25 March 2011

Mwinjilisti ajitokeza kumpinga Magufuli

Na Edmund Mihale

SIKU moja baada ya wakazi wa Shinyanga kumtetea Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Magufuli kuwa anaandamwa na mabosi wake kwa kutekeleza sheria kuhusu
bomoabomoa, mkazi mmoja wa Arusha ameibuka na kupongeza hatua ya Rais Jakaya Kikwete na Waziri Mkuu, Bw. Mizengo Pinda kupunguza kasi ya waziri huyo.

Akizungumuza katika Ofisi za gazeti hili, Mwinjilisiti wa Kanisa la Huduma za Uinjilisti ya Mila na Desturi za Makabila ya mbalimbali, Raymond Kiwale alisema ametoa ujumbe huo kwa niaba ya wenzake 100, kuwa maagizo hayo ya Rais Kikwete na Bw. Pinda yamezingatia utu.

"Magufufuli anatakiwa kukosolewa kwa kubomoa nyumba wanazoishi watu kwa kuwa ni kitendo cha ukatili. Mimi niko katika barabara ya Dodoma-Minjingu, 1987 tulisogezwa mita 15 kila upande tukalipwa fedha za mazao tu bila nyumba.

"Walituambia kuwa suala la nyumba hawana uwezo nalo, bali wanatulipa mazao tu. Nakumbuka mimi nililipwa sh. 40,000 wakati huo zilikuwa nyingi mno nikajenga nyumba nje ya mita hizo.

"Wakaja tena 1997 wakapima mita 22.5 kila upande lakini wakasema kuwa hawalipi fidia kwa kuwa tumevamia hifadhi ya barabara, hivyo hatutalipwa chochote. Akaja Waziri Mkuu wakati huo, Bw. Fredrick Sumaye tukamueleza shida yetu akatumbia kuwa atawaleta watalaamu wa ujenzi lakini nao pia wakatuambia kuwa hakuna fidia kwa kuwa sheria hiyo iko tangu 1932," alisema.
                
Alisema kuwa kwa wamepima tena mita nyingine kufikia 30 na kuwataka kubomoa nyumba hizo, jambo ambalo hawakubaliani nalo, na sasa wanashukuru maamuzi ya 'kumfunga kufuli Magufuli'. 

10 comments:

  1. Magufuli sio katili bali anasimamia sheria iliyopo. Hebu magufuli nakuomba ujiuzuru tu maana hauwezi kufanya kazi na wasanii

    ReplyDelete
  2. Jiuzulu magufuli, achana na hao wacheka hovyo kabisa!

    ReplyDelete
  3. Jamani someni sheria ya barabara ya mwaka 1932.kila kitu kiko wazi humo

    ReplyDelete
  4. Hata akijuuzulu aende zake katili mkubwahuyu asiye na roho ya ubinadamu hata kidogo. Maelezo aliyotoa Rais na waziri mkuu ni sawa kabisa kwani yamezingatia utu. kumbuka barabara hizi hazikubuniwa na magufuli bali serikali ilijenga barabara kwa kufuata mapito ya watu ambao walikuwa wanaishi maeneo hayo tangu ukoloni. sheria ya mwaka 1932 inaseaje? nani anaijua? kama haikufungiwa kwenye makabati na hao walioitunga. kwanza sheria hiyo ilikuwa ni ya ukolono ambao wakoloni walitengeneza barabara kufuata watu walipo na walipozoea kupita. kwani sheria hiyo inasema ni mita ngapi. kuna mapungufu mengi hapa. Hivi sasa kuna sheria ingine mpya sijui ni ya mwaka 1999 au hivi karibuni zaidi inayotaka upana wa barabara uwe mita 60 badala ya wa sasa wa mita 45. Sasa mwaka kesho wakijenga barabara wale walio nje ya mita 45 wataambiwa waondoke na nyumba zao zitabolewa tena bila fidia kama anavyofanya huyu mtu wenu. Mh. Rais kumtaka atoe maamuzi kuzingatia halihalisi si kumdhalilisha kama wengi mnavyodai ni kumkumbusha pia kuwa hao anaowanyia jeuri ya namna hiyo ndio waloweka serikali hapo ili iwasidie na si kuwatesa. Magufuli anaona kazi kubwa huko ujenzi ni kubomoa nyumba za wananchi tu. Hakuna serikali duniani inayoendeshwa kwa staili hii hata kidogo huu ni ubabe uliopitiliza. Leo kuna watu na akili zao wanamsifu mtu stupid wa namna hiina kumshabikia ajiuzulu. YES kama anaona hajatendewa haki aende " GENDA MAGUFULI" we don't care. kwani unasaidia nini zaidi ya kutes wananchi maskini ambao kujenga nyumba hizo walijinima na watoto wao kupata mahali pa kujisetiri. Think abou that urais hauwaniwi kwa staili hiyo. KWENDA HUKO go to hell

    ReplyDelete
  5. Kwa kweli staili ya Rais kukosoa mbele ya halaiki watendaji katika baraza lake la Mawaziri Kunaweza leta athari kubwa mno huko mbeleni katika utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya chama chake.
    Kufanya hivyo kunavunja ari ya utekelezaji wa ilani hiyo miongoni mwa watu alio waamini na kuwapa jukumu hilo.
    Kwa kifupi, achague namna sahihi ya kuwashauri na si kutafuta sifa kwa wananchi kwa kujifanya mfuatiliaji kumbe anajiharibia mwenyewe.
    Mimi binafsi namkubali na nazikubali shughuli za Mh Maghufuli za kiutendaji na napinga vikali wale wote wanao endekeza siasa bila kujali utekeleji wa majukumu magumu kama aliyo pewa Maghufuli ambayo yataleta tija kubwa hasa kwa kizazi kijacho.
    Mh Maghufuli nakushauri uyatupilie mbali mawazo ya hao mangwine na uchape kazi kama ulivyo panga vinginevyo waachie wafanye wenyewe. Naamini kwa majukumu uliyo nayo endapo siasa itahusishwa sana, ifahamike kuwa utekelezaji utachukua muda mkubwa mno.

    Hivyo napenda kuwa wazi kwamba nikokinyume kabisa na mbinu wanazotumia hawa viongozi wa juu wa tz kushauri watedaji wao maana ni kinyume kabisa na kanuni za uongozi bora!
    Kwa hayo machache, naomba kuwasilisha.

    ReplyDelete
  6. Magufuli ni mtu katili, leuri, thalimu, mnyanyasaji, dikteta na muuaji mkubwa sana tena malipo yake inafaa anyongwe hadi kufa. Huwezi mtu mwenye akili timamu ushindwe kwa akili kidogo tu kama ya panya kuelewa kwamba barabara hii au ile imepandiashwa daraja wakati watu wakiwa wameshajenga nyumba zao wewe unawavunjia eti kisa unatekeleza sheria, huu ni unyama ni lazzima ukomesha. Hizo sheria anazitekeleza kwenye kubomolea watu nyumba zao tu mbona kipindi cha kuuza nyumba za serikali alivunja sheria hata kuwauzia malaya zake wanafunzi wa chuo kikuu ambao hawakuwa hata wafanyakazi wa serikali.nashauri hata akijiuzulu asipate nafasi kuhamia chama kingine chochote arudi chato akalime maboga

    ReplyDelete
  7. Mheshimiwa Magufuli, hivi kwenye wizara yako hakuna kitu kingine cha kufanya isipokuwa kuvunja nyumba zilizoko kwenye hifadhi ya barabara?Naamini ziko kazi tele!Kama wakubwa zako wanakuzuia kuzivunja nyumba, wewe tunga jambo lingine la kufanya na uwaache wakae wanavyotaka.Wewe hujui hizo petrol station na mahoteli na majumba unayotaka kuvunja ni yao au washikaji wao?Jua kwamba inji hii ukijifanya kuchunga sheria utaumia. Hizi sheria zinatungwa ili zivunjwe na sio zitunzwe.Achana nao.Badala yake Imarisha karakana za ujenzi(TEMESA), Vivuko,Majengo nk.Hao wanaotaka ubinadamu waendelee nao halafu siku ya kudaiwa ahadi walizotoa usikie watasema nini.
    Nchi zote duniani zilizoendelea zilipata maendeleo kwa kutumia sheria walizojitungia na mara nyingine kutumia UBABE katika kusimamia sheria hizo na sio ubinadamu na unafiki wa kuongoza.Kwa staili hii HATUFIKI! Bw Magufuli wewe usijiharibie CV yako.Ni bora ukatekeleza mambo niliyoyataja hapo juu, na ukiona wanakuzuia uachane nao ubakie mbunge wa Chato na heshima yako ibakie. ukicheza watakuzamisha wakuache huko!Angalia na uchunge sana hapo umekalishwa kwenye kuti kavu.Wasalaam.

    ReplyDelete
  8. Magufuri hana kosa kusimamia sheria zilizopitishwa na Bunge na kusainiwa na rais. Rais alimwapisha Magufuri kusimamia sheria hizo. Kwanini wanamfunga luku? Makosa ni ya Kiwete na Punda na siyo Msuguri

    ReplyDelete
  9. Kaka Magufuli pombe ukitaka kuwapatia hao wasanii nakuomba ugombee urais mwaka 2015, alafu tunafunga wote wasanii, mimi mmoja kati ya hao tutakaokupa kula

    ReplyDelete
  10. Magufuli anataka Urais lazima watu wabomolewe nyumba kila kona

    ReplyDelete