24 February 2011

Washambuliaji wampa imani Ancelotti

COPENHAGEN, Dernmark

KOCHA Carlo Ancelotti, anaamini ushindi wa Chelsea wa mabao 2-0 dhidi ya timu ya FC Copenhagen, umethibitisha kuwa washambuliaji wake wanaweza
kuifikisha mbali timu hiyo katika michuano ya Klabu Bingwa Ulaya.

Baada ya mwishoni mwa wiki iliyopita timu hiyo kutupwa nje ya michuano ya Kombe la FA dhidi na Everton, alikuwa ni mchezaji Nicolas Anelka ambaye alimpa raha kocha wake, Ancelotti baada ya kuipachikia mabao mawili timu yake yaliyoiweka Chelsea katika mazingira mazuri ya kutinga hatua ya robo fainali ya michuano hiyo ya Klabu Bingwa Ulaya.

Kipigo katika mchezo huo kutoka kwa timu hiyo ya Denmark, katika mchezo huo wa kwanza wa hatua ya 16 bora ambao ulifanyika kwenye Uwanja wa Icy Parken ingesababisha madhara kwa kocha Ancelotti, ambaye yupo chini ya shinikizo kali, lakini mabao yaliyopachikwa na Anelka yakamthibitishia Muitaliano huyo kutokuwa na cha kuogopa kuhusu hatima yake katika klabu hiyo.

Katika mchezo huo, Ancelotti aliamua kumpumzisha Didier Drogba kwenye benchi wakati akitumia mfumo wa  4-4-2 huku, Anelka na Torres wakisimama katika nafasi ya ushambuliaji ambapo, Anelka alionesha uwezo wake kwa kupachika mabao mawili.

Mabao hayo yamfanya msimu huu kufikisha saba kutoka mechi sita alizocheza kwenye mashindano hayo ya Ulaya huku, Torres naye akikaribia kuondoa wingu jeusi tangu ajiunge na timu hiyo akitokea Liverpool.

Drogba amekuwa na kiwango katika siku za hivi karibuni, lakini hata hivyo halalamiki kusugua benchi na  Ancelotti, anasisitiza kuwa nyota huyo amekuwa hataki kulalamika kuhusu kupumzishwa kutokana na kuwa anatakiwa kupumzishwa ili aweze kuendelea kuwa fiti katika michuano ya Klabu Bingwa Ulaya.

Alipohojiwa na kaka mchezaji huyo bora barani Ulaya, Ancelotti alisema: "Ndiyo, nadhani ndiyo hivyo. Tunataka kuendelea kutunza kiwango chake, lakini kubadikishana itakuwa ni vizuri zaidi kwake katika michuano ya Ligi Kuu na Klabu Bingwa."

"Wanakulabiliana na uamuzi wangu bila matatizo na jambo hili ndilo la msingi. Kuwa nao wote katika kipindi hiki ni muhimu kwa wakati huu," aliongeza kocha huyo.

Alisema kwa sasa ana washambuliaji hatari, hivyo anapaswa kuwa na maamuzi wakati wa kuwachezesha kulingana na mechi.

"Didier alicheza saa mbili dhidi ya Everton. Torres na Anelka nao walikuwa fiti kwa pamoja wanacheza vizuri," alisema kocha huyo.

Licha ya Torres kutofanikiwa kufunga wakati alipopata nafasi nzuri tatu, Ancelotti anasema mshambuliaji huyo wa timu ya taifa ya Hispania, mwenendo na kujituma kwake vinamfanya akaribie kupata fursa hiyo ya kuzifumania nyavu.

Katika mechi hizo zilizofanyika usiku wa kuamkia jana, Real Madrid ilishindwa kutamba tena mbele ya timu ya Lyon katika michuano ya Klabu Bingwa Ulaya, baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1.

No comments:

Post a Comment