25 March 2011

Sumaye kuwatolea uvivu vijana CCM

*Kupasua jipu mbele waandishi wa habari leo

Na Mwandishi Wetu

WAKATI joto na mvutano wa hali tete ya malumbano likipanda ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Waziri Mkuu Mstaafu, Bw. Fredereck Sumaye leo
atavunja ukimya kwa kuzungumza na waandishi habari jijini Dar es Salaam kuhusu shutuma mbalimbali zinazoelekezwa kwake kufuatia msimamo wake wa kukisoa chama hicho na mustakabali wake ndani ya chama hicho.

Katika siku za karibuni, Bw. Sumaye na baadhi ya makada wenzake wakongwe ndani ya CCM wamejikuta kwenye malumbano makali na Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) kwa kile kinachoelezwa ushauri wanaoutoa kutozingatia taratibu za chama.

Katika ngazi mbalimbali na kwa nyakati tofauti, UVCCM imekuwa ikishambulia kauli za viongozi hao kwa madai kwamba zimekiuka taratibu za chama kwani hazina lengo la kukijenga bali kukibomoa.

Mapema mwaka huu, Bw. Sumaye alikaririwa akiitaka CCM kujibu hoja zinazotolewa na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) badala ya kuacha jukumu hilo mikononi mwa mwenyekiti wa chama hicho, Rais Jakaya Kikwete.

Kauli ya Bw. Sumaye ilipokelewa kwa mitazamo tofauti ndani ya chama hicho huku ikishambuliwa vikali na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Propaganda wa CCM Bw. Tambwe Hiza aliyemtaka kufuata taratibu za chama badala ya kuzungumzia barabani.

Hiza aliungwa mkono pia na Katibu wa UVCCM, Bw. Martin Shigela aliyemtaka Bw. Sumaye na wastaafu wenzake kutumia vikao vya chama kutoa maoni yao au kuwasilina moja kwa moja na Mwenyekiti wa chama hicho kwani wana uwezo huo.

UVCCM Mkoa wa Pwani nayo ilihoji matamshi hayo ya Bw. Sumaye na Bw. Edward Lowassa kukikosoa chama hicho bila kufuata taratibu kwa maelezo kwamba hatua hiyo inachochea machafuko nchini.

Mwenyekiti wa UVCCM mkoani humo, Bw. Abdallah Ulega alisema matamko yaliyotolewa na wastaafu hao hayaelekei kushauri bali yalijikita katika ajenda binafsi zilizofichika.

"Kila mmoja alimsikia Waziri Mkuu mstaafu, Bw. Sumaye akiitaka CCM kujibu hoja za CHADEMA na si kuiachia serikali sasa unaweza kujiuliza CCM ni nani, kwanini asitumie vikao vya chama kushauri. Pia tumemsikia Mzee wetu Lowassa naye akisema eti serikali ipandishe mishahara ya wafanyakazi yeye mwenyewe alikuwa ndani ya serikali miaka miwili tu iliyopita, kwanini hakushauri hilo huko nyuma?" alikaririwa akisema Bw. Ulega.

Katika mkutano wa Baraza Kuu la Vijana lilifanyika hivi karibuni mjini Dodoma, lilipendekeza kwa chama hicho kuendelea kuwaelekeza viongozi umuhimu wa kuzingatia maadili na nidhamu kwa kutumia vikao halali kuwasilisha hoja zao.

Kaimu Mwenyekiti wa umoja huo, Bw. Benno Malisa alisisitiza kuwa si vyema kwa viongozi na wanachama wa CCM kutumia matamko kukidhoofisha chama na wao kujijengea umaarufu binafsi.

Hata hivyo, wachunguzi wa mambo ya kisiasa wanaeleza kuwa hatua yoyote ya kuwazuia wastaafu kukikosoa chama hicho ni njia mojawapo ya kukivuruga zaidi kwani kauli wanazotoa zina mwelekeo wa kukisaidia na kukinusuru tofauti na dhana inayotafsiriwa.

Wachunguzi hao walikwenda mbali zaidi na kuoanisha hatua ya kuandamwa kwa matamshi ya Bw. Sumaye na kipindi cha kuelekea mwaka 2005 ambapo mahasimu wake kisiasa walielekeza makombora mazito ya kumbomoa ili kukidhi malengo yao kisiasa.

Mkutano wa leo wa Sumaye na wanahabari unatarajia kutoa mustakabali mpya na msimamo Waziri Mkuu huyo mstaafu wa awamu ya tatu katika siasa za malumbano ya ndani zilizogubika chama hicho hivi karibuni.

Bw. Sumaye aliwahi kukaririwa na gazeti hili akisema hoja anazotoa dhidi ya chama chake ni utaratibu za kawaida ambao hauhitaji vikao.

"Nilichosema mimi hii kazi wanayofanya CHADEMA wanahamasisha umma hivyo viongozi wetu nao katika ngazi mbalimbali wafanye vikao kuelimisha umma. Hili kweli linahitaji mpaka nilisemee kwenye vikao?" alikaririwa akihoji, Bw. Sumaye.

14 comments:

  1. Hana mpya huyo,ni uraisi wa 2015 unamsumbua,ole wao CCM wapitishe jina lake watakuwa wamekitoa rehani chama kwa upinzani.Ni afadhali ata Membe japo naye hana mvuto wa kiuongozi kwa ngazi kama ile.

    ReplyDelete
  2. Nadhani kauli za kuwataka viongozi na wana CCM kutumia vikao vya chama hicho kuwasilisha mawazo yao ni kutaka kuwaziba midomo. hata hivyo kama mawazo hayo hawakuyapitisha kwenye vikao na ni yamsingi kwanini CCM na wana CCM kwa ujumla wasiyafanyie kazi? ni Hami juma

    ReplyDelete
  3. SEMA SUMAYE ILI CCM KIFE

    ReplyDelete
  4. huu ndio mwanzo wa kufa kwa ccm

    ReplyDelete
  5. Kwenda kwa Mkurugenzi Manispaa ya Ilala.
    Ufisadi huu hadi lini Ofsi ya Maji Ilala.
    Inashangaza kuwa watu wachache ndio wanaokula pesa kizembe tu ofsi ya maji ikiongozwa na Fisadi namba moja Selestina Magesa, na group lake Opitaty Kwembe mtu alie na darasa la kwanza ila wizi anaujua kupta mtu yeyote, pamoja na Wilfred Kavishe, Alex Odena, na Kahema amekuja ofsi ya maji kuja kuiba vzr pesa za miradi ya maji maana kahema na Optaty kwembe ni mahawara waliobobea! Mkurugenzi tunapenda kukutaarifu kuwa pesa ya wiki ya maji haijafaya kazi yoyote kwani baadhi ya madiwani walichoshwa na upuuzi wa viongozi hawa wa ofis ya maji na kususia uzinduzi wa wiki ya maji visima havina ubora na pia miradi mingi ni hewa tunakuomba utoe samaki wabovu ofisi ya maji ili ili kuwasaidia warengwa wa miradi husika. Tunashangaa kuona kuwa huyu kahema kaja kinyemera ofisi ya maji kisa ni mpenzi wa Optaty kwembe tunashangaa pia kuona kisima cha depot kuchimbwa kwa miliion 9 badala ya million 5, na kisima hakina ubora wa utoaji maji ya kutosha pia watumishi hapo depot bwanakosa maji vyooni na hakuna anaelishughulikia swala hili.
    TUTAENDELEA KUKUPA TAARIFA ZAIDI KUHUSU UOZO WAO NA TUNAOMBA UWAKALISHE NA KUWATIMUA IKIBIDI KWANI HAWANA NIA NZURI NA MATAKWA YA SERIKALI ZAIDI YA KUJINUFAISHA WAO TU.

    ReplyDelete
  6. UVCCM ni mtandao wa mafisadi tu wala mtu asiwadanganye ila jambo la kushukuru ni hoja iliyotolewa na Mh Kimaro kwamba kwa sasa UVCCM haina mvuto wowote ule tena. Hakuna kijana wa kitanzania anayeweza kuwasilikiliza kwa sasa. Tunalifahamu vizuri kundi linalowaaongoza na kuwaelekeza cha kusema. Ili mafisadi waendelee kuongoza hata baada ya fisadi mwenzao Kikwete kuondoka 2015. Sasa ni lazima waelewe hawana chao. Sisi sote ni vijana tunaweza kupambana nao. Tena wao siku hizi hawana hoja kwani ufisadi umemaliza hoja zao. Chadema inachukuchukua nchi 2015. Hata Rostam na kundi lake wafanyeje safari hii hawawezi. Watajalibu sana kuleta udini na ukabila ili labda iwasaidie lakini safari hii hatudanganyiki kamwe. Wakichakachua kura tutaenda mitaani. Tunahabari wanataka kuleta swala la rais atoke Zanzibar huo ndo utakuwa mwisho wao. Mpango wa kumchafua Sumaye unasukwa na nani na ni kwa nini tunajua kila kitu. UVCCM hawawezi kumfananisha Sitta na fisadi wao Rostam hata kidogo. Lakini tunajua wanapewa fedha na kundi la Rostam liwavuruge watu kama Sitta. CCM ole wao kifo chao kipo njiani

    ReplyDelete
  7. Haya tena wakati umefika wa kujua pumba zipi na mchele upi. Maskiinii CCM mgawanyiko ndani ya chama chetu uko pale pale na inavyoelekea utazidi kwani hizi jumuiya za chama kila moja ina kivuli nyuma yake. Mafisadi papa walioko kwenye chama ndio wanaokigawa chama chetu kwa kutumia nguvu walio nayo ki-fedha. Ninawaomba wana-CCM wenye nia njema na chama wakati umefika wa kuwapiga chini wafanya biashara walioko CCM kwa manufaa ya biashara zao. Akina ROSTAM ndio wanaoua chama chetu. Umaskini wetu usitumiwe kama uchochoro wa wao kupitia ili waendelee na safari yao ya kufilisi nchi yetu. Tuweni macho sana na hao. Hata hivyo Mh. Sumaye hajasema chochote kibaya kwani alitoa wazo zuri tu kwamba CCM wajibu hoja za CHADEMA badala ya malumbano. Hoja zote CHADEMA Walizotoa kwenye maandamano yao yazijajibiwa. Ni kwa nini au wanaogopwa. Ila hata hivyo tunashukuru maandamano yao kwani uwajibikaji wa viongozi wa juu umeanza kuonekana. Maana nao walibweteka wakajisahau kabisa hata vitu kama sukari vimeshuka bei. Hayo ni matunda ya kelele za CHADEMA.

    ReplyDelete
  8. HUYO NI MWIZI ANAYETAFUTA PA KUJIFICHA,NI MUHIMU LEO AKAWEKA WAZI NI JINSI GANI ALIVYOKUWA MKUU WA SHUGHULI ZA SERIKALI WALIUZA MGODI WA KIWIRA KWA BEI YA KUTUPA KWA RAIS WAKE NA YONA,ATUELEZE NDEGE YA RAIS GHARAMA ZAKE,BANDARI KUSAINIWA MKATABA WA MIAKA KUMI NA TANO MBELE KABLA ULE ULIEKUWEPO HAUJAISHA WAKATI MKATABA WA ZAMANI ULIWEKA WAZI NI MPAKA MKATABA UKIISHA NDIO UNAWEZA KURENEW,ATUELEZE MKATABA WA RITES (RELI),MADINI NA MENGINEYO MENGI, HUYU MWIZI ANATAFUTA PA KUJIFICHA,WAMEFILISI NCHI ATI LEO ANAKUJA KUSEMA KITU,WATANZANIA MSIWE WAJINGA,WANASIASA WANAWAPINDUAPINDUA WATAKAVYO KWA UJINGA WETU WA KUWAENDEKEZA

    ReplyDelete
  9. KAMA MNAJUA NI MWIZI KWA NINI HAMMKAMATI? ACHENI KUTUDANGANYA! NYIE NDIO WEZI, MNAJIFICHA KWA KUWAPAKA MATOPE WENGINE

    ReplyDelete
  10. SUMAYE-UVCCM SI BUA TU BALI WAMEJAA USWAHILI PIA!!!!!

    Sumaye, katika mazungumzo yake alionekana kama mtu anayenusa hatari inayotaka kuikumba CCM na taifa kutokana na kauli zinazotolewa na Katibu Mkuu wa CCM, Yusufu Makamba na viongozi wa UVCCM
    Sumaye alisema kauli nyingine iliyotolewa na UVCCM Pwani ambayo ni ya hatari ni ile waliyoeleza kwamba Sumaye na Lowassa wasahau urais wa 2015, kwa vile hawataupata na kwamba tayari Rais Kikwete ana jina la mtu atakayekuwa rais.
    “Kwa kauli hii naweza kusema " amani, utulivu na usalama wa nchi upo hatarini. Hii inaonesha kuwa UVCCM tayari wanamjua mtu ambaye ameandaliwa kuwa Rais mwaka 2015 na hivyo wanachokifanya ni kutaka kumsafishia njia kwa kuwashambulia wanaCCM wengine.
    “Wanataka kutueleza kuwa tayari Rais Kikwete ana hilo jina na wanachokifanya wao ni kumpigania awe rais, hata kama hana uwezo wa kutuongoza, jambo ambalo ni la hatari sana.
    Alizungumzia pia kauli kwamba Rais hawezi kutoka Kanda ya Kaskazini kuwa ni kauli ya kibaguzi na inayopaswa kulaaniwa na CCM; “Huu ni ubaguzi wa hatari maana unaweza kukigawa chama. Hakuna kiongozi atakayeiongoza nchi hii kwa misingi hiyo ya ubaguzi wa dini, rangi, utaifa.

    ReplyDelete
  11. AKAMATWE NA NANI NA WENYEWE WANALINDANA,SUBIRINI IKO SIKU ITAFIKA,HICHO NI KIHEREHERE TU CHA WOGA,KAMA WEWE UNAMTETEA UNGEJIBU HAYO NILIYOTAJA HAPO JUU YA EPA,BANDARI,RELI,MIGODI,MASHIRIKA YA UMMA KUUZWA KWA BEI YA KUTUPWA,KIWIRA,NDEGE YA RAIS,RADA. HUYO NI MWIZI MKUBWA WALIOANGAMIZA NCHII ANATAFUTA PA KUJIHIFADHI,DHAMBI YA WIZI INAMTAFUNA

    ReplyDelete
  12. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  13. TATIZO LA UVCCM NI UDUNI WA ELIMU DUNIA, HATA UKIONA MANENO WANAYOSEMA NIKAMA VILE MTU HAJAENDA SHULE!NAKAMA WALIMALIZA SHULE BASI WALIMALIZA KWA KUDRA YA MWENYEZI MUNGU MWENYE REHEMA ZOTE.
    KINACHO NISHANGAZA ZAIDI NI KWA NINI MWENYEKITI WA CCM AMEKAA KIMYA NA KURUHUSU HAYA MAJIBIZANO YAKIENDELEA? BILA SHAKA SASA TUNAWEZA KUONA UDHAIFU WA HUYU MWENYEKETI WA TAIFA WA CCM.

    ReplyDelete
  14. BARUA YA WAZI KWA WANA-CCM.
    Hivi haya maneno na malumbambano ya kila siku hamuoni kuwa badala ya kujenga chama chenu mnakibomoa chama hiki kikongwe? Hivi mwenyekiti wa chama hiki mheshimiwa J.kikwete yuko wapi? hivi kweli anafurahia hali hii ya malumbano yasiyo na tija? hivi mzee makamba kwa hekima ya uzee wake anaona busara kupayuka kila siku kwa mambo yale yale? Sumaye akisema kitu wanamjibu, lakini chadema wakirusha dongo la CCM wanakaa kimya kiasi kwamba wananchi wanafikiri ni kweli yale chadema wanayosema ni kweli! mbona kama katibu wa chama hujibu mapigo ya chadema? mie naona mzee makamba husitahili cheo hicho!ni muda wako mzuri wa kujiuzuru nafasi hii, hapo ulipofikisha chama inatosha!!! unajenge uswahili sana katika chama na sasa umemuambukiza mwenyeketi wa CCM mh. J kikwete uswahili huo.
    Ebu tukumbushane kama siyo mageuzi haya batiri ndani ya CCM ya sasa,enzi ya uwenyekiti wa baba wa taifa hali hii ya kutukanana kada wa CCM kwa kada wa CCM ingeweza kutokea? kwa mtazamo wangu chama cha CCM kimekosa mvuto tena na jinsi kinavyoendeshwa ni ibilisi tu ndiye anayejuwa chama kinatumia dira gani! NINI KINAFANYA KIKWETE KUKAA KIMYA??? bila shaka anahusika na kile kinachoendelea sasa hivi ndani ya chama chake, vinginevyo kikwete ameshindwa kuongoza chama ni bora aachie ngazi kama mwalimu nyerere alivyoachia ili chama hiki kirudiwe na hadhi na heshima kama ilivyokuwa mwanzo.

    ReplyDelete