22 March 2011

Ushindi dhidi ya Man City wampa jeuri Ancelotti

LONDON, England

KOCHA wa Chelsea, Carlo Ancelotti ametangaza kuwa baada ya kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Manchester City, mbio za kuwania ubingwa wa
Ligi Kuu zimeanza tena.

Kwa ushindi huo iliyoupata usiku wa kuamkia jana kwenye Uwanja wa Stamford Bridge, mabingwa hao watetezi wamechupa hadi nafasi ya tatu na wakiwa wamebakisha pointi tisa nyuma ya vinara wa ligi hiyo, Manchester United huku wakiwa na mechi moja kibindoni.

"Tuna mechi tisa za kucheza na tunapaswa kuonesha uwezo wetu," alisema Ancelotti.

"Tunapaswa kujaribu kushinda kila mechi. Manchester United walishinda Jumamosi hivyo pengo bado ni lilelile," aliongeza.

Alisema kutokana na kuwa kwa sasa kuna mapumziko ya mechi za kimataifa na wakati wachezaji watakaporejea, angependa kuona moyo na morali kama huo.

No comments:

Post a Comment