Na Waandishi Wetu
ASKOFU Mkuu wa Kanisa la Moravian Tanzania, Alinikisa Cheyo amewaonya viongozi wa dini wanaojiita mabingwa wa uponyaji wanaoponda matibabu wa
mchungaji Ambilikile Mwasapile wa Kijiji cha Samunge, Loliondo wilayani Ngorongoro na kuwataka kuacha tabia ya kukaa kwenye maombi ili Mungu awajibu.
“Unajua mambo ya Mungu si siasa na wala haitatokea kuwa siasa hasa mtu akisema mwenyewe kuwa amepewa uponyaji huo na Mungu unaposimama kumpinga maana yake ni kuwa unatangaza vita na Mungu aliyempa unabii huo," alisema.
Akihubiri katika ibada maalumu katika Ushirika Mkubwa wa Itili wa kanisa hilo jijini Mbeya, Askofu Cheyo alisema kuwa amepata kigugumizi cha kuzungumzia suala hilo tangu lianze kutokana na uzito wake na kwa kutambua kuwa yeye anaheshimu sauti ya Mungu anapoamua kumtumia mtu.
Alisema kuwa Mungu anapoamua kuleta ukombozi kwa wanadamu haangalii umaarufu wa mtu ili amtumie bali anachoangalia ni unyenyekevu wake kuona kama ataweza kubeba unabii anaompa kwa ajili ya kuwasaidia watu wake.
Askofu Cheyo alisema kuwa jambo la msingi la kuzingatia watu waache kumwangalia mchungaji Mwasapile binafsi bali wamwangalie Mungu anayesema ndiye aliyempa ufunuo wa dawa hiyo kisha ndiye atakayewaponya kutokana na imani yao.
Alishangaa kuona viongozi wa dini kuanzisha malumbano kuhusiana na jambo ambalo mhusika anayelifanya amesema wazi kuwa ni ufunuo kutoka kwa Mungu hali ambayo alisema kumpinga ni kuonesha ubinafsi na kutafuta umaarufu usio na maana.
Kiongozi huyo alisema kuwa huu si wakati wa kutafuta umaarufu na kulumbana wakati Watanzania wanahitaji jibu la matatizo yao, sasa wameona kuwa limepatikana Loliondo ambako hata hivyo alisema
lazima wamtangulize Mungu.
Alisema kuwa Watanzania na watu wengi kutoka nje ya nchi wanapaswa kwenda kupata dawa na mti huo wakiwa wameweka imani yao kwa Mungu na kuamini kuwa baada ya kunywa tu watakuwa wamepona magonjwa yao tofauti na hivyo dawa hiyo haiponyi bila Mungu.
“nawambia ndugu zangu katika siku za sasa watu wamekuwa wakiamini sana habari ya Loliondo na kila leo kumekuwa na taarifa za Loliondo , mimi nasema kuwa kinachoponya ni imani ya mtu anayekwenda huko na bila imani atakuwa amepoteza muda kwani mchungaji Mwasapile anamtegemea Mungu,†alisema.
Aliwaonya 'wanaoiba' wagonjwa mahututi ambao hawajiwezi kutoka hospitalini kuwa kufanya hivyo ni kuwalazimisha wagonjwa hao wapone huku wao wakiwa hawajasikia habari za Loliondo, kutokana na ukweli kuwa imani huja baada ya kusikia na kuona.
“Acheni kuwatorosha wagonjwa mahospitalini walio mahututi ambao kwa kweli hawajitambui, wataishia kufia njia bila ya hata kufika kunywa dawa hiyo ambayo msingi wake mkubwa ni imani ya mtu anayekwenda kunywa na anaanza kupona tangu akiwa njiani," alisema.
Askofu Laizer naye akerwa
Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Kati, Thomas Laiser amewataka ‘wanaochonga’ juu ya tiba hiyo wafunge midomo yao badala ya kuzuia watu wasikimbilie huko.
Alisema kuna baadhi ya watu wasiowatakia mema binadamu waliopewa
karama na Mwenyezi Mungu na kutoa kauli za kejeli kama inavyotokea kwa mchungaji huyo, jambo ambalo si zuri kwani watu wanachofuata si kuzuia kifo bali kupunguza maumivu wanaoyopata kutokana na kusumbuliwa na magonjwa sugu kama sukari kwa muda mrefu.
“Mtu kama anayo mashaka na tiba ya Mchungaji Mwasapile afunge mdomo wake siyo kuzuia watu kufuata tiba. Tunachoamini tiba hiyo ina mahusiano makubwa na imani na maombi, na katika maombi kuna kukubaliwa mapema, baadaye na maombi mengine kukataliwa kabisa…lakini wengi wameshuhudia kupona sukari na shinikizo la damu,†alisema Askofu Laiser wakati akizungumza na gazeti hili
jana.
Alisema bahati mbaya idadi kubwa tu ya wagonjwa wanatoroshwa hospitalini wakiwa mahututi na kukimbizwa kwa mchungaji huyo na kukumbana na matatizo mengi yakiwemo safari ndefu katika barabara mbovu, hivyo kupoteza nguvun nyingi.
“Mambo ya Kimungu ni ya Mungu ni vigumu kuyabadilisha kibinadamu, nimekuwab nikipata simu nyingi toka Rwanda, Uganda, Burudi na kwingineko kuomba mchungaji Mwasapile kubadilisha kituo cha huduma, nawajibu kuwa haiwezekani kwani ni suala la kiimani na maombi…hata mchungaji mwenyewe alipenda kutoa tiba hiyo Babati mkoani Manyara alikataliwa,†alisisitiza Askofu Laiser.
Ajibu swali iwapo mti anaotumia kama dawa ya tiba hiyo ukimalizika katika maeneo hayo hawezi kubadilisha kituo, Askofu alisema kwa mujibu wa mchungaji huyo akiba ya dawa hiyo ipo ya kutosha na hawatarajii kwisha katika siku za karibuni.
...Dawa ya Babu yamchanganya Mtikila
Huduma ya uponyaji inayoendeshwa na Babu imeendelea kuwachanganya baadhi ya viongozi wa dini, wa karibuni kabisa akiwa Mchungaji Christopher Mtikila ambaye ameiponda na kuwaponda waotumia dawa hiyo kutibu maradhi mbalimbali.
Licha ya Mchungaji Mtikila kukiri mbele ya waandishi wa habari jana kuwa dawa hiyo inaponya, ameiponda na kudai kuwa hakuna jipya linaloendelea huko Loliondo.
Tangu Mchungaji Mwaisapile aanze kutoa huduma ya dawa hiyo ambayo inadaiwa kutibu magonjwa sugu baadhi ya viongozi wa dini, akiwamo Kiongozi wa Full Gospel Bible Fellowship Askofu Zachary Kakobe wamekuwa wakitoa kauli mbalimbali za kupinga huduma hiyo inayokimbilia na maelfu ya watu wa ndani na nje ya nchi.
Mchungaji Mtikila jana alitoa mpya pale aliposema 'hata vikombe vinavyotolewa kunywea dawa hiyo ni vya rangi ya kijani na njano, hivyo akadai kwamba hiyo ni zindiko la CCM'.
Hata hivyo, vikombe vinavyotumika ambavyo hata mwandishi wa habari hizi aliviona baada ya kufika Liliondo vina rangi mchanganyiko wa wa rangi, vikiwamo vyekundu, vyeupe, blue, kijani na njano.
Mchungaji Mtikila pia alisema kwamba Loliondo hakuna neno la Mungu, bali ni 'machemsho ambayo wananyeshwa watu bila imani katika Kristo'.
Mchungaji Mtikila aliwaponda pia viongozi mbalimbali waliokwenda Loliondo kupata huduma hiyo ya dawa kwa madai kwamba tiba hiyo imethibitisha kuwa 'nchi inaongozwa na waathirika wa magonjwa sugu wasioweza kuzingatia mipango ya muda mrefu ya Taifa kwa sababu wanaishi kwa matumaini'.
Na Gladness Mboma, Dar; Charles Mwakipesile, Mbeya; na Said Njuki, Arusha
nashukuru askofu kwa kumsapoti mchungaji wa loliondo,kwani mtikila na wenzake hawana jipya ndo maana hata siasa imemshinda naomba na yeye akapate kikombe ili kimsaidie akili yake ikae sawa.
ReplyDeleteHata Bwana YESU hawakumkubali,so its natural tusishangae kwa wasioamini
ReplyDeleteNashangaa sana viongozi wenzangu zaidi wa kipentekoste wanaoipinga dawa hii. Mungu ametenda neno kuu sana. Mimi ninamshukuru Mungu na kumwombea mchungaji huyu aendelee vyema. Ninasikitika pia watu wanaokwenda kunywa dawa na wakirudi wanamsema vibaya Mchungaji "eti ni mganga" badala ya kumshukuru Mungu na kutoa ushuhuda wa kumtukuza Mungu. Hii ni mbaya sana.
ReplyDeleteMchungaji Pentekoste
Bado nasisitiza huu nu utapeli. yaani dunia yote mungu akaona ashushe neema Loliondo! Mtaingia aibu ya mwaka wote mnaoshabikia ujinga huu. babu chuma njuluku haraka haraka kabla hawajashtuka wakosa akili hawa. manataka kutuambia mnajenga hospitali na zahanati za nini kama kuna tiba za miujiza namna hii? Bomoeni Bugando, KCMC, Peraamiho, Hindu Mandal, Agha Khan, n.k. Acheni ushabiki wa kizamani. Ngoja waliotibiwa waanze kufa ndio babu atatolewa nduki hapo Loliondo. Shenzy kabisa nyie
ReplyDeleteMujahidina bwana hawana manufaa yeyote. Wao ni kujilipua tu na kutukana.
ReplyDeleteWanapigania sharia ili wakate watu viungo. Lakini watu wagonjwa wakiponywa wanakasirika na kutukana matusi.
Wamejaa mapepo ya mauti. Muda wote wanawaza majambia na jinsi ya kuunganisha mabomu.
Wacheni Mchungaji atusaidie. Nyie endeleeni na semina zenu za namna ya kuuwa watu wengi kwa mpigo (mauaji ya halaiki/kimbari) ndio fani yenu. Kwa sababu hamna uwezo wa kuleta jambo lolote zuri duniani.
Mchungaji endelea na matibabu ya halaiki.
Nadhani sasa wananchi wameona umuhimu wa kuwa na uwiano wa maendeleo kwa nchi hii badala ya kukazania Dar-Kilimanjaro.
ReplyDeleteHebu fikiria, kama barabara ya Serengeti inayopendekezwa ingekuwa imejengwa, wagonjwa wetu wasingetaabika kama ilivyo sasa.
Tunawaomba wale wooote wanaoendeleza LONGOLONGO na kupinga ujenzi wa barabara ya Serengeti walegee na washindwe. Upinzani wao sio kuwa wanapenda sana wanyama wa serengeti, bali hawapendi maendeleo yawafikie watu wa serengeti na ngorongoro.
Napenda kuwajulisha viongozi wetu wa kitaifa kuwa wamechelewa sana kujenga hii barabara. Uingereza, Ujerumani, Kenya, nk wanapata watalii wengi kuliko serengeti. Je barabara zipo au hazipo kwenye vivutio vyao vya kitalii??
Mwenyezi Mungu hajaribiwi wala hadhiakiwi.
ReplyDelete