25 March 2011

Japan yatoa bilioni 46 za umeme

Na Benedict Kaguo

SERIKALI ya Japan imekabidhi msaada wa Yen za Japan bilioni 2.5 (sh. bilioni 46) kwa ajili ukarabati na ujenzi wa vituo vipya vya umeme katika Mkoa wa
Kilimanjaro ili kupunguza makali ya mgawo wa nishati hiyo.

Sambamba na kiasi hicho cha fedha Japan pia imekabidhi kiasi cha Yen milioni 40 (sh milioni 737.2) za upanuzi wa daraja la Rusumo katika mpaka wa Tanzania na Rwanda.

Makabidhiano hayo yalifanyika jana kati ya Balozi wa Japan Bw. Hiroshi Nakagawa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Uchumi Bw. Ramadhan Kijja, makao makuu ya wizara hiyo jijini Dar es Salaam.

Balozi wa Japan Bw. Nakagawa alisema serikali ya nchi hiyo inatambua kuwa umeme ni nishati muhimu katika maendeleo ya Taifa ndio sababu wakaamua kutoa msaada huo ili kuwapunguzia wananchi makali ya nishati hiyo.

1 comment:

  1. Kwenda kwa Mkurugenzi Manispaa ya Ilala.
    Ufisadi huu hadi lini Ofsi ya Maji Ilala.
    Inashangaza kuwa watu wachache ndio wanaokula pesa kizembe tu ofsi ya maji ikiongozwa na Fisadi namba moja Selestina Magesa, na group lake Opitaty Kwembe mtu alie na darasa la kwanza ila wizi anaujua kupta mtu yeyote, pamoja na Wilfred Kavishe, Alex Odena, na Kahema amekuja ofsi ya maji kuja kuiba vzr pesa za miradi ya maji maana kahema na Optaty kwembe ni mahawara waliobobea! Mkurugenzi tunapenda kukutaarifu kuwa pesa ya wiki ya maji haijafaya kazi yoyote kwani baadhi ya madiwani walichoshwa na upuuzi wa viongozi hawa wa ofis ya maji na kususia uzinduzi wa wiki ya maji visima havina ubora na pia miradi mingi ni hewa tunakuomba utoe samaki wabovu ofisi ya maji ili ili kuwasaidia warengwa wa miradi husika. Tunashangaa kuona kuwa huyu kahema kaja kinyemera ofisi ya maji kisa ni mpenzi wa Optaty kwembe tunashangaa pia kuona kisima cha depot kuchimbwa kwa miliion 9 badala ya million 5, na kisima hakina ubora wa utoaji maji ya kutosha pia watumishi hapo depot bwanakosa maji vyooni na hakuna anaelishughulikia swala hili.
    TUTAENDELEA KUKUPA TAARIFA ZAIDI KUHUSU UOZO WAO NA TUNAOMBA UWAKALISHE NA KUWATIMUA IKIBIDI KWANI HAWANA NIA NZURI NA MATAKWA YA SERIKALI ZAIDI YA KUJINUFAISHA WAO TU.

    ReplyDelete