31 March 2011

Serikali ya JK imepoteza mwelekeo-Lipumba

Na Benedict Kaguo, Tandahimba

MWENYEKITI wa Taifa wa Chama Cha Wananchi CUF, Profesa Ibrahim Lipumba amesema Serikali ya Rais Jakaya imepoteza mwelekeo hadi inayosababisha migongano
baina baina ya viongozi kwa viongozi akitolea mfano suala la Waziri wa Ujenzi John Magufuli kuumbuliwa na rais mbele ya mkutano wa hadhara.

Badala yake alisema ingekuwa vema kwa rais kumuita katika Baraza la Mawaziri ili kumweleza udhaifu wake kuliko kumshambulia mbele ya umma wa Watanzania na kuifedhehesha serikali mbele ya wananchi.

Akihutubia wakazi wa Mji wa Tandahimba Mkoani Mtwara katika mwendelezo wa mikutano ya operesheni Zinduka juzi jioni, Profesa Lipumba alisema kitendo hicho kimeonesha udhaifu mkubwa wa uongozi uliooneshwa na Rais Kikwete.

“Ndugu zangu Serikali ya CCM inasambaratika, na hili suala la Waziri Magufuli kukanywa na Rais Kikwete kwenye mkutano wa hadhara ni kielelezo cha rais kushindwa kuongoza nchi, hii ni fedheha kubwa kwa serikali,” alisema Profesa Lipumba.

Alisema hali hiyo wananchi wanapaswa kuiona kuwa ni ishara ya serikali ya CCM kushindwa kuongoza nchi, ndio sababu kumekuwepo na matukio mengi ya migongano kati ya viongozi wa juu wa serikalini.

“Watu wanaoweza kukaa kwenye Baraza la Mawaziri wakazungumza lakini watu wanaumbuana hadharani, sasa Waziri Magufuli anakanywa mbele ya umma ni wazi uwezo wake katika maamuzi utakuwa umetetereka,” alisema Profesa Lipumba.

Alisema jambo la msingi badala ya viongozi hao kulumbana hadharani wangekuwa ndani ya Baraza la Maziri na kutoa mawazo mazuri juu ya utekelezaji wa suala hilo la bomoabomoa kwani huwezi kumbomolea mtu nyumba wakati hakuna bajeti ya kujenga barabara.

3 comments:

  1. Lipumba unafiki utakumaliza:
    Chadema wakisema maneno hayo hayo unasema wanachochea vurugu... yetu macho na masikio.
    Hata hivyo sipingi hoja yako ya msingi kuwa CCM inaenda mrama. Ninachoogopa ni kuwa wapinzani hamkai sawa ili kuziba ufa huo wa uongozi ili CCM wakiondolewa tuwe na timu nzuri ya kuongoza.
    Kingine cha kustaajabisha ni kutowasikia UVCCM, ambao wamejipachika ukiranja wakilisemea hilo la Kikwete kutotatulia tofauti za maamuzi ndani ya vikao husika.
    Sasa nitawakumbusha kama walikuwa hawajui/wamesahau: Tabia ya kusemea nje ya vikao halali imejikita zaidi kwa Mwenyekiti wao na si Sumaye

    ReplyDelete
  2. M N A F I K I.

    KAMWE HATUDANGANYIKI

    ReplyDelete
  3. acheni ushabiki wa kijinga kingekuwa chadema ndo kimesema ndo mngesifia kasema pro, mnafiki kwa mtazamo huu wa wananchi wa tz kizuri unachopenda wwe tu hata mwenzio afanye zuri gani linakuwa baya huo wenu ni uchawi bado kuruka tu usiku, mtajiju subirini slaa aseme musifie hata akinya mavi yake mtasema dhahabu duh usiombe kuzaliwa tz mbumbumbu watupu zero +?!!!!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete