16 March 2011

Arsene Wenger amkumbuka Lehmann

LONDON, Uingereza

KOCHA Arsene Wenger wa Arsenal, ameamua kumfuata kipa wake mkongwe wa zamani Jens Lehmann. Kipa huyo aliyestaafu wa Ujerumani mwenye umri
wa miaka 41, ambaye hapatani na kipa wa Emirates, Manuel Almunia.

Anamtaka ili kusaidia timu ambayo ina tatizo la mlinda mlango, kutokana na kuumia kwa makipa wake Wojciech Szczesny na Lukasz Fabianski.

Kitendo cha Wenger kumrudisha Lehmann, kinaweza kuwashangaza mashabiki wa klabu hiyo.

Lehmann alikuwa Arsenal kwa miaka mitano, kabla ya kuondoka kwenda Stuttgart mwaka 2008 baada kuzozana na Almunia. Aliamua kustaafu soka katika majira ya joto yaliyopita.

No comments:

Post a Comment