04 March 2011

Mwinjilisti aliyejeruhiwa Mto wa Mbu afariki dunia

Na Glory Mhiliwa, Arusha

MWINJILISTI wa Kanisa la Pentekoste la Mto wa Mbu, Jackson John ambaye alikuwa mmoja kati ya waliojeruhiwa kwenye mapigano baina ya
waumini wa madhehebu ya kiislamu na kikristo yaliyotokea Februari 24 wilayani Monduli amefariki dunia.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na ndugu wa mwinjilisti huyo  zinadai kuwa alifariki jana alfajiri katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC.

Mapigano hayo yalitokea baada ya waumini wa kiislamu kuwashutumu Kiongozi wa Kanisa la Full Salvation Church, Mchungaji John Chenge (29) aliyekuwa akihubiri injili eneo la Comix  kwa kukashifu dini ya kiislamu.

"Ndugu yetu kafariki, unajua alipigwa sana alitobolewa na misumari kwenye kifua hata kwenye macho. Amekufa kutokana na majeraha ya misumari aliyoyapata kwenye kifua ambako baadhi ya misumari iliichelewa kutolewa; alisema mmoja wa ndugu wa marehemu ambaye
hakupenda kutaja jina lake.

Hata hivyo, Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Arusha, Akili Mpwapwa alikana kusikia taarifa hizo.

Kwanza nyinyi nani kawaambia mimi sina hizo taarifa, sijaletewa. Ndio nazisikia kutoka kwenu," alisema Kamanda Mpwapwa.

Katika mpigano hayo vitu mbalimbali viliharibiwa yakiwamo makanisa ya Angilikana na Pentekoste, shule ya Mama Anna na nyumba za wakazi wa Mto wa Mbu kwa kuchomwa moto.

Kutokana na vurugu hizo Jeshi la polisi linawashikilia watu kadhaa, akiwamo Bwanga Musa (54), Shaban Hassan (58), Gabriel Kamunya (45), Ana Sospeter (40), Rashid Mziray (29), Frank Mwenda (42) pamoja na Bakari Twalib (18).

16 comments:

  1. Mheshimiwa Wasira, hapo je? Chadema wakamatwe?

    ReplyDelete
  2. Ninachokiona haukuwa ugomvi baina ya wakristo na waislam, isipokuwa na Waislam kuwavamia wakristo maana sijasikia uharibifu wa mali za waislam wala kusikia kama walijeruhiwa.

    ReplyDelete
  3. Ngoja tuone serikali ya Kikwete itachukua hatua gani.

    ReplyDelete
  4. ukitukana dini ya mwenzako bila ushaidi wa maandishi si sawa na matokeo yake ni haya.Tujifunze kusema na kutenda

    ReplyDelete
  5. Haya ndio matokeo ya Kikwete, viongozi wetu wa kikristo mmezidi kuwa wakimya. Morogoro tena jana jamaa kakwidwa koo kisa anagalia gazeti la GLOBAL P. Jamani tunakwenda wapi. Mbona wao wanafanya mihadhara kule mwembeyanga na sehemu nyingine mbona wakristo wanavumilia.

    Kama ni kweli serikali ijibu bila ya hivyo sasa wakristo uvumilivu uishe na sisi tuingie barabarani. We wasira, mrema cheyo na wezako wanafiki wakubwa manatumaliza na hao mayahudi waliomuuwa yesu hatutakubali kamwe.

    ReplyDelete
  6. hapa dodoma kuna msikiti mmoja pale majengo yaaaniiiii ni kutukana kutukana kutukanaaa...je kikwete unataka tuseme imetosha? na hii inaitwa radio imani yaani ni kutukana kutukana kutukana....je kikwete unatupa maelekezo gani?

    ReplyDelete
  7. Wakristo na waislamu tuvumiliane jamani,tumeishi vizuri miaka mingi na hata kuoleana;tunakwenda wapi? serikali ya ccm inasemaje?

    ReplyDelete
  8. Rais Kikwete amesema mara nyingi sana kuwa kuna Udini...sasa waliofanya Waislamu Arusha kakaa kimya bila kusema lolote. Wakristu wakisema kitu kupinga serekali wanasema udini....Kikwete, Kikwete nani ni mdini kama sio wewe?

    ReplyDelete
  9. Hii ndiyo faida ya JK kukuza UDINI kwakutetea UCHAKACHUAJI WAKE. Yeye na baadhi ya WAISLAMU watakuwa wamefurahi kuuwa KAFIRI kama wanavyotuitaWAKRISTO, na wanaamini wataenda peponi moja kwa moja. Nakuanzia leo tukisikia MIHADHARANI kwao wanaisoma vibaya BIBLIA na kutukashifu, nasisi tutachukua hatua mkononi. Hili tatizo limeletwa na CCM, sasa tusikie kama WASIRA na wenzie watatudanganya nini tena.

    ReplyDelete
  10. Wakristo na chama chetu cha CHADEMA tupoo...tupambane hawa waislam hawana chao mwaka 1015!

    ReplyDelete
  11. SAFI SANA.FAIDA YA KUTUTUKANIA MTUME WETU NDIYO HIYO.WENGINE JIFUNZENI.TUMECHOKA.

    ReplyDelete
  12. wewe unayeshadadia kifo cha mtu kwa sababu kamtukana mtume; hivyo ndivyo mafundisho ya mtume yasemavyo kwamba atakayemtukana auawe? damu za watu hawa zitakulilieni!

    ReplyDelete
  13. KAMA VIONGOZI WA CCM WATAACHA WOGA NA KUKEMEA MIHADHARA POTOFU DHIDI YA DINI YA KIKRISTO INAYOENDESHWA NA WAISLAMU WASIOJUA CHOCHOTE KUHUSU UKRISTO WALA KUNNGOZWA NA ROHO MTAKATIFU ...NCHI HII ITAISHI SALAMA
    KAMA AMBAVYO WAISLAMU WANAVYOTAKA KUR'AANI ISINAJISIWE WALA MTUME MOHAMED KUNENEWA VIBAYA ..NDIVYO WAKRISTO TUNAVYOTAKA CCM WAFUATILIE MIHADHARA HATARISHI KWENYE MISIKITI INAYOENDESHA CHUKI NA UNAFIKI DHIDI YA WAKRISTO
    HAPA NDIPO VIONGOZI WA CCM WANAPOTAKIWA WAACHE UNAFIKI WA KUNYOOSHEA VIDOLE CHADEMA.
    WAACHE KUWAOGOPA WAISLAMU ...KAMA VIONGOZI WA KIKRISTO WA CCM HAWAWEZI BASI RAISI MWISLAMU NA MAKAMU MWISLAMU WAFANYE HII KAZI LA SIVYO DAMU IKIMWAGIKA WATABEBA LAWAMA NA SIYO CHADEMA ISIYO HUBIRI CHUKI ZA KIDINI WALA ISIYO NA MAMLAKA YA DOLA YA KUONDOSHA MIHADHARA HIYO MIBAYA NA HARARISHI KWA WATANZANIA TUSIOJUA CHUKI TUNAOONA BAINA YA DINI HIZI

    ReplyDelete
  14. Ni Bora chama chetu cha kikristo cha CHADEMA kingeingia ikulu, WAISLAMU waingeipata. Mahubiri yao yote ya kuukashfu ukristo yangekoma. Tusubiri mwaka 2015, WAKRISTO WOTE Tuchague CHADEMA, ili kipambane na hawa ndume wenye kukashfu dini yetu.
    BWANA AHIMIDIWE!

    ReplyDelete
  15. Siamini pia kama Mungu anapenda wapumbavu!!!!!!

    ReplyDelete
  16. Kama akili mnatumia katika kula ubwabwa, kuzaa na kuleta Vurugu, nafikiri hata mngepewa ubongo wa nzi ungewatosha kufanya hayo mnayoyafanya!

    ReplyDelete