Na Amina Athumani
MBUNGE wa Jimbo la Kibaha Mjini, Silvesta Koka anatarajia kufunga mashindano ya Klabu Bingwa ya Ngumi za ridhaa, ambaye ataambatana na Mbunge wa
Jimbo la Kibaha Vijijini Hamoud Jumaa.
Mashindano hayo yatafungwa leo, Uwanja wa ndani wa Taifa, Dar es Salaam ambapo kutakuwa na mapambano kumi ya fainali.
AKizungumza Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Ngumi za Ridhaa Tanzania (BFT), Makore Mashaga alisema fainali za michuano hiyo zitaanza saa tisa alasiri na kuwataka wapenzi na wadau mbalimbali wa mchezo huo kujitokeza ili kushuhudia vipaji vipya.
Alisema kwa ujumla mabondia wote kutoka mikoa 24 ya Tanzania Bara walionesha kiwango cha juu katika michuano hiyo.
"Tofauti na miaka yote ya mashindano haya, mabondia wa Dar es Salaam pamoja na wa Klabu za Jeshi ndiyo waliokuwa wakipewa kipaumbele kwa kuwa walikuwa wakifanya vizuri zaidi, lakini mashinmdano haya tumeweza kushuhudia vipaji vingi zaidi kutoka mikoani," alisema Mashaga.
Alisema baada ya fainali hizo Mbunge Jumaa atakabidhi medali kwa washindi watakaoibuka kidedea.
No comments:
Post a Comment