Na Zahoro Mlanzi
SIKU chache baada ya serikali kutangaza kuufunga Uwanja wa Uhuru kwa ajili ya matengenezo, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limesema litahakikisha
michezo iliyopaswa kupigwa kwenye uwanja huo, itapigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Taarifa hiyo ya kufungwa kwa uwanja ilitolewa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Emmanuel Nchimbi hivi karibuni jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na gazeti hili Dar es Salaam jana, Ofisa Habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Boniface Wambura alisema watajitahidi timu zinazotumia uwanja huo zimalizie michezo yao kwenye Uwanja wa Taifa.
"Tutahakikisha hilo tunafanya ila kuna mchezo mmoja kati ya JKT Ruvu na Polisi Dodoma, tayari mchezo huo ulishapangwa kupigwa Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga," alisema Wambura.
Alisema michezo ya timu zingine kama Azam FC, Yanga, Simba na African Lyon kuna uwezekano mkubwa wakachezea michezo iliyobaki kwenye uwanja wa Taifa.
Alisema si lazima timu zote zicheze katika uwanja huo kama kuna timu itaona kuna umuhimu wa kucheza nje ya mkoa husika ni bora iwasilishe mapema jina la uwanja watakaotumia.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya Nchimbi, uwanja huo utafungwa kuanzia April Mosi hivyo michezo yote itakayofuata italazimika kupigwa nje ya uwanja huo.
Ratiba ya TFF kwa timu zinazotumia uwanja huo baada ya kufungwa inaonesha kwamba Simba itaumana na JKT Ruvu Aprili 6, African Lyon na Yanga April 7, Azam na Polisi Dodoma April 5 na Simba itaumana na Majimaji Aprili 10.
HAKUNA NJIA MBADALA YA KUPATA ULAJI ILA NI KUUFUNGA HUU UWANJA? MAANA NI JUZI TUU ULIFUNGWA ZAIDI YA MIEZI 3 KWA AJILI YA MATENGENEZO NA HASWA KWA AJILI YA KUAPISHWA RAISI SASA HATA MIEZI MITATU HAIJAISHA UNAFUNGWA TENA KUNANI AU KWA AJILI YA TAREHE 7?MATENGENEZO HAYO NI YA NINI?KULIKONI?
ReplyDelete