Na Zahoro Mlanzi
SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu la Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo 'DRC' (FECOFA), ;imezitaka Klabu za TP Mazembe, FC Lupopo, DCMP na
Club kulipa dola 20,000, badala ya 10,000 kwa ajili ya maandamano ya madini ya upepo, kabla ya robo fainali na nusu fainali ya michuano ya Klabu Bingwa Afrika, hazijaanza.
Kwa mujibu wa taarifa ya mtandano wa klabu hiyo,iliyotolewa juzi, ilisema endapo klabu hizo hazitalipa kwa wakati, zitalazimika kulipa mara mbili ya kiwango hicho.
TP Mazembe licha ya kupongezwa na Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), katika mashindano ya Super Cup yaliyofanyika Januari, mwaka huu, lakini haitaweza kulipa fedha hizo kwa kuwa wanakabiliwa na gharama kubwa katika kuandaa timu kwa ajili ya mashindano mbalimbali, usafiri, chakula, malazi,uchapaji wa tiketi na gharama za ulinzi.
Klabu ilisema pamoja na fedha wanazopata katika michezo yao, mapato wanayoingiza hayalipi na kwamba, hata timu zinapocheza kwao Lubumbashi, huwahudumia vizuri, hususani katika Ligi ya Mabingwa na ndio maana mpaka sasa hakuna malalamiko.
"Kama uchapishaji wa tiketi, kwa pakiti ni zaidi ya dola 10,000 (zaidi milioni 10) ambazo hutumika katika michezo yetu na zinatengenezwa kwa ubora wa juu kwa kukwepa hasara ambazo zinaweza kutokea kwa watu kutengeneza zaidi," ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.
Katika michezo, uamuzi kama huo hurudisha timu zilipotoka kwani kuna wakati hata waamuzi huchelewa katika mechi na maofisa wa CAF ambapo kitendo hicho husababisha timu kuadhibiwa.
Shirikisho hilo likiondokana na mambo kama hayo, ushindani uliokuwepo awali nchini humo, utarudi tena na kuzidisha mafanikio katika michuano ya Afrika.
No comments:
Post a Comment