18 March 2011

Ferguson: Kufungiwa mechi ni sawa kutema mate

 LONDON, Uingereza

ALEX Ferguson, ambaye amefungiwa mechi tano ameelezea kuwa kitendo hicho ni sawa na kutema matope.Kocha huyo wa Manchester United, Fergie pia
ametozwa faini ya pauni 30,000 na wakuu wa Chama cha Mpira wa Miguu England (FA) kutokana na kumdhalilisha refa, Martin Atkinson.

Kwa adhabu hiyo atalazimika kukaa jukwaani katika mechi nne wakati timu yake ikicheza na kukosa mechi ya nusu fainali ya kuwania Kombe la FA, dhidi ya
Manchester City, imefanya awe kocha wa kwanza kufungiwa wakati timu yake ikicheza Wembley.

Ferguson alikuwa na matumaini ya kutoadhibiwa katika mashitaka ya kufanya kitendo kisichokuwa cha kiuanamichezo, iliyosikilizwa juzi na FA.

Alisema anaamini kuwa ameadhibiwa kwa kuonekana kutomwamini refa, Atkinson kwa uchezeshaji wake katika mechi dhidi ya Chelsea iliyoishia kwa kufungwa mabao 2-1 ugenini Stamforde Bridge Machi Mosi mwaka huu.

Chanzo kutoka United kilisema yeye anaamini kuwa alitoa maoni kutokana na uchezeshaji wa refa. Hakulenga kutaka kueleza kuwa refa huyo alipendelea na kumsahihisha kuzingatia sheria baada ya mechi.

Aliungwa mkono na kocha wa Chelsea, Carlo Ancelotti.

Kocha huyo wa Kiitaliano alisema: "Ninajua kile alichosema baada ya mechi. Haikuwa vizuri lakini kufungiwa mechi tano imezidi mno."

Ferguson alimlaumu, Atkinson kwa kutompa kadi nyekundu mlinzi wa Chelsea David Luiz kwa kumchezea faulo, Javier Hernandez na Wayne Rooney wakati tayari alishakuwa na kadi ya njano.

Kocha wa United alisema: "Unatakiwa kutaka refa anajali sheria, au refa imara na hatukuwa na refa wa hivyo. Lazima niseme, wakati nilipoona ni refa gani atakayechezesha, nilishikwa na hofu."

Ferguson katika msimu uliopita alifungiwa mechi tatu kutokana na kutoa maoni ya kumponda refa
Alan Wiley.

Sasa adhabu yake itaanza Machi 22, mwaka huu kwa kukosa mechi dhidi ya West Ham (April 2), Fulham  nyumbani (Aprili 9), dhidi ya City Aprili 16 au 17, Everton nyumbani (Aprili 23) na Arsenal ugenini (Mei Mosi).

No comments:

Post a Comment