Na Mwali Ibrahim
TIMU ya taifa ya ngumi za ridhaa inatarajia kuingia kambini Machi 15, mwaka huu kwa ajili ya kujiandaa na michuano ya Mataifa ya Afrika 'All African Games' inayotarajia
kufanyika Septemba mwaka huu Maputo, Msumbiji.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Ngumi za Ridhaa Tanzania (BFT), Makore Mashaga alisema tarehe hiyo ni kwa mujibu wa kalenda yao ya mwaka, hivyo wataifuata na kuhakikisha timu inaingia kambini kwa tarehe husika.
"Hatutegemei kubadilisha tarehe, kwani itakuwa ni kinyume na kalenda yetu, hivyo tutahakikisha tunaifuata na mabondia kuanza kambi mapema kwa ajili ya kujifua na michuano hiyo na mingine itakayojitokeza," alisema Mashanga.
Alisema kuhusiana na kuchagua wachezaji watakaounda kikosi hicho kwa ajili ya kuanza maandalizi, tayari makocha wameshawaona na watawatangaza hivi karibuni kwa ajili ya kuanza kambi hiyo.
Mashaga alisema wanatarajia kuchagua mabondia 20, na katika kila uzito watatoka baada ya uzito kugawanyika katika vipengele 10, ikiwa ni kwenye uzito tofauti.
No comments:
Post a Comment