo la kuwalipa ndio bomoa iwe kwa idadi ya hao watakaobomolewa huwezi vunja nyumba Nchi nzima zaidi ya nyumba laki moja wakati kwa sasa fungu ulilonalo ni lakutosha njumba elf 20!! Izingatiwe na pia kuwapa muda ukimvunjia aende wapi ni mpk umpatie kiwanja na malipo tusiwe kama mavuvuzela ilimradi tunasema tuu.
Magufuli kaza buti baba hata YESU hakuwaogopa Mafarisayo. Tupo nyuma yako kwa maombi. Mungu anakulinda baba.
ReplyDeletemiafrika ndo tulivyo
ReplyDeletenchi hii haina rais wa nchi ila yupo wa familia ya wezi
ReplyDeletekweli kuongoza tanzania ni kazi kubwa. kama mawazo na uelewa wa watu ndio huu,kazi ipo. yaani hata kauli ya kawaida kabisa isiyohitaji kufika chuo kikuu iliyotolewa na rais nayo haieleweki? kweli kazi ipo. ila ifike mahala watu tuzipe nafasi akili zetu na kuacha majungu na chuki binasfi, maana mimi binasfi sidhani kama rais kakataa nyumba zisivunjwe, alichosema yeye hata huo uvunjaji ufuate sheria na taratibu siyo kuropoka tuu eti nawapa saa 48 muwe mmeshavunja hizo nyumba wakati hiyo bara bara ndiyo kwanza ipo katika uchambuzi yakinifu hata bajeti yake haijulikani itatoka wapi, je huo ni uungwana wa wapi? na kwa manufaa ya nani? acheni majungu yaani mnamchukia rais hata kama akifanya jambo zuri kiasi gani? wakati mwingine lazima muangalie na mazingira siyo tuu kufuata sheria. hivi hata nyinyi katika maisha yenu kila siku huwa mnafuata sheria?
ReplyDeleteMagufuli huwezi kufanya kazi katika mazingira na mahusiano kama hayo na wakuu wako wa kazi.Kwanza JK alitakiwa ama amuwajibishe Waziri mkuu kwa kitendo chake cha kumshambulia waziri aliye chini ya mamlaka yake; ama basi amuwajibishe Magufuli kwa kumwomba ajiuzulu kwa utendaji kazi wa kibabe. JK na Pinda wote wamekosea; na ili Magufuli awe shujaa katika suala hili, anapaswa kujiuzulu ili kumfundisha JK na Pinda utawala bora.
ReplyDeleteKAMA JAKAYA KIKWETE NA PINDA WAKE WANGEKUWA NWAKWELI WANGEANZA KUWASHAMBULIA HADHARANI ROSTAM AZIZI NA LOWASA MAANA WAO NDO WANAOONGOZA NCHI KWA KUMTEKA KIKWETE NA KUFANYA WATAKAYO.SHELI ZA WAKUBWA KAMA KOBIL SHELI,HOTEL NA MAGHOROFA KWENENYE HIFADHI YA BARABARA NDO CHANZO CHA JK NA PINDA KUMVAA MAGUFULI HADHARANI .SONGA MBELE BABA MAGUFULI HAO VIBARAKA WA MAFISADI HAWANA JIPYA
ReplyDeleteUNAPOCHANGIA WACHA USHABIKI WA KULETA KUJIFURAHISHA TOA USHAHIDI WA WAZI NI SHELI IPI AU HOTELI AUGHOROFA LIPI NA WAPI?WACHA KUPANDIKIZA CHUKI ZEMBE.RAISI KASEMA VIZURI TUU,MAGUFULI KAMA MSOMI NA INJINIA AFIKIRIE MARA MBILIMBILI UTAMVUNJIAJE MTU KIRAHISI WAKATI UJENZI WAKE WA KUDUNDULIZA MIAKA ZAIDI YA 4 KAJENGA NYUMBA YA VYUMBA 6 NA MUDA HUO WOTE MLIKUWA WAPI WEWE MKURUGENZI WA HALMASHAURI AU WAKAGUZI WA ARDHI NA NANI KATOA KIBALI!! TOFAUTI NA LEO WATU WANAJENGA JENGO LA GHOROFA 12 KWA MWEZI UJE UMVUNJIE KAMA KIMBUNGA? NIA YENU MAGUFULI AKASIRIKE ACHUKIE ILI AJIUZULU HALAFU AMKOMOE NANI? ANA AKILI TIMAMU ANAJUWA ALIKOTOKA NA ALIPO NA ANAPOKWENDA. KAENI KIMYA KALAGABAHO
ReplyDeleterais huyu amechoka kuwafurahsha mafsad na sasa anataka kutufurahsha wananch kwa kaul za unafk zilizojaa unafk. nadhan anaendelea na mchezo uleule wa kutafuta cheap popularity lakn bahat mbaya watanzania tumemshtukia.n aibu rais zuzu kujfanya anamfokea magufuli huku akiwa n mtuhumiwa namba moja richmond na tuhuma nyngne lukuk.huyu rais ameshndwa kumwajbsha lowasa na rostam ambao n mafsad papa lakn kwa maguful anajkomba. yeye si saiz ya magufuli na n aibu kujifanansha na mwanaume jasr kama magufuli.
ReplyDeletetanzania ina bahati mbaya sana ya kuwa na rais pmb kama huyu. yaan anaongoza nch kwa hsia kulko sheria? huruma hii ndio imeifanya nchi kuendelea kuangamia. mikataba ya huruma,mafsad wanaonewa huruma,wafujaj wanaonewa huruma, nk. nch hii bla wanaume jasr kama maguful hatufk. ole wet kwa rais huyu wa ajabu
ReplyDeletekatba na sheria ndio zinaongoza nch na s huruma na visingzio vya ajabu ajabu.kikwete angekuwa na akl angeiga ya maguful na s kumkosoa.maguful angekuwa rais nchi hii isingefka hapa.rais hewa nchi hewa.
ReplyDeleteAcha pumba zako mchangiaji wa mwisho na wawili juu yako ni mtu mmoja uwe na nidhamu na adabu 3.49 mpk 3.59 anajifanya watu tofauti huwezi mwita Raisi pmb kama wkt wewe ndio pumba kabisa, yaani chizi maarifa
ReplyDeleteKAULI MBIU YA CCM WAKATI WA UCHAGUZI MKUU WA 2010 ILIKUWA ''ARI ZAIDI, KASI ZAIDI NA NGUVU ZAIDI'.
ReplyDeleteDr. John Pombe Magufuli anazingatia kaulimbiu hiyo.
SASA INASHANGAZA, Wakubwa zake wanamkataza kuonyesha kasi zaidi!
Nina hakika sasa, Mawaziri wengine watalala usingizi wa pono kwa sababu Boss haeleweki!?
Je, Watanzania mnajua maana yake ya kasi zaidi? Je, si wote tuliona 'Ari mpya, Kasi Mpya na Nguvu Mpya' zilikotufikisha!?
TAFAKARI.
Rais hahitaji au hapashwi kwenda kila wizara kuona wanavyotenda kazi.Mawaziri ndiyo wanapashwa kumpa taarifa za kazi zao katika Baraza la Mawaziri ambalo huwa wanakutana kila baada ya muda uliopangwa.Inaonekana Rais amekosa kazi ofisini kwake! Je Makamu wa Rais wake ana kazi gani lakini. Kunywa kahawa ofisini kwake!!!
ReplyDeletekubwa hapa n kuwa utendaj wa maguful unamuumbua kikwete.sasa maguful anaonekana wa maana kjulko hata rais mwenyewe na ndio maana kikwete anamwonea wvu. jtahd kuwa mwanaume kama maguful kwa utawala wa sheria na kuepuka utawala wa kiswahba na uanamtandao na watu wote watakuheshimu. n bahat mbaya kuwa tuna rais pmb kama wewe. rais punguan ataiteketeza nchi
ReplyDeletekikwete hv unajckiaje kuendelea kuwa ikulu pamoja na uzuzu wote huo? hv unafkr ikulu n ya kla m2 kias kwamba hata vilaza kama wewe wanaeza kukaa? naomba kama unajua umuhmu na utukufu wa ikulu utoke haraka uwapshe wanaume watawale kwan ww huelewek. lait ungekuwa na angalao chembe ya akl na utendaj wa maguful nch isingekuwa hapa. ole wa taifa ambalo rais wake n kituko kama huyu. ole wetu watanzania
ReplyDeleteHakuna mtu aliyekamilika..ndivyo Mungu alivyopenda kutuumba. Ndio Maana kila siku tunamwomba Mungu atujalie na kutuondolea mapungufu yetu.
ReplyDeleteDr Magufuli anafanya kazi nzuri ya kusafisha uozo uliosababishwa na watangulizi wake. Wananchi tunaomba tumuunge mkono na kumwombea asitetereke. Pia tunamwombea asiwe legelege na asimwonee mtu bali atekeleze kazi zake kwa mujibu wa sheria. Utu uwepo lakini kwa mipaka na atueleze sababu za kuweka utu huo. Mfano anaweza kusema tutatathmini na kulipa fidia, kisha tutabomoa nyumba hizi baada ya mwaka mmoja. Muda huo watu wautumie kupata makazi mengine. Baada ya hapo, hata akitoa masaa 48 ni sawa kabisa.
Wakuu wameshauri uwajibikaji wa pamoja ktk baraza lao, hakuna tatizo na hilo. Tatizo ni udhalilishaji wa mchapa kazi mbele ya wale anaowaongoza.
Kuna watu wameropoka kulipa mabilioni ya wananchi kwa mafisadi bila kikao cha baraza la mawaziri lakini kimyaa hadi leo.
Wengine hawajulikani hata wanafanya nini katika wizara zao, nadhani wanasubiri tu miaka 5. Hawajitumi wala kuondoa kero za wananchi. Mheshimiwa mmoja ameamua kulia na ufisadi wa kugawa nchi hadi walalahoi wake wanakufa kwa ukata huku wakikatazwa kuchimba madini. Huyu sijui kama atadumu, manake anataka kupunguza ulaji wa Mafisadi.
Nchi yetu ni ya ajabu sana. Ukiiba hela kidogo utatafutwa hadi Chunya na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria. Ukiiba mabilioni (vijisenti), unaombwa na mkuu wa nchi urudishe kidogo benki, na unahakikishiwa msamaha. Aibu tupu!
Kero za wananchi ni huduma mbovu (elimu, afya,miundo mbinu, nk), kupanda kwa gharama za maisha (maisha magumu) na kutokuwa na njia za kupata kipato halali. serikali ikizipunguza kero hizi wala hutasikia watu wanaandamana, labda kwa kuunga mkono maendeleo na kukazia mabadiliko mazuri.
ni ajabu kuwa leo hii hata kikwette anadrk kusmama mbele ya mwanaume kama magufuli na kumkosoa.naulza,amepata wap ujasr mkubwa kias hcho? amejpma kias gan mpaka kudrk kumkosoa maguful? anajckiaje anapoojfanansha na mwanaume huyu ambaye taifa linamheshimu kwa misimamo yake yenye manufaa kwa taifa? anaezaje kujfanya mwanaume mbele ya shujaa m,aguful wakat akna lowadsa na rostam wamemshnda?mbon ccm yenyewe ss inaelekea kaburn na hana ubavu wa kuikoa? kikwete jpme sana il usijiaibshe hasa kunapowakabl mashujaakama maguful
ReplyDeleten bahat mbaya kuwa watanzania weng hasa vjjn hatujaaamka tusingeruhusu kutawaliwa na rais kioja kama huyu na tungefanya kwel kama tunisia, misri na libya tena bla kuamshwa na chama makn kama chadema. wanaisingzia chadema kuwa inaleta machafuko lakn watanzania watakapoamka hawataisubr chadema iwaambie waandamane. na huo ndio mwsho wa ccm na mifxsad yake. chadema zungeken nch nzma mkielimsha watu na siku mja juhud zenu ztazaa matunda
ReplyDeletekikwete mpole kwa pumba na udhaifu wako.siamn kuwa rais anaeza kuwa taahra kias hcho
ReplyDeleterais huyu n laana na balaa kwa taifa.uuuuuuuuuuuuuuuui
ReplyDeleterais huyu n janga kwa taifa. n bomu, n hewa,n kioja , n kituko, n kichekesho,n taahra, n pmb, n laana, n pmb,n zuzu,n baa,na zaid ya yote n maangamz kwa taifa. uuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuui, watanzania tuende wap?
ReplyDeletekikwete nch imekushnda rud ligoba ukacheza midundko na taarab kwan hyo utaiwezea kwa sana
ReplyDeleteAma kweli nchi imejaa wajinga,hao mabwana zao ndio walizunguka huko Magufuli alipotaka kuvunja wakaanza kupandikiza chuki wananchi waichukie serikali,sasa serikali imeliona hilo inajirekebisha sasa tena haohao wanaanza kujidai kumtetea Magufuli wakati mwanzo walikwenda kwa wananchi kumpandikizia chuki. Hivi niwaulize kitu kimoja ni matajiri wangapi wataokumbwa na bomobomoa hiyo,ni wachache mno,lakini watu wa kawaida ndio wengi,sasa wanaonewa huruma mnaanza kupiga kelele na wakivunjiwa mnapiga kelele sasa kama sio utaahira ni nini? mbinu zenu zinafahamika na unafiki wenu haujifichi.
ReplyDeleteits true!kweli kikwete nchi imekushinda!rudi lugoba.
ReplyDeletemagufuli ndo mwanaume,nyie mnaomtetea rais pengine mna majumba yenu mliyojenga kwenye hifadhi ya barabara,MGUFULI OYEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE
ReplyDeleteAnayofanya magufuli ni sawa na Raisi pamoja na waziri mkuu wake walitakiwa wamuite waziri wao magufuli ofisini na kujadili matatizo yaliyotokea na kuwekana sawa wao wenyewe na baadae waongee na wananchi.Haikuwa sahihi kwa Raisi na waziri mkuu kumshambulia magufuli hadharani.Pia kwa upande wa serikali inaudhaifu mkubwa kwa sabababu serikali ilitakiwa kuwazuia raia wake kutokujenga katika maeneo yasiyoruhusiwa na kuhakikisha muda wote kunakuwa na alama za tahadhari zinazoonyesha ya kuwa ujenzi wa aina yoyote ile hauruhusiwi katika maeneo husika,Badala yake utaona serikali inawaangalia watu wakianza ujenzi mpaka wanamaliza na kuishi hata miaka ishirini na ndipo wanaanza kumfahamisha muhusika wa ujenzi huo kwamba hakutakiwa kujenga katika eneo hilo.Ingekuwa ni busara mtu kufahamishwa mapema tangu anaanza tu kuchimba msingi na mamlaka husika wanachukuwa hatuwa ya kuzui ujenzi huo.Hii ingesaidia sana kuondoa kero zote hizi.
ReplyDeleteMagufuli hakushambuliwa ni uzushi tu huo. Magufuli alitakiwa aangalie pahala barabara ilikuwepo na mahali barabara ilikuta watu. acheni propaganda za kijinga,baba zenu na mama zenu huko vijijini ndio waathirika wakubwa wa zoezi hili
ReplyDeleteacha upuuz wako ww mchangiaj hapo juu
ReplyDelete