21 March 2011

Madiwani wamshinikiza DED kuwapeleka Loliondo

Na Yusuph Mussa, Korogwe

BAADHI ya Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe Vijijini wamemshinikiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Bw. Lameck Masembejo
kuwawezesha ili kupata tiba kwa Mchungaji Ambilikile Mwaisapile 'Babu', Loliondo.

Akizungumza kwenye Baraza la Madiwani mwishoni mwa wiki iliyopita Diwani wa Kata ya Mkomazi, Bw. Benson Mapanda alisema baadhi ya madiwani wa halmashauri hiyo ni waathirika wa UKIMWI, hivyo ni vizuri wakafika kwa Babu.

"Halmashauri wenyewe walituhamasisha kupima virusi vya UKIMWI, na kweli wengine wetu tukakutwa tumeathirika, sasa tunaomba halmashauri ituwezeshe tufike Loliondo.

"Hata kama halmashauri itasema haina fedha, lakini ituwezeshe magari, halafu sisi wenyewe tutachangia mafuta" alisema Bw. Mapanda.

Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Bw. Sadick Kallaghe alisema halmashauri haina bajeti ya kwenda kwa Babu, lakini akasema ni ruksa mtu binafsi kufika kwa Babu na
kujigharamia mwenyewe.

3 comments:

  1. POLENI MADIWANI MUHIMU NI KUMUHAMASISHA HUYO MKURUGENZI ATOE GARI PAMOJA NA MBUNGE WENU AKUWEZESHENI KUCHANGIA MAFUTA ANZENI WENYEWE KUJICHANGISHA ILI MUPATE KIANZIO ILI MBUNGE NA MKURUGENZI AONE KWELI MNA NIA
    NA WATAHAMASIKA NAWAJUWA HAO NI WASIKIVU NA WANA HURUMA

    ReplyDelete
  2. kwani ni wangapi mmeathirika ili nione jinsi ya kuwasaidia kwa usafiri na malazi

    ReplyDelete
  3. Mbunge wa Korogwe Vijijini Mh. Profesa Maji Marefu a.k.a Stephen Ngonyani hawezi kuwatibia madiwani wake ?

    ReplyDelete