10 March 2011

Mnigeria kortini kwa kukutwa na kilo 800 za heroin

Na Rehema Mohamed

RAIA wa Nigeria, Bw. Luvinus Chime (43) amefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa tuhuma ya kusafirishwa na kukutwa na kilo 810 za
dawa za kulevya aina ya heroin.

Akisomewa mashtaka hayo na Mwendesha Mashtaka, wakili wa Serikali Bw. Biswalo Mganga mbele ya Hakimu Mustapha Siyani ilidaiwa kuwa mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo Machi 3, mwaka huu.

Ilidaiwa kuwa mtuhumiwa alikutwa na dawa hizo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere akiwa katika harakati ya kusafiri.

Hata hivyo, mtuhumiwa huyo hakutakiwa kujibu lolote kutokana na mahakama hiyo kutosikiliza kesi za aina hiyo, mpaka itakapowasilishwa Mahakama Kuu.

Mtuhumiwa huyo amerudishwa rumande hadi kesi yake itakapotajwa tena Machi 23, mwaka huu.

Wakati huo huo, Bw. William Muchange amefikishwa mahakamani hapo kwa tuhuma za kughushi hati ya kiwanja namba 38631, kwa lengo la kuiwasilisha katika Wizara ya Ardhi kama hati halali.

Akisomewa mashtaka hayo na Wakili wa Serikali Bi. Anna Malipula mbele ya hakimu Bw. Mustapha Siyani, ilidaiwa kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo Agosti 2010, Sinza Barabara ya Shekilango.

Ilidaiwa kuwa mtuhumiwa kwa makusudi akijua kuwa kufanya  hivyo ni kosa, aliiwasilisha hati hiyo kwa Ofisa wa Ardhi Bw. Mosses Mbua akidai ni halisi

Mtuhumiwa huyo alikana kosa hilo na yupo ndani kutokana na kukosa wadhamini. Kesi imeahirishwa hadi Machi 23, mwaka huu.

6 comments:

  1. Jamani waandishi muwe waangalifu. Kilo 800 ni karibu tani moja ya mzigo hawezi kusafiri nao mtuhumiwa kama luggage (ambayo nadhani maximum ni 40kg kwa Business Class au 1st Class). Ina maana itabidi uwende kwenye cargo.

    Au ulikusudia gram 800 ambayo ni chini ya kilo moja?

    Jamani musikimbie umande wakati wa kusoma somo la hesabu.

    ReplyDelete
  2. TUNAWASIFU KWA BIDII LAKINI KINACHOONEKANA NI KUWAKAMATA WASLE TU WALIOCHOMEANA LAKINI WENYE KAZI ZAO HAWAKAMATWI!!NA PIA MWISHO WAKE WA HIZO HABARI ZINAISHIA HAPOX2,HUWEZI KUJA KUSIKIA HUKUMU JUU YA WATU HAO,MFANO MZURI WANGEIGA CHINA WATU HAWA HAWANA MJADALA NI KUUWAWA AU KIFUNGO CHA MAISHA HIVI MTU ANAKUNYA VIDONGE (PIPI)TOKA TUMBONI TENA KWA USHUHUDA WA WATU ZAIDI YA ASKARI MAANA KUNAKUWA NA MADAKTARI UNASIKIA UCHUNGUZI UNAFANYIKA HV KUNACHUNGUZWA NINI KAMA SI RUSHWA?

    ReplyDelete
  3. Inamaana huyu mwandishi wa habari anataka kutuambia kwamba huyu jamaa alikuwa amekodi ndege ya mizigo kwa ajili ya kubeba hizo kilo 810 za madawa??
    Majira mbona mnachakachua tena..Au mnataka kutuambia kuwa hakuna mtu anayepitia (mhariri) hizi habari kuhakikisha kuwa ziko sahihi kabla hazijawekwa hewani??

    ReplyDelete
  4. KWA KIAKILI TUU MWANDISHI KAKOSEA KUNA HAJA GANI KULALAMIKA SAAAANNNNA ALIKUWA NA MAANA YA GRM 800 MAANA KILO 800 NI TANI KASORO KILO 200, MAANA INGEKUWA KILO 800 UNGESIKIA PIA HAPO KWAMBA KIASI HICHO NI KIKUBWA KAMA KILE CHA ...., NK;TUSIPENDE KUWA WAFIFILISHI SANNA KANA CDM

    ReplyDelete
  5. ndio maana tanzania hakuna waandishi wa habari bali kuna makanjanja wa habari si wasomi wa habari za kitafiti na uaangalizi wanakurupuka tu shame on them

    ReplyDelete
  6. Chanzo cha kuaminika kiasi! Police Arrest Four, Seize 81-Kilogrammes of Heroin in Dar es Salaam.
    http://allafrica.com/stories/201103070647.html

    ReplyDelete