18 March 2011

Mamilioni ya DECI yalikuwa yanatunzwa ofisini-Shahidi

Na Rehema Mohamed

SHAHIDI namba sita katika kesi ya DECI, SP Suleman Nyakulinga amesema fedha zilizokuwa zikikusanywa katika matawi ya mikoani zilikuwa zikihifadhiwa
ofisini.SP Nyakulinga aliyasema hayo jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya hakimu Bw. Stuwati Sanga wakati akitoa ushahidi wake.

Alidai kuwa kutokana na hali hiyo waliwashawishi wakurugenzi wa matawi hayo kupeleka fedha hizo benki na ndipo walipofanikiwa kuzizuia zaidi ya sh. bilioni 12 katika akaunti zilikowekwa.

Fedha zilizozuiwa zipo katika akaunti ya benki ya NMB, Dar es Salaam Comunity Banki, Akiba na CRDB.

Washitakiwa katika kesi hiyo ni Wakurugenzi wa DECI, ambao ni Bw. Jackson Mtares, Bw. Dominick Kigendi, Bw. Timotheo Ole Loitg’nye, Bw. Samwel Mtares na Mhasibu na Msemaji wa kampuni hiyo, Bw. Arbogast Kipilimba.

Vigogo hao wanakabiliwa na mashtaka ya kuendesha na kusimamia mradi wa upatu na kupokea amana kutoka kwa umma bila leseni. Kesi itaendele tena kesho.

No comments:

Post a Comment