Na Tumaini Makene
BAADHI ya wabunge wametoa maoni tofauti juu ya uamuzi wa asasi sita zisizokuwa za kiserikali zinazoshughulika na masuala ya haki za binadamu na
utawala bora kwenda mahakamani kupinga Sheria ya Mfuko wa Jimbo wakisema uamuzi huo si sahihi kwa kuwa sheria hiyo haina tatizo.
Akizungumza na Majira jana Dar es Salaam juzi, Mbunge wa Kigoma Mjini, Bw. Peter Serukamba alisema kuwa haoni tatizo katika sheria hiyo kwa kuwa imemsaidia kutumia fedha hizo kutengeneza madawati na kupunguza adha ya kero hiyo kwa wanafunzi jimboni kwake.
"Hivi inasaidia nini kuangalia 'postmoterm', unaletewa taarifa tayari fedha zimeshaliwa, kisha mnasema fulani apewe adhabu, kazi haijafanyika na fedha hazirudi. Mimi binafsi jimboni kwangu tumezipata zile za awali milioni 40/- hivi nikawaambia wenzangu hizi tunazipeleka kwenye madawati zote, sasa tunasubiri awamu ijayo.
Kwa upande wake Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Bw. Kabwe Zitto alisema kuwa anawaunga mkono wanaharakati hao kwenda mahakamani 'lakini hawana hoja'.
"Wao walipaswa kuwa-engage (kuwashirikisha) kwanza wabunge, wawaoneshe jinsi sheria hiyo ilivyo mbovu, sasa wanakimbilia mahakamani, mimi nawaunga mkono lakini they don't have an argument, hawana hoja. Mimi nimekuwa nikipinga sheria hiyo ya mfuko wa jimbo tangu mwanzo.
Hata hivyo, mbunge huyo alisema hata yeye amekuwa akiipinga. "Tangu mwanzo nilikuwa miongoni mwa watu waliopinga mbunge kuhususishwa katika masuala ya namna hii, badala yake fedha hizo zingeweza kutumika kuimarisha ofisi za wabunge," alisema Bw. Zitto.
Tatizo ni ufisadi sio mfuko na wabunge na washiriki wa mfuko huo watazitafuna,hatuna administration nzuri ya kudhibiti hizi pesa zitaishia mikononi mwa walafi,kwa nini iwe kwa mbunge?
ReplyDelete