Na Lilian Justice, Morogoro
RAIS Jakaya Kikwete, anatarajia kutoa zawadi kwa washindi wa mbio za Nusu Marathon zilizoandaliwa na mwanariadha bingwa wa mbio hizo Mkoa wa
Morogoro, Christopher Ngao.
Mbio hizo zinazotarajia kutumia sh. milioni tano zitaanza na kumalizikia katika Uwanja wa Jamuhuri mjini Morogoro, zitakwenda sambamba na maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Mei Mosi, itakayofanyika Kitaifa Mkoani Morogoro.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana Mwanariadha huyo, alisema maandalizi ya mbio hizo za kilometa 21 yapo katika hatua za mwisho ikiwa ni pamoja na kutoa tarifa kwa Jeshi la Polisi na watalamu wa kupima umbali.
Ngao alifafanua kuwa chini ya kocha Herman Ndisa na tayari baadhi ya wanariadha mkoani Morogoro wamejitokeza na kuweka kambi katika Milima ya Uluguru ikiwa ni njia ya kuwawezesha kukabiliana na ushindani ulipo kwa wanariadha kutoka Arusha, Manyara, Singida, Dodoma na Kilomanjaro.
"Nawaomba wanariadha wenzangu popote hapa mkoani waje tujifue vyema, ili tuwaoneshe washindani wenzetu kuwa Morogoro si ya kuchezea katika riadha, zawadi zilizoandaliwa hapa zisiondoke," alisema.
No comments:
Post a Comment