LONDON, England
NYOTA wa Liverpool, Steven Gerrard amesema anajisikia mwenye furaha baada ya kuchagua kubaki katika klabu hiyo ya Anfield.Kauli ya mchezaji huyo
imekuja baada ya timu za Chelsea na Real Madrid, kujaribu kumuwinda bila mafanikio na kisha mchezaji huyo kuamua kubaki katika klabu hiyo ya Liverpool.
Aliiambia tovuti ya klabu hiyo juzi kuwa: "Ilikuwa vizuri nipokuna kichwa kutafakari wakati klabu zilipoanza kunitamani, lakini kwa sasa nikiangalia nyuma najivuna kwa kufanya uamuzi sahihi."
Nyota huyo alisema kuwa kila mtu mawazo ambayo anayapata akiwa nyumbani na kisha kutwaa ubingwa, huku marafiki na wanadungu wakiungana naye kusherehekea hayawezi kupingwa.
Alisema kuwa inakuwa vizuri zaidi timu inapotwaa ubingwa ukiwa unaichezea.
No comments:
Post a Comment