08 March 2011

Aua mke kwa kumkata na jembe

Na Suleiman Abeid, Shinyanga

JESHI la Polisi Mkoani Shinyanga linamsaka mkazi wa Kijiji cha Bunonga wilayani Shinyanga anayetuhumiwa kwa kumuua mkewe kwa kumkata na  jembe
kichwani na kufa papo hapo.

Kaimu Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Shinyanga, Bw. Justus Kamugisha alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 10.00 jioni katika kijiji cha Mwamala wilayani Shinyanga ambapo amemtaja mtuhumiwa anayesakwa kuwa ni Bw. Masanja Manoni mkazi
wa Bunonga.

Bw. Kamugisha alisema chanzo cha mauaji hayo kinatokana na ugomvi wa kifamilia kati ya Bw. Manoni na mkewe Bi. Dotto Luhende hali ambayo ilisababisha mke kukimbilia ukweni kwa wazazi wa mume kutafuta usuluhishi.

Alisema baada ya Bi. Dotto kukimbilia ukweni, Bw. Manoni aliamua kumfuata huko ambako wazazi walijaribu kuwasuluhisha lakini hata hivyo hawakupa muafaka hali ambayo haikumfurahisha mume.

Bw. Kamugisha alifafanua kuwa kutokana na kushindikana kwa suluhu kati ya wanandoa hao wawili ndipo Bw. Manoni alipochukua uamuzi wa kukatisha maisha ya mkewe ambapo aliamua kumkata na jembe kichwani na akafa papo hapo
na yeye mwenyewe kutoroka.

No comments:

Post a Comment