18 March 2011

Mourinho kumrithi Ancelotti, Chelsea

MADRID,Hispania

KOCHA wa timu ya Real Madrid, Jose Mourinho ameripotiwa kwamba anataka kuchukua mikoba ya Carlo Ancelotti katika klabu ya Chelsea majira
haya ya joto.

Gazeti la London Evening Standard, liripoti jana kwamba hatua hiyo ni kutokana na kuwa hadi sasa kibarua cha Ancelotti, bado ni kitendawili na wengi wanadai kibarua hicho kinaweza kunusurika kama atatwaa ubingwa wa Klabu Bingwa Ulaya.

Kwa muibu wa gazeti hilo, tayari kocha huyo ameshaelezewa kama maiti inayotembea ndani ya klabu hiyo na inaelezwa kwamba, Mourinho ndiye atakayekabidhiwa mikoba hiyo.

Gazeti hilo linaeleza kuwa kurejea kwa Mourinho katika klabu hiyo ya Chelsea, kunapewa nafasi kubwa kutokana na uwezo wake wa muda mrefu katika udhibiti wa timu.

Mbali na udhibiti, kuondoka kwa Mkurugenzi wa Michezo katika klabu hiyo Frank Arnesen, kwenda katika Klabu ya Hamburg kunafungua njia kirahisi kurejea kwa 'Special One' katika klabu hiyo.

Jambo jingine muhimu linaloelezwa kuwepo kwa uwezekano huo ni kutokana na kwamba Mourinho, bado ni maarufu katika timu hiyo na anaendelea kuwa na mapenzi na baadhi ya wachezaji muhimu katika timu hiyo.

No comments:

Post a Comment