18 March 2011

Kundi la walioua polisi lazidi kupukutika

Na Patrick Mabula, Kahama

WATUHUMIWA sita kati ya tisa wa ujambazi wanaodaiwa kuua Askari Polisi wawili katika Kituo Kidogo cha Polisi Kagongwa, wilayani Kahama wamekamatwa
na wananchi katika vijiji mbalimbali na wanne kuuawa kwa kipigo huku wawili wakinusurika lakini hali zao zikiwa mbaya.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Bw. Diwani Athumani alisema jana kuwa watu hao baada ya kuua polisi kituoni hapo walitoroka na kukimbilia sehemu mbalimbali na wananchi walikuwa wakiwatilia mashaka na kuwakamata na kuwashambulia hadi kuwaua baadhi yao.

Mahabusu hao ambao walikuwa 10 katika chumba cha kituo hicho baada ya kuua polisi na kufanikiwa kutoroka na bunduki mbili za askari siku ya Jumanne saa 12:45, kati yao mmoja aliuawa siku hiyo baada ya kukamatwa na wananchi wenye hasira na wengine kufanikiwa kutokomea kusikojulikana.

Bw. Athumani alisema watuhumiwa hao tisa waliokuwa wamebaki wakati wanakimbia kila mmoja alikwenda kivyake vijijini hali ambayo ilifanya polisi kutowa taarifa kwa wananchi maeneo yote na walanza kushirikiana na jeshi hilo kwa kuwasaka na jana alhamisi kufanikiwa kukamata sita kati yao wannne wamewapiga kwa hasira na kuwaua papo hapo.

Alisema katika kushirikiana huko kila mtuhumiwa aliyekuwa akikamatwa vijijini huko na wananchi askari polisi walikuwa wanashindwa kudhibiti hasira za wananchi hao waliokuwa wanawashambulia kwa kipigo.

Kamanda Athumani alisema jeshi lake linafanya jitihada za kuhakikisha maisha ya majambazi hao wawili yanaokolewa ili wapate kuwahoji kupata mtandao mzima ingawa hali zao ni mbaya na hakupenda kuwataja majina yao.

Jumanne watuhumiwa wa ujambazi waliokuwa wamewekwa mahabusu walimteka askari mmoja na kuchukua bunduki yake na kumpiga risasi yeye na mwenzie. Waliouawa ni PC Salum Mwanakatwe na PC Ngwegwe Dira kisha waliporwa bunduki mbili moja aina ya SMG na bastola.

No comments:

Post a Comment