Na Mwandishi Wetu
WASHINDI wa Tuzo za Injili 2011, walipatikana wiki iliyopita katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam ambapo wasanii 18 walifanikiwa
kutwaa tuzo hilo.
Awali Kampuni ya Tanzania Gospel Music Award Promoters ilitangaza vipengele 18, ambavyo vilikuwa vikishindaniwa na wasanii 67 kutoka sehemu mbalimbali nchini.
Katika mashindano hayo ya kuwania tuzo hizo, yaliyodhaminiwa na Mradi wa 'Zinduka Malaria haikubaliki' na Clouds FM, waimbaji mbalimbali walionesha vipaji vyao kwenye ukumbi huo.
Washindi wa tuzo hizo ni kama ifuatavyo:
1.Msanii bora wa kiume kwa ujumla wa mwaka Boniface Mwaitege
2.Msanii bora wa kike kwa ujumla wa mwaka Christina Shusho
3.Kundi bora la mwaka Double E
4.Kwaya bora inayotumia vyombo vyote
Revival Choir (Kinondoni)
5.Kwaya bora inayotumia piano tu
Magomeni SDA
6.Kwaya bora isiyotumia chombo chochote
Kwaya kuu KKKT (Azania Front)
7. Bendi bora ya injili New Life Band
8.Single bora ya msanii wa kike Upendo Kilahiro
9.Single bora ya msanii wa kiume Charles Thobias
10.Msanii bora mpya wa kiume Thomas Bernard
11.Msanii bora mpya wa kike Martha Mwaipaja
12.Wimbo bora wa mwaka The Whispers Band`
13.Wimbo bora toka nje ya Tanzania Solomon Mukubwa
14. Video bora ya mwaka John Lisu
15.Mtunzi bora Upendo Nkone
16.Mtayarishaji bora wa muziki wa injili Ephraim Kameta
17.Mtengenezaji bora wa video za injili MBC Hot Media
18.Balozi bora wa jamii Miriam Shilwa.
No comments:
Post a Comment