LONDON, England
MKURUGENZI wa soka katika timu ya Liverpool, Damien Comolli amesema ukame wa mabao unaomkabili nyota wao wa zamani, Fernando Torres
ndani ya timu yake mpya ya Chelsea ni nafuu kwa upande wao.
Mkrugenzi huyo alisema jana kuwa endapo mchezaji huyo tayari angekuwa amepachika mabao tangu aondoke katika klabu yake, yangeweza kuzungumzwa mengi kuhusu nyota huyo.
Kauli ya Mkurugenzi huyo inadaiwa ni kutokana na Reds kujaribu kujizuia kumuuza mchezaji huyo, wakati wa usajili wa dirisha dogo wa Januari mwaka huu bila mafanikio.
Na kutokana na hali hiyo, Comolli alisema kupitia mtandao wa klabu: "Nafikiri watu wangekuwa na mengi ya kuongeza juu ya Torres kama angekuwa anafunga mabao, lakini ningependa afanye hivyo siku za usoni lakini si kwetu sisi."
Alisema mara zote amekuwa akisema kuwa unapokuwa na mtu ambaye hataki kuwepo kwenye klabu yako halafu ukampeleka mahali ambapo walikuwa wakimuhitaji hali hubadilika.
Mkurugenzi huyo alisema kuwa hali hiyo ni kama kuna mwanga mkali katika anga mpya isiyokuwa na mawingu, tangu siku hiyo, jambo hilo lilipotokea na akasema kuwa lakini limekuwa na mtazamo chanya.
No comments:
Post a Comment