LONDON, Uingereza
MCHEZAJI wa Santos, Neymar amelalamikia vitendo vya ubaguzi wa rangi vilivyokuwepo uwanjani wakati wa mechi ya kirafiki kati ya Brazil dhidi ya Scotland.Mechi hiyo
iliyochezwa katika Uwanja wa Arsenal wa Emirates, inadaiwa ilikuwa na vitendo vinavyoashiria ubaguzi wa rangi dhidi ya nyota wa Santos, Neymar.
Brazil iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 katika mechi hiyo, ambayo yote yaliwekwa kimiani na Neymar ambaye alikuwa katika kiwango cha juu.
Neymar mwenye miaka 19, alirushiwa ndizi uwanjani kitendo ambacho kinatajwa kuwa ni ubaguzi wa rangi.
Ndizi ni tunda linalopendelewa na nyani. Timu ya Brazil ina wachezaji mchanganyiko wazungu na weusi.
"Mazingira haya ya ubaguzi kwa ujumla yanasikitisha," Neymar aliiambia televisheni ya Brazil channel Sportv.
"Walikwua akinizomea sana na hata wakati nikienda kupiga penalti uwanja wote walikuwa wakizomea. Tuliacha kucheza katika nchi yetu kucheza hapa na kitu kama hiki kinatokea, Inasikitisha," alisema.
No comments:
Post a Comment