Na Zuhura Semkucha Shinyanga
CHAMA cha Mapinduzi Mkoa wa Shinyanga kimesema kuwa maendeleo ya wananchi hayawezi kuletwa kwa kushinikiza kufanya maandamano na badala yake ni
kufanya kazi kwa bidii ili kujipatika, kipato huku serikali ikifanya juhudi ya kushisha bei ya bidhaa.
Hayo yalisemwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Shinynga, Bw. Hamisi Mgeja alipokuwa anazindua ziara ya chama hicho ambayo itafanyika katika kila kata, Manispaa ya Shinyanga.
Bw. Mgeja alisema kuwa suala la kufanya maandamano wananchi wasiliunge mkono na badala yake wajitahidi kufanyakazi kwa bidii kwa sababu kwenye maandamano hawatapata fedha za kupunguza makali ya maisha.
"Ukienda kwenye maandamano jiulize unaacha shughuli ngani na ukiumia huko nani anakupa fedha za matibabu wale wanakuja na kuondoka tu na si vinginevyo hakuna serikali inayofurahia hali ngumu kwa wananchi wake asikudanganye mtu," alisema.
Pia alisema kuwa kwa wakati huu Serikali ya CCM inafanya jitihada za kuhakikisha kuwa bei ya bidhaa inashuka kulingana na ahadi tulizotoa wakati wa
uchaguzi mkuu na si kwa shinikizo la chama fulani kuandamana.
Aidha alisema kuwa CCM hakipendi kuona wananchi wanataabika kwa sababu ni aibu kwa taifa lingine lolote lile hivyo wananchi waendelee kuwa na imani
na chama hicho kwa sababu ndio chama walichokichagua.
"Hata ndani ya nyumba kukiwa na njaa wazazi wote wawili hawafurahi suala hilo habisa na ukikuta wazazi wanafurahia jambo hilo ujue fika kuwa ni wajinga hivyo ndivyo ilivyo kwa CCM hatufurahii kuona hali hii hata kidogo kwani hata sisi inatuadhiri tu," alisema.
Mwenyekiti huyo alisema kuwa bidhaa zinazolalamikiwa kupanda bei ndio hizo ambazo zinanunuliwa na viongozi na kutumiwa na familia zao hivyo janga hilo ni la wote jambo lililopo sasa ni kuhakikisha kuwa zinashuka bei ili kila mmoja aone matunda ya CCM.
"Sisi bwana hatubahatishi na hatuleti maendeleo kwa sababu ya chama fulani kimeandamana hao walioandamana sisi ndio tumewaleta kwa sababu CCM ndio kina serikali na vyama vingi vililetwa na serikali sasa hapo mnatuona sisi wabaya kweli wananchi msikubali kudanganywa sawa na mgeni anakuja kwako halafu
unataka akutawale inawezekana kweli," alisema.
CCM Mkoa wa Shinyanga imeanza ziara zake katika majimbo yote kwa kupita kata kwa kata ikiwa na lengo la kuwashukuru wananchi kwa kukipigia kura chama hicho.
si kweli! Ingekuwa maandamano hayaleti maendeleo, Mubarak si angekuwa madarakani hadi leo? Kwani nyie CCM maandamano ya CHADEMA, yanawakera nini? Kwani nanyi mmekatazwa kuandamana kama mlivyokatazwa na Makamba wakati wa kampeni kushiriki midahalo ya wazi? Mnaelewa hasa malengo ya chama chochote cha siasa au mnakurupuka tu ili Kikwete awaone mna busara?
ReplyDelete