01 April 2011

Walimu Lindi wandamana kudai fedha za kujikimu

Na Said  Hauni, Lindi

WALIMU 70 kati ya 100 waliopangwa kufundisha katika Shule za Msingi, Halmashauri ya Lindi vijijini mkoani hapa, wameandamana hadi Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa
halmashauri hiyo, Bw. Hijob Shemkalwah, kushinikiza kulipwa fedha zao za kujikimu.

Maandamano hayo nusura yakwamishe safari ya mkurugenzi huyo ambaye alikuwa anakwenda   Dar es salaam, pamoja na kuuwaga mwili wa Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Lindi, Ahamed Shenzigwah aliyefariki katika ajali ya gari, Machi 27 mwaka huu, Kata ya Nyengedi.

Maandamano yalifanyika katika ofisi ya halmashauri hiyo, Machi 28 mwaka huu, saa 3:30 asubuhi.

Majira aliwashuhudia walimu hao, wakimzuia mara mbili mkurugenzi huyo kupanda gari yake kwa ajili ya kustisha safari yake.

Hata hivyo mkurugenzi huyo alipata nafasi ya kuondoka katika kibano hicho, baada ya mkurugenzi huyo kuwataka walimu hao kumuona Kaimu Ofisa Elimu, Bw. Sagara Mgimba.

Wakizungumza katika kikao hicho cha pamoja na Kaimu Ofisa Elimu huyo, walimtaka kuwalipa fedha hizo ili kuondokana na matatizo yanayowakabili yakiwemo ya mazingira magumu ya maisha.

“Ndugu Ofisa Elimu nyinyi ni viongozi wetu tunaowategemeeni kututatulia matatizo yetu, mnadiriki kutusaliti na kupuuza matatizo yetu, hivi tuwaelewe vipi wenziwetu mbona walimu wa maeneo mengine wamelipwa fedha zao sisi ugumu upo wapi?” alihoji mmoja wa walimu hao.

Alisema tangu waripoti Septemba mwaka Jana katika halmashauri hiyo na katika vituo vyao vya kazi ,hawajalipwa fedha hizo, bali wamekuwa wakisumbuliwa kwenda katika ofisi hiyo na kupewa ahadi  zisizozaa matunda.

Aidha walisema kwamba kutokana na kuchelewa kulipwa kwa fedha zao hizo, kunawafanya waishi katika mazingira magumu, kwa kuzingatia walio wengi wamekuwa wakihifadhiwa katika nyumba za walimu wenzao waliowatangulia kwa kipindi chote cha miezi mitano sasa.

Alisema ugumu huo unatokana na wao kukosa fedha za kununulia vifaa vya kuanzia maisha, vikiwemo vitanda, magodoro ya kulalia, meza na vyombo vya kupikia.

Akijibu hoja hizo Bw. Mgimba, aliwaomba  walimu hao kuendelea kufanya subra, wakati viongozi wao, wakiendelea na jitihada za kuwasiliana na uongozi wa wizara katika kulipatia ufumbuzi wa tatizo  hilo.

“Walimu wenzangu uongozi wa halmashauri yenu, wala haina nia mbaya na nyinyi ya kukalia malipo yenu, tatizo ni wizara haijaleta fedha, kwani hata zile sh, 100,000/- tulizokupeni awali tulizikopa kutoka maeneo mengine,” alisema Bw. Mgimba .

Naye, Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Bw. Selemani Ngaweje, aliwataka walimu hao

Kwa mujibu wa utaratibu uliowekwa na Wizara ya Elimu Mfunzo ya Ufundi walimu wapya wanaoanza kazi wanatakiwa kulipwa fedha za kujikumu siku 14 mara baada ya mtumishi kuwasili katika kituo chake cha kazi, ili ziweze kumsaidia kuanzia maisha.

No comments:

Post a Comment