03 March 2011

Simba Temeke wataka jihadi Jumamosi

Na Andrew Ignas

UONGOZI wa matawi ya Klabu ya Simba Wilaya ya Temeke umewataka wachezaji wa timu hiyo kuhakikisha wanacheza kwa jihadi katika mechi ya
Ligi Kuu dhidi ya watani wao jadi Yanga itakayopigwa Jumamosi ili washindi na kutoka kifua mbele.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Dar es Salaam juzi Katibu wa matawi hayo, Hussein Simba alisema wachezaji wao wanatakiwa kujituma katika mchezo huo kama fainali.

"Nachotaka kuwaomba wachezaji wa Simba ni kuhakikisha mchezo wetu dhidi ya watani wetu Yanga, tunautumia vizuri ili tuweze kurudi kileleni," alisema.

Alisema licha ya ushindi mzuri waliopata katika mchezo uliopita dhidi ya Mtibwa Sugar, lakini wanachotakiwa kuangalia zaidi mbio za ubingwa.

Hata hivyo Katibu huyo amewataka wachezaji kuwa na ushirikiano wa hali na mali katika mechi hiyo, badala ya kutegeana uwanjani.

3 comments:

  1. mnapiga kelele mambo kibao utafikiria kuna ti za maanaoooooooo vijitim vyenyewe feki ubabaishaji tu havina mbele wala nyuma maendeleo hakuna tim zina zaidi ya miaka 40 ubabaishaji tu nashanga mtu mzima na akili yake eti anataka hata kupigana au kujaribu hata kupoteza uhai wake sababu ni mshabiki wa simba au yanga hainiingii akilini

    ReplyDelete
  2. Mzee naona huelewi maana ya upinzani,naona ungewaachia wenye kuujua mpira waendelee,,,kachangie mada nyingine huu si uwanja wako

    ReplyDelete
  3. wewe mtoa maoni ywa saa 8:42pm, ndio wale wale mkijiita arsernal au Manchester basi mnajiona waingereza tayari, kwani wewe umefanya juhudi gani kuinua soka bongo? swala la upenzi lipo pale pale hata kama ni level ya match za mchangani hiyo ndio sports, kama wewe unazo starehe nyingine u better carry on na uwaachie wenzio starehe zao. Usilete politics kwenye sports.

    ReplyDelete