18 March 2011

Familia yateketea kwa moto Mkuranga

Na Mwandishi Wetu

WATU wanne wa familia moja wameteketea kwa moto na kubaki majivu katika tukio lililotokea juzi usiku katika Kijiji cha Mudimuni Kitongoji cha Bundani
wilayani Mkuranga mkoani Pwani.

Kwa mujibu wa taarifa za uhakika kutoka ndani ya Jeshi la Polisi, waliokufa ni bibi wa miaka 70 na wajukuu wake watatu.

Waliokufa wametajwa kuwa ni Bi. Ramla Abdallah (70) na wajukuu zake watatu, Paulata Kulwa Mtambo (12) mwanafunzi wa darasa la tano katika Shule ya Msingi Mdimuni, mapacha Radhia Salum Mkokwa na Rahama Salum Mkokwa.

Watu hao walikuwa wakiishi katika nyumba ya tembe. Taarifa za awali zilieleza kuwa moto huo unaweza kuwa umeanzia jikoni.

Habari kutoka polisi zilieleza kuwa marehemu hakuwa na ugomvi na mtu yeyote. Juhudi za kumpata Mkuu wa Polisi Mkoa wa Pwani ili kueleza kwa udani tukio hilo hazikufanikiwa kwa kuwa yupo nje ya kituo chake cha kazi.

No comments:

Post a Comment