*Ma-RC sita, Lukuvi kukutana leo Arusha
Na Said Njuki, Arusha
WAKATI msongamano bado ukitishia tiba ya Mchungaji Ambilikile Mwasapile katika kijiji cha Samunge Loliondo wilayani Ngorongoro, wasafirishaji
wamegundua mbinu mpya ya kuficha maiti kwa kuwakalisha vitini na kuwafunika kwa shuka kama wagonjwa mahututi ili kukwepa gharama za usafirishaji maiti hizo.
Habari za uhakika zilizopatika kutoka eneo hilo zimeeleza kuwa wasafirishaji hao wamebuni mtindo huo wa kinyama wa kuchanganya abiria na maiti kwa lengo kusubiriana hadi wapate kikombe cha babu kisha waondoke kwa pamoja kurudi walikotoka huku wakihakikisha maiti hiyo haigunduliki.
Kufuatia hali hiyo abiria hao wanaridhia kitendo cha kuchanganywa na maiti huku wakizuia gari la wagonjwa (ambulance) kwa magogo na mawe linalopita kukagua wagonjwa waliozidiwa ili maiti hizo zisigundulike na timu hiyo ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo.
Akithibitisha matukio hayo jana jijini Arusha, Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro Bw. Elias Wawa Lali alisema hali hiyo inaongeza ugumu wa kutoa huduma hiyo kwa wagonjwa walio mahututi licha ya nia nzuri ya kutekeleza azma ya serikali ya kuhuduma jamii.
“Ni kweli matukio hayo yapo na mbaya zaidi baadhi ya wasafirishaji wamekuwa wakificha maiti zilizokufa katika magari yao kwa lengo la kuwasubiri watu wanaosubiri kupata tiba kwa mchungaji huyo. Jana (juzi) walizuia gari la wagonjwa wakidai linawapeleka kwa babu jamaa na ndugu zao kumbe si kweli, ukaguzi ni sehemu ya kazi yao,†alisema DC Lali huyo.
Alisema kuwa hivi sasa ni wagonjwa watano ndio wameripotiwa kufa lakini huenda wapo zaidi na jitihada zinafanyika kubaini hilo kwani wapo waliokufa kabla ya kupata tiba ya mchungaji huyo na wengine baada ya kupata tiba hiyo.
Maiti hizo zilikuwa hazijatambuliwa na kwamba kamati ya ulinzi ya usalama inaendelea kufanya uchunguzi zaidi juu ya vifo hivyo wakiwa na timu nzima ya kuhakiki usalama wa watu kiafya.
Akizungumzia hali ilivyo, alisema magari imeongezeka kwa kiwango kikubwa na kwamba magari yamefikia kilomita 30 kabla ya kufika kwa babu katika kijiji cha Yasindito hali inayozidisha ugumu wa kudhibiti athari zinazoweza kujitokeza.
Hali hiyo imeonekana kuitisha serikali, hivyo Wakuu wa Mikoa sita inayopakana na Arusha wamelazimika kukutana leo jijini hapa kujadili pamoja na mambo mengine jinsi ya kupunguza idadi ya watu wanaoingia huko kwa kile kinachoonekana ni kushindwa udhibiti wa watu wanaoingia huko licha ya maelekezo kadhaa kutolewa.
Wakuu wa mikoa wanaokutana ni wa Manyara, Singida, Kilimanjaro, Shinyanga, Mwanza, Mara na Arusha kama mwenyeji.
Katika hatua nyingine watu mashuhuri nchini wamezidi kuingia Samunge kupata kikombe kwa babu ambapo Jumamosi imeripotiwa kuwa makamishna waandamizi na makamanda kadhaa wa Jeshi la Polisi nchini walitinga kwa babu kupata kikombe hicho.
Viongozi hao wa jeshi hilo walipata fursa hiyo baada ya kumalizika kwa mkutano mkuu wa watendaji wa jeshi hilo uliofanyika Chuo cha Polisi Moshi hivyo wakaoana watumie furasa hiyo kumfikia Babu kabla hawajarudi katika vituo vyao vya kazi.
Habari zilizothibitishwa kutoka Loliondo zilieleza kuwa makamishana hao walifika Samunge Jumamosi jioni na kujikuta wakilala bila kumwona Mchungaji hadi siku iliyofuata ambapo walipatiwa tiba hiyo na kugeuza huku wakisindikizwa na viongozi wa jeshi hilo wa wilaya ya Ngorongoro.
“Ndiyo tulikuwa na ujumbe mzito wa jeshi hilo lakini idadi na vyeo vyao siwezi kujua…walilazimika kulala kabla ya siku ya iliyofuata walipopatiwa huduma na kuondoka,†alibanisha mtoa habari wetu.
Naye Gladness Mboma anaripoti kuwa DC Lali amesema kuwa wanaangalia uwezekano wa kufunga barabara zinazoingia Kikiji cha Samunge ili kutoa nafasi kwa watu walioko katika eneo hilo kupungua.
Bw. Lali alitoa kauli hiyo jana wakati alipokuwa akizungumza kwa njia ya simu katika kipindi kilichorushwa na Televisheni ya Channel Ten, ambacho pia kilimshirikisha Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mwananyamala, Dkt. Sofinias Ngonyaji.
Alisema kuwa wiki mbili zilizopita msongamano wa magari na wananchi ulikuwa umepungua, lakini kwa sasa magari ni mengi huku msongamano wa watu ukiwa ni mkubwa, jambo ambalo inabidi kuangalia uwezekano wa kufunga barabara zinazoingia kwa mchungaji huyo.
Naye Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mwanyamala, Dkt. Ngonyani aliwataka wagonjwa wote waliokuwa wakitibiwa Mwananyamala na kisha wamekwenda kunywa kikombe cha babu kurudi hospitalini hapo kwa ajili ya kuchukuliwa vipimo vya kitabibu zaidi kuangalia kama wamepona.
"Ninatamani kupata wagonjwa waliokwenda kwa babu kupata kikombe ambao walikuwa wanatibiwa hospitalini hapo ili kuchukua tena vipimo vyao kuangalia kama kweli wamepona, nawaombeni mkirudi msiache kuja hospitali kuendelea na dozi zenu za dawa," alisema.
Dkt. Ngonyani aliwataka pia wagonjwa wengine wa kisukari, kansa na mengineyo wanaokwenda kwa babu kupata dawa nao wasiache kufuata masharti ya dawa na mengineyo kwa kigezo cha kuponyeshwa na dawa hiyo.
Wee acha kwa kuwa tumekubali ujinga wa tiba itokanayo na ndoto ya kibabu kimoja basi tujiandae kuona na kusikia mengi ya ajabu. Naona hata hao wanaofanya hivyo nao watadai wameoteshwa na mungu! Kwa mara nyingine tena nawatonya CHADEMA na Serikali na wale wote wanaojiheshimu kukaa mbali na utapeli huu.
ReplyDeleteWaandishi wa habari; jamani nendeni shule: Umeandika: "..maiti zilizokufa.."Una maana gani?
ReplyDeleteYote haya yanachangia kwamba sasa Taifa letu linayumba.Elimu tumeiweka pembeni na wengi tunaishi kwa kuamini tu. Nabii "Babu" atatuponyesha hata ukimwi. Mungu Ibariki Tanzania.
Viongozi wetu kujadili swala la Loliondo ni kutoa picha gani kwetu? Kwamba sasa hospitali zetu hakuna kitu. Ee Mungu tusaidie na janga hili, akili zetu zimeliwa na nini? Au ndo watu wameshabuni mradi wao? Hapana, hii si haki. So akitokea mwingine Tunduru wote tutaenda huko.
ReplyDeletehebu watanzania tuwe macho jamani haya mwengine katokea Mbeya huyo nae pia anatoa vikombe tena viwili na mwingine atakuja na vikombe vitatu hebu watanzania tuwe macho tujwe dawa zilizopimwa jamamni tuacheni mambo hayo ya enzi ya vita vya majimaji
ReplyDelete