LONDON, England
KOCHA wa Chelsea, Carlo Ancelotti ametupilia mbali nafasi ya timu yake kutetea ubingwa wa Ligi Kuu, licha ya kuilaza Blackpool 3-1.Ushindi huo
umeifanya Chelsea, ipitwe kwa pointi tisa na vinara wa ligi hiyo Manchester United, wakiwa na mchezo mmoja kibindoni watakaocheza na Manchester United katika Uwanja wa Old Trafford.
Lakini Ancelotti alisema: "Lengo letu kwa wakati huu ni kubakia katika timu nne bora.
"Tunazidi kuwasogelea Manchester United, lakini hatuna budi kujiandaa kwa mchezo ujao na kujiandaa vizuri kwa kila mechi."
Alisema kwamba kwa sasa timu yake ipo nyuma kwa pointi tisa na wana mchezo dhidi ya Birmingham, lakini ni jambo ambalo si rahisi kufikiria kama wataweza kutetea ubingwa wao.
Chelsea sasa wamekusanya pointi 51 wakishikilia nafasi ya nne.
No comments:
Post a Comment