28 March 2011

David Villa ainusuru Hispania kufungwa

GRENADA, Czech

MSHAMBULIAJI David Villa, juzi aliinusuru timu yake ya Hispania kufungwa na pia kujiwekea rekodi ya kufunga mgoli mengine katika kampeni ya kuwania kufuzu
Euro 2012, kwenye mechi dhidi ya Czech iliyochezwa mjini Granada.

Shuti la mbali la Jaroslav Plasil, liliipatia timu ngeni bao la kuongoza katika dakika ya 30 kwenye mechi hiyo ya Kundi I.

Kipindi cha pili Villa alimiliki mpira kisha kumfunga kipa wa Chelsea, Petr Cech kwa shuti la chini na baadaye alikuja kufunga bao jingine kwa penelti.

Katika mechi zake 72 alizochezea timu ya taifa ya Hispania, Villa amefunga mabao 46 ikiwa ni mawili zaidi ya Raul.

Mchezaji huyo wa zamani Real Madrid ametumia dakika 102 kufunga mabao 44 katika timu yaHispania lakini, Villa amefunga mabao 46 katika mechi 72.

Ushindi huo wa Hispania ambao umefanya kufikisha pointi 12 katika mechi nne, umeifanya Hispania kuwa na rekodi ya ushindi kwa asilimia 100 kama ilivyo Uhoalanzi ambayo nayo ilishinda mabao 4-0 dhidi ya Hungary ukiwa ni ushindi wao wa tano katika kampeni ya kuwania kufuzu Euro 2012 Kundi E.

Rafael van der Vaart, ndiye alianza kuwafungia bao Uholanzi dakika ya nane ambao ni washindi wa pili katika fainali za Kombe la Dunia 2010 kisha,Ibrahim Afellay aliongeza bao la pili kabla ya mapumziko.

Dirk Kuyt alivunja mtego wa kuotea wa Hungary na kufunga goli na kufanya matokeo kuwa 3-0, huku Robin van Persie akifunga karamu ya magoli dakika ya 62 kwa kufunga bao la nne.

Italia imechukua uongozi katika Kundi C, baada ya kuilaza Slovenia bao 1-0 katika mechi iliyopigwa mjini Ljubljana, bao lake pekee liliwekwa kimiani na Thiago Motta dakika ya 73.

Patrice Evra alirejea katika kikosi cha Ufaransa, baada ya kufungiwa mechi tano na kuisaidia timu yake kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 katika Uwanja wa Barthel dhidi ya Luxembourg.

No comments:

Post a Comment