21 March 2011

...Dawa ya Babu yamchanganya Mtikila

Na Gladness Mboma

HUDUMA ya uponyaji inayoendeshwa na Mchungaji Ambilikile Mwaisapile maarufu kama Babu imeendelea kuwachanganya baadhi ya viongozi wa dini, wa
karibuni kabisa akiwa Mchungaji Christopher Mtikila ambaye ameiponda na kuwaponda waotumia dawa hiyo kutibu maradhi mbalimbali.

Licha ya Mchungaji Mtikila kukiri mbele ya waandishi wa habari jana kuwa dawa hiyo inaponya, ameiponda na kudai kuwa hakuna jipya linaloendelea huko Loliondo.

Tangu Mchungaji Mwaisapile aanze kutoa huduma ya dawa hiyo ambayo inadaiwa kutibu magonjwa sugu baadhi ya viongozi wa dini, akiwamo Kiongozi wa  Full Gospel Bible Fellowship Askofu Zachary Kakobe wamekuwa wakitoa kauli mbalimbali za kupinga huduma hiyo inayokimbilia na maelfu ya watu wa ndani na nje ya nchi.

Akizungumzia tiba hiyo, Mchungaji Mtikila jana alitoa mpya pale aliposema 'hata vikombe vinavyotolewa kunywea dawa hiyo ni vya rangi ya kijani na njano, hivyo akadai kwamba hiyo ni zindiko la CCM'.

Hata hivyo, vikombe vinavyotumika ambavyo hata mwandishi wa habari hizi aliviona baada ya kufika Liliondo vina rangi mchanganyiko wa wa rangi, vikiwamo vyekundu, vyeupe, blue, kijani na njano.

Mchungaji Mtikila pia alisema kwamba Loliondo hakuna neno la Mungu, bali ni 'machemsho ambayo wananyeshwa watu bila imani katika Kristo'.

"Nakiri kwamba dawa za huyu Mchungaji zinaponya na ndio maana watu wengi wanakimbilia huko kutokana na nchi kutokuwa na uongozi halali," alisema Mchungaji Mtikila.

Alisema kuwa kama ungekuwepo uboreshaji wa huduma za afya na tiba ya bure kwa walalahoi mpaka vijijini watu wasingeacha makanisa na kuelekea Loliondo.

Mchungaji Mtikila aliwaponda pia viongozi mbalimbali waliokwenda Loliondo kupata huduma hiyo ya dawa kwa madai kwamba tiba hiyo imethibitisha kuwa 'nchi inaongozwa na waathirika wa magonjwa sugu wasioweza kuzingatia mipango ya muda mrefu ya Taifa kwa sababu wanaishi kwa matumaini'.

5 comments:

  1. mtikila na kakobe wakae kimya,huo ni wivu tu hawana lolote je wangekuwa wenyewe ndo wamepewa bahati hiyo nazani hata sh.500 kwao ingekuwa laki,mtikila siasa imemshinda.

    ReplyDelete
  2. Mtikila anasumbuliwa na ugonjwa wa wivu na ujinga.Ndio maradhi ya nayo msumbua mtikila ninamwomba akapewe kikombe cha babu

    ReplyDelete
  3. kwahiyo babu wa Loliondo ana mjukuu kule Rombo sasahivi! na kwanini wa rombo amezuiwa lakini babu hawajamzuia?

    nchi ya tz inasifika kwa kutegemea ushirikina, hii ni aibu!

    ReplyDelete
  4. Pumbavu wewe Mtikila tena shetani wa miguu mia. Sisi tunakunywa dawa na tunapona, nini wewe mwizi wa sadaka kanisani. Hukuwa na ajira ya kukuingizia kipato wewe na familia yako, sadaka imekusaidia sasa unajitapa nini na uchungaji wako feki uliojaa majungu kwa viongozi wa nchi na fitina zako ndiyo maana unafungwa jela kila mara mjinga wewe.Ndiyo maana unakuja kanisani kuhubiri ukiwa umevaa hirizi ili watu watoe sadaka kwa wingi. Una majungu kiasi kwamba huwezi hata kupata usingizi ukifikiria kesho utapika jungu gani na kwa nani. Unamponda Babu, unawaponda wanao kunywa dawa, unazua juu ya rangi za vikombe, kama wewe si mchawi, ulijuaje juu ya rangi hizi? Jee, Nyumbani kwako, mashuka, mapazia, sahani, bakuli, makochi na vitanda na meza na makabati na vikombe ni vya rangi moja?? Acha unafiki wako tunakujua sana na ujinga wako. Uponde, usiponde, na sisi pia tuliokunywa dawa tunakuponda wewe na mpumbavu mwenzio Kakobe, wezi watupu na wachawi na wafitina wakubwa nyie. Acheni majungu yenu ya kishenzi, Kwani pameandikwa wapi kwenye Biblia kwamba Mtikila na Kakobe tu ndio wenye kupokea maono toka kwa Mungu? Kakobe na Mtikila ndio Manabii wasafi wanao stahili kupewa sadaka kwa kutumia mahirizi yao yaliyo mifukoni??? Ushindwe kwa jina la Yesu wewe Mtikila shetani mkubwa.

    ReplyDelete
  5. Habari za chini kwa chini zinasema kuwa, baadhi ya wachungaji wamekuwa na wasiwasi kuhusu huduma ya Babu Mwasapile wakiamini kuwa, kama ushuhuda wa watu kupona utakuwa mkubwa, wao hawana chao kwa vile wameshawaombea sana watu lakini matatizo yao yako pale pale.
    Wakati huo huo, kuna ushahidi wa kutosha kuwa, baadhi ya waumini walio kwenye foleni ya kufika kwa babu kupata kikombe wamekuwa wakitoa ushuhuda namna walivyoombewa katika makanisa ya kilokole lakini bila mafanikio na ndiyo hao hao sasa wanalalamika juu ya babu huyu.
    “Hofu ya wachungaji hao ipo kwenye vituo vyao vya maombezi vilivyofurika mjini, wakati huu vitabaki tupu, watu wanakwenda Loliondo na hawatasubiri tena maombezi.”
    Kauli za wachungaji hao ni ishara kwamba, hakuna mwananchi anakayeweza kusubiri muujiza wa kupona ugonjwa kwa kutumia maneno ya jukwaani wakati kuna babu Loliondo anatibu bila mahubiri ya muda mrefu

    ReplyDelete