25 March 2011

Watalaamu wa maji wapungua

Na Edumund Mihale

RAIS Jakaya Kikwete amesema iwapo Wizara ya Maji haitachukua juhudi za makusudi za kusomesha watalaamu wake itakumbwa na upungufu mkubwa wa
wataalamu wa sekta ya maji katika siku zijazo.

Akizungumuza katika ziara aliyofanya wizarani hapo Dar es Salaam jana, Rais Kikwete alisema kuwa watalamu waliopo ni wale walichukua kozi zao kwa wakati mmoja na hivyo watastaafu katika kipindi kimoja na kuiacha wizara hiyo ikiwa haina wataalamu.

"Wataalamu hawa waliosoma pamoja na hivyo wataondoka siku moja, bora wangeachiana hata miaka mitano mitano lakini haiwezakani, msipochukua juhudi za makusudi wizara itabaki bila ya wataalama wa sekta ya maji," alisema Rais Kikwete.

Alisema ni vema wizara ikatumia Chuo cha Maendeleo ya Maji ambacho kinatoa elimu ya ngazi ya astashahada kuwawezesha wanafunzi wake kukubalika katika vyuo vikuu nchini ili kuziba pengo hilo.

Akisoma taarifa utekelezaji maagizo ya Rais Kikwete aliyoyatoa 2006 jana, Waziri wa Maji, Prof. Mark Mwandosya alisema wizara yake imeanza kushughulikia changamoto zinazoikabili ikiwemo ya kufundisha watalamu zaidi .

Alisema kuwa imefundisha watalamu wa sekta ya maji kwa kuwajengea uzoefu shughuli ambayo wataalamu wachache wenye uzoefu katika ngazi ya mikoa wilaya na mamlaka ya maji na hata wilayani. 

2 comments:

  1. KWELI KABISA NCHI INAKABILIWA NA UPUNGUFU WA WATAALAMU WA MAJI MAANA HATA YA MVUA HATUWEZI KUYAVUNA MAANA SEHEMU NYINGI ZINGEWEZA KUONDOKANA NA TATIZO LA MAJI. MFANO KWA SASA OFISI YA MAKAMU WA RAISI IMELALA KABISA!!WANAOHUSIKA NA MAZINGIRA MVUA ZINAZO NYESHA HADI SASA MAJI YANAPOTEA BURE HATA WA KUYAFATILIA YAINGIE MTERA HAKUNA MAJI MENGI YANAPOTEA NJIANI,YAMETEGWA NA WAKULIMA NA WAFUGAJI KWA HIYO KWA SASA HAYAIINGII KABISA KATIKA BWAWA HILO,HIVI KWELI HAWA WANAOHUSIKA WANAUMIA NA JAMBO HILI? HAWAWEZI KUJIULIZA IWEJE MAJI MPK LEO HAYAJAONGEZEKA? MAANA MVUA ILIYONYESHA MPK LEO ANGALAU MITA ZINGEZIDI HAPO NI UZEMBE WA WANAOHUSIKA MBONA SIKU ZA NYUMA 2006 JAMBO HILI LA KULINDA VYANZO VYA MAJI LILITILIWA MKAZO? AU WANANGOJA RAISI AENDE WIZARANI AANZE KUWAFUNDISHA KAZI na KUWAKANA NA RIPOTI ZAO UCHWARA?

    ReplyDelete
  2. Juma makonde---- pugu mwakanga.March 25, 2011 at 12:41 PM

    Kwa dar es salam hiyo mikakati ya kuhakikisha wakazi mkoa huo wanaondokanana na tatizo la maji na sisi wakazi wa Pugu tutanufaika na mikakati hiyo? na kama ni ndiyo bombo au mabomba ya maji hayo yataanzia wapi hadi wapi? tujibiwe

    ReplyDelete