MOSCOW, Russia
BEKI wa zamani wa timu ya taifa ya Brazil, Roberto Carlos ametaka kuchukuwa hatua kutokana na kushamiri kwa ubaguzi wa rangi nchini Russia.Mchezaji huyo
alilalamika kutokana na kupigwa na ndizi na shabiki, wakati alipokuwa uwnajani kwenye mechi.Ametoa wito huo katika siku ambayo Chama cha Soka cha nchi hiyo kilisema kuwa hakihusiki na jambo hilo.
Cerlos ambaye amesaini na klabu ya Anzhi Makhachkala, mwenzi uliopita alikutwa na dhahama hiyo katika mchezo dhidi ya Zenit St Petersburg Jumatatu.
"Tabia kama hiyo haikubaliki," alisema mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 37 na kuongeza, "Nina uhakika kuwa klabu itafanya kila kitu kinachowezekana kumpata mhusika. Hiyo ni namna ya kuweza kuondokana katika tatizo hilo."
Uwezo wa hali ya ubaguzi wa rangi katika timu za Russia inatia doa nchi hiyo, ambayo imepewa uenyeji wa fainali za Kombe la Dunia mwaka 2018.
Lakini Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) na Shirikisho Mpira wa Miguu Ulaya (UEFA), yote yametoa msimamo kutounga mkono vitendo vya ubaguzi, mashirikisho yote yamenawa mikono kuhusu jambo hilo.
Viv Anderson ambaye ni mchezaji mweusi kutoka England awali alitoa kilio kwa taasisi hizo.
Alisema: "Matukio kama haya yamekuwa yakitokea Russia kwa miaka minne, au mitano iliyopita lakini hakuna kilichofanyika.
Anderson alisema suala hilo linatakiwa kukemewa kwa kuwa nchi hiyo itaandaa fainali za Kombe la Dunia, watu wanaweza kuhofia kwenda.
No comments:
Post a Comment