11 March 2011

Singida kuzalisha umeme megawati 1,000

Na Mwandishi Wetu

MKOA wa Singida umeelezwa kuwa na uwezo wa kutengeza umeme wa upepo wa megawati 1,000 ikiwa itawekeza kwenye mradi huo kwa kushirikiana na
kampuni ya kutoka China.

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Bw. Lazaro Nyalandu alisema hayo jana baada ya kurejea nchini kutoka China, alikokwenda kwenye ziara ya siku 10 akiongoza ujumbe wa serikali uliokwenda kujiridhisha kuhusu uwezo wa kiutendaji na kiteknolojia wa kampuni ya kutengeneza umeme wa upepo ya CDIG.

Kampuni ya CDIG ina uwezo mkubwa katika utekelezaji wa mradi umeme wa upepo katika Mkoa wa Singida, teknolojia ya Kichina ni ya kiwango cha kimataifa na tumeridhika nayo, alisema Bw. Nyalandu.

Aliongeza kuwa baada ya kujiridhisha na ubora wa mashine zinazotengenezwa na kampuni hiyo, ujumbe wa China utatembelea Tanzania kuangalia uwezekano wa kuingia mkataba na kampuni hiyo ili mradi huo kuanza.

Bw. Nyalandu alisema muda wa kuanza kwa mradi huo utategemea uharaka wa serikali katika kuingia mkataba na kampuni hiyo.

Aliongeza kuwa ujumbe huo ulitembelea kampuni ya Sinovel inayotengeneza mapanga ya kuzalisha upepo na kujionea uwezo mkubwa walionao.

Tumekuta kuna panga moja linalozalisha umeme ambalo lina urefu wa mita 42 na mtambo mmoja wenye uzito wa tani 262. Tumeridhika kwamba wenzetu wako mbali na wana uwezo katika teknolojia ya umeme wa upepo, alisema Bw. Nyalandu.

Alisema mkoa huo umetenga hekta 50,000 kwa ajili ya shamba la kutengeneza umeme wa upepo. Alisema eneo jingine nchini ambalo linaweza kuzalisha umeme wa upepo ni Makambako mkoani Iringa.

Akiwa nchini humo, Bw. Nyalandu alisaini makubaliano ya awali na mashirika mawili yatakayowezesha uanzishwaji wa kituo cha utafiti na maendeleo kwa ajili ya kufanya utafiti kuhusu umeme unaotokana na jua na upepo.

Alisema kituo hicho kitakachokuwa katika moja ya vyuo vikuu nchini, kitasaidia kutoa wataalamu waliobobea katika fani ya umeme wa jua na upepo.

Katika makubaliano hayo, Tanzania itakuwa ikituma wanafunzi na wataalam nchini China kujifunza zaidi kuhusu umeme wa jua na upepo.

6 comments:

  1. HAYA SASA NDIO MAMBO YANAYOTAKIWA NA KULETA MOYO HAPO NI KUHARAKISHA MCHAKATO UANZE MARA MOJA ILI TUONDOKANE HII HALI YA KUZOROTESHA MAISHA YETU NA UCHUMI KWA UJUMLA.UKIRITIMBA KWA MAMBO KAMA HAYA HAYAFAI,WASIWASI WANGU HAPO HILO NENO LA NAIBU WAZIRI KUANZA KWA MRADI KUNATEGEMEA UHARAKA WA SERIKALI KUTILIANA SAINI YA MAKUBALIANO!! HAPO NDIO 10% IPATIKANE NDIO KIELEWEKE ITACHUKUWA HATA MIAKA 2 HAKIJAELEWEKA INATAKIWA RAISI AU WAZIRI MKUU ATOE AGIZO LA KUHARAKISHA KUANZA MRADI HUO TENA KUWAPA MUDA WA MWISHO ISIZIDI NDANI YA MIEZI 3 MKATABA UWE UMESAINIWA

    ReplyDelete
  2. NDO YALIYOMKUTA LOWASSA RICHMOND HAYO HARAKAHARAKA ZILIZO NA DILI NYUMA YAKE. SUALA HAPA NI JE ALICHOKIONA NAIBU WAZIRI NI KWELI? MAANA TUSHAONGOPEWA SANA TU MWISHO WA SIKU TUNAKUTA TUMELAMBA JOKER.

    ReplyDelete
  3. Wachina mnawajua pale wanapotaka jambo lao lipite! na pia mafisadi nao wanapotaka kupitisha ulaji. Zitatolewa sifa zote nzuri, delegesheni itafikishiwa peponi na warembo kutoka pande zote za dunia. Kinachotakiwa siyo kukimbilia. Zifanyike tathmini kulingana na taratibu za kisheria. Na siyo kwa kuwa waziri kaona panga la mita 42.
    Si mnamkumbuka huyu alifanya kampeni kwa kutumia Helkopta. Alitoa wapi hizo pesa.
    Tufikiri

    ReplyDelete
  4. Umemme unotekana na teknolojia ya upepo upo pia kuna umeme unaotokana na makaa ya mawe tuache mambo ya siasa mbali.Kuna nchi kama ujerumani hata marekani na nchi nyingine kubwa duniani wanazo hizo teknolojia.
    Nijambo la busara sana kutoka kwa Nyalandu badala ya kusubiri mvua kila mwaka na mvua zinapo kosekana matatizo yake ni kama haya tuliyo nayo.Matatizo ya umeme Tanzania yameenza katika miaka iliyopita inawezakufika haza zaidi ya mitano lakini hakuna hatua za muhimu zilizo chukuliwa kutoka kwa viongozi wausika pamoja na kuangalia nchi za wenzetu wanafanyaje.Huu ni mwanzo mzuri hongera sana mheshimiwa nyalandu.Tunataka viongozi kama hawa ambao bado ni damu mpya katika karne hii ya leo. Vijana ni taifa la leo na wazee ni taifa la jana na watoto ni taifa la kesho.

    ReplyDelete
  5. Hapa anasifiwa mhe. Nyalandu kwa kutembelea China au kwa kufanya utafiti? au kuona panga lenye mita 42 au kusema wenzetu wako mbali ndo utafiti? tunao wataalam katika vyuo vyetu vikuu kwa nini tusiwatume hao wakaenda China kwa gharama za nchi kufanya utafiti na kuishauri serikali badala ya ziara ya mhe. ambaye kwa ujumla alifikia hotelini na kutembezwa sehemu mbili tatu kisha kupewa 10% yake ili awe mpiga debe mzuri...hili tatizo ni la miaka kibao na sidhani kukurupuka kusaini mkataba ndo ufumbuzi...utafiti wa kina utainufaisha nchi!!!!

    ReplyDelete
  6. Achinjwe kama ataleta uwekezaji umeme wa bei ghali kama DOWANS/IPTL wakati rasilimali ni zetu.

    Uwekezaji wa kuwanyonya watanzania na kunufaika na 10%, taifa lipoteze mabilioni kwa ajili ya familia moja tu wakati Watanzania milion 40 wanateseka.

    Tujiulize, huo umeme utakuwa bei gani?

    ReplyDelete