22 March 2011

Kocha Italia amtema De Rossi

ROMA, Italia

KOCHA wa timu ya taifa ya Italia, Cesare Prandelli amemteka katika kikosi chake kiungo wa timu ya AS Roma, Daniele de Rossi alichokitangaza kwa ajili ya
mechi mbili za kimataifa.

Katika mechi hizo, Italia inakabiliwa na mechi mbili ambapo itasafiri hadi Ljubljana kwa ajili ya mechi ya kufuzu fainali za Matifa ya Ulaya, Euro 2012 ambayo imepangwa kufanyika Machi 25, mwaka huu na kisha kwenda mjini Kiev kwa mechi ya kirafiki dhidi ya Ukraine ambayo itafanyika Machi 29 mwaka huu.

Kikosi hicho ambacho kilitarajia kukutana jana asubuhi kwenye uwanja wa mazoezi wa Coverciano kinaundwa na walinda mlango, Buffon (Juventus), Sirigu (Palermo) na  Viviano ambaye anadakia Bologna.

Mabeki ni Astori (Cagliari), Balzaretti (Palermo), Bonucci (Juventus), Chiellini (Juventus), Criscito (Genoa) na Gastaldello (Sampdoria).

Viungo ni Maggio (Napoli), Ranocchia (Inter), Santon (Cesena), Aquilani (Juventus), Marchisio (Juventus), Mauri (Lazio), Montolivo (Fiorentina), Thiago Motta (Inter), Nocerino (Palermo) na Parolo (Cesena).

Washambuliaji ni Cassano (Milan), Gilardino (Fiorentina), Giovinco (Parma), Matri (Juventus), Pazzini (Inter) na Rossi (Villarreal).

No comments:

Post a Comment